Mshambuliaji Mbrazil, Neymar da Silva Santos Junior, maarufu tu kama Neymar akishangilia baada ya kuifungia mabao matatu Paris Saint-Germain dakika za 20, 22 na 81 katika ushindi wa 6-1 dhidi ya Red Star Belgrade kwenye mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Ufaransa. Mabao mengine ya PSG yamefungwa na Edinson Cavani dakika ya 37, Ángel Di María dakika ya 41 na Kylian Mbappe dakika ya 70
No comments:
Post a Comment