Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi mjini Morogoro juzi, lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu na watoto mkoani humo .
Washiriki wa kongamano hilo.
Kongamano likiendelea.
Mtoa mada Mogani Isdori akitoa mada kuhusu ulipaji kodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akitoa mada kuhusu matumizi ya mitandao.
Mwanachuo cha Jordan cha mjini Morogoro, Aviva Chrispin akiuliza swali.
Mjasiriamali, Neema Heri akitoa ushuhuda wa mafanikio yake.
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, Dk.Suleiman Rashid akitoa mada kuhusu umuhimu wa vifungashi kwenye Tangaza na kuongeza thamani ya bidhaa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo akizungumzia umuhimu wa vifungashio na kuongeza thamani ya bidhaa.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa kongamano hilo, DC Mchembe pamoja na watoa mada.
Mjasiriamali, Sara Ngonyani akitoa mada.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akimkabidhi zawadi ya saa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF, Mwajabu Dhahabu akimkabidhi zawadi ya picha baba yake Mzee Dhahabu.
Picha ya pamoja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki katika kongamano hilo.Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF.
WANAWAKE nchini wametakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu na wabunifu ili waweze kuinuka kiuchumi.
Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe mjini Morogoro juzi wakati akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu, watoto na wazee mkoani Morogoro.
"Ili mjikomboe kiuchumi mnatakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu nawabunifuna uiunga katika vikundi vya ujasiriamali muweze kupata mikopo nakufanyashughuli mbalimbali za biashara" alisema Mchembe.
Alisema dhana ya 50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake si kuosha vyombo bali ni mwanamke kuweza kufanya kazi za uzalishaji mali kama wanavyofanya wanaume na kumiliki ardhi.
Akizungumza wakati akitoa mada katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo aliwataka wanawake hao kutumia mitandao ya kijamii kwa maufaa badala ya kuitumia kwa masuala yasiyo na tija.
"Jamani wanawake wenzangu tutumie simu zetu kwa ajili ya maendeleo, kama kupeana taarifa, kutafuta masoko ya bidhaa zetu na si vinginevyo" alisema Mgongo.
Akitoa zawadi ya pekee katika kongamano hilo alisema kwa kutambua umuhimu wa mtoto wa kike Shule ya John The Baptist Girls High School imetangaza fursa ya kusomesha bure wanafunzi watatu wa kidato cha kwanza na watatu wengine hadi cha nne kwa mwaka 2019.
Alisema anachotakiwa kufanya mwanafunzi ni kufika shuleni hapo siku yoyote ndani ya mwezi wa oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mtihani wa kuchuana na kuwa fursa hiyo imetolewa na Mfuko wa Ndibalema John Mayanja Memorial Scholarship.
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu alisema kuwa kongamano hilo lenye lengo la kuwajengea uwezo ajira binafsi watoto wa kike ni la kwanza tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka jana.
Alisema kufanyika kwa kongamano hilo ni maandalizi ya kuelekea katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yatakayofanyika hivi karibuni.s
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeweka mazingira mazuri ya kuwasaidia wajasiriamali na kuwa imetenga fedha kwa ajili ya kuwakopesha hivyo akato mwito kwa wajasiriamali hao kuongeza thamani ya bidhaa zao kwa kuziweka katika vifungashio vilivyobora.
Katika hatua nyingine Mtaka aliipongeza kampuni ya Trumark kwa kazi kubwa inayoifanya ya kuwasaidia vijana kuzitambua fursa za maendeleo na akatoa mualiko kwa wajasiriamali hao kwenda Simiyu kwenye maonyesho ya viwanda vidogo vidogo (SIDO) yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23 hadi 28.
Kongamano hilo lilihitimishwa kwa makundi mbalimbali pamoja na watoa mada kupata zawadi na vyeti vya ushiriki.
No comments:
Post a Comment