Mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi ambaye atazindua albamu yake skiku ya tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka huu
Na mwandishi wetu, Dar
es Salaam. Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi, utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.
Mbali na Lowassa, waimbaji watakaosindikiza uzinduzi wa albamu hiyo inayoitwa ‘Hakimu wa Haki’ ni Bahati Bukuku, Dk Tumaini Msowoya, Tumaini Njole, Tumaini Mbembela, Madamu Ruth ,Iren Mwamfupe, Bony Mwaitege, Margie Muliri, Juvenalista Mabuma Edson Mwasabwite.
Akizungumza na Mwananchi, Mariam alisema amemualika Lowassa kwa sababu ndiyo aliyeanza kuibu kipaji chake, alipompa nafasi ya kuimba siku ya sherehe yake ya kuzaliwa.
“Lowassa ni baba yangu, aliibua kipaji change ndio maana nikatamani awe mgeni rasmi na amekubali, namshukuru sana Mungu kwa sababu hii,” alisema.
Alitaja nyimbo zilizo kwenye albamu yake kuwa ni Hakimu wa Haki, Pam Pam tukuza, Natafuta Mshauri, Chereko leo, Nasikia Kuitwa, Agano Langu, Ushindi Lazima na Mapambazuko.
“Nasikia kuitwa ndio wimbo ambao niliimba wakati nikianza mbele ya baba Lowassa, kwa hiyo ilipofika hatua ya kuandaa albamu yangu niliuweka na huo kwa sababu ndio ulionifungulia njia,” alisema.
Akizungumzia changamoto alizokutana nazo kwenye muziki huo, Mariam alisema ni gharama kubwa ya uandaaji wa muziki pamoja na kusambaza kazi hiyo.
“Naimba muziki kwa sababu nasikia kuitwa kwa ajili ya kazi hiyo, kusema kweli gharama za uandaaji wa kazi nzuri ni kubwa hata hivyo namshukuru Mungu kwa sababu nimeshakamilisha hatua ya kwanza,” alisisitiza.
Hata hivyo alisema, imekuwa rahisi kwake kufikia ndoto ya mafanikio kwa sababu ya sapoti kubwa kutoka kwa waimbaji waliotangulia.
Mariam amesema tayari tiem ya wacheza show ‘dancers’ imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya siku hiyo.
“Mara nyingi waimbaji wa muziki wa injili huwa tunapuuzia wacheza shoe lakini ni watu muhimu na hawa ndio huwa wanafanya watu wafurahie matamasha, kwa hiyo tayari nimeshawaingiza kambini,” alisema.
Akizungumzia uzinduzi huo, mwimbaji Jesca Gazuko anayetamba na wimbo wa ‘Bwana Amefanya’ alisema ujio wa Lowassa unaonyesha namba ambavyo viongozi wamekuwa wakisapoti kazi za waimbaji wanaochipukia.
No comments:
Post a Comment