Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB), Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Ndg Marco Mtunga na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Prof Damian Gabagambi wakionyesha hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles
Tizeba leo tarehe 11 Octoba 2018 ameshuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano
ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi.
Katika hafla hiyo iliyofanyika katika
Ukumbi mdogo wa Mikutano katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini
Morogoro Waziri Tizeba amesisitiza matrekta hayo kutumika ipasavyo kwenye sekta
ya kilimo ili kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo nchini jambo litakalokuwa
na manufaa kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Taasisi ambazo zimeshirikiana
kufanikisha utiaji saini huo ni Bodi ya Pamba ambayo ipo chini ya wizara ya
kilimo, Benki ya Maendeleo ya kilimo-TADB, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na
Tume ya Maendeleo ya ushirika.
Dkt Tizeba alisema kuwa Vyama vya ushirika
vya msingi vinapaswa kuongeza juhudi katika kilimo ili kuakisi kulipa gharama
za mkopo ambao ni asilimia 20 ya mkopo wote katika kipindi cha miaka mitatu huku
asilimia zingine 80 zikilipwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo-TADB.
Utiaji huo wa saini hati ya
makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta 300 kwa vyama vya msingi vya ushirika unajili
wakati ambapo hivi karibuni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe
Kassim Majaliwa alimkabidhi
Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 ya
Ursus kwa ajili ya
kukopeshwa kwenye vyama vya ushirika vya
msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.
Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini Dkt Tizeba
alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi
ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni
za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia
majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.
“Katika kilimo cha
Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha wakulima walichelewa kuanza
kuandaa mashamba kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana,” Alikaririwa
Dkt Tizeba na kuongeza kuwa
“Mara mvua
inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza
kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika
kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya
mara mbili”
Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za
mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa
kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia
ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa
pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.
Alisisitiza kuwa Bodi ya Pamba pamoja na Tume
ya Maendeleo ya ushirika zinapaswa kufuatilia kwa karibu hatua zote mwenendo wa
ufanyaji kazi wa matrekta hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa punde
yanapoanza kufanya kazi yawe yanafanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.
No comments:
Post a Comment