BREAKING

Thursday, 17 May 2018

YANGA YALE YALE,YATOA SARE IKIWA NYUMBANI DHIDI YA RAYON SPORTS YA RWAMNDA


Dakika 90 za mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda zimemalizika katika Uwanja wa taifa, Dar es Salaam kwa matokeo ya suluhu ya 0-0.

Mchezo huo ulionekana kwa kila timu kucheza kwa uangalifu zaidi huku wote wakikosa nafasi kadhaa za kufunga ikiwemo Yanga kupitia Chirwa aliyegongesha mwamba mnamo kipindi cha pili.

Mchezo ambao ni wa pili kwa timu zote mbili katika hatua ya makundi ya michuano hiyo unaiweka Yanga katika mazingira magumu ambapo mpaka sasa inakuwa imeambulia pointi moja pekee.

Ikumbukwe katika mechi iliyopita Yanga ilikubali kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0 dhidi ya dhidi ya USM Alger huko Algiers, Algeria.

Wakati huo Rayon Sports inakuwa imejikusanyia alama 2 kwenye kundi hilo 'D' baada ya sare ya 1-1 dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya kwenye mechi yake ya kwanza iliyopigwa Kigali, Rwanda.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube