BREAKING

Thursday, 3 May 2018

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA VIJANA U-20 AMMY NINJE AMTEMA KAMBWILI KISA KUONYESHA 'MAHABA NA YANGA'



Mlinda Mlango wa kikosi cha Ngorongoro Heroes na klabu ya Yanga, Ramadhan Kabwili ameondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo ya vijana chini ya miaka 20.

Kabwili amejiunga na Yanga kwa ajili ya mchezo wa kimataifa ambao wanaenda kukabiliana na USM Alger katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga imemuhitaji kipa huyo kulingana na Beno Kakolanya kuripotiwa kuumwa hivyo anaweza asijumuishwe kwenye kikosi cha Yanga kitakachocheza dhidi ya wapinzani wa Yanga huko Algeria.

Yanga inatarajiwa kuondoka leo nchini kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo huo wa mkondo wa kwanza utakaopigwa Mei 6 mjini Algiers.

Tayari Kabwili ameshaungana na Yanga na anatarajiwa kuwa sehemu ya msafara, huku Kocha wa Ngorongoro, Ammy Ninje, amesema atachukua mbadala wa Kabwili kutoka JKU ya Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube