BREAKING

Monday, 28 May 2018

NAIBU WAZIRI MAVUNDE AFUNGUA MKUTANO WA WADAU WA WCF KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI JIJINI MBEYA

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akipeana mikono na mama mjane, Atulehemu Kiduko, ambaye analipwa fidia ya kila mwezi kufuatia kifo cha mumewe wakati akiwa kazini kwenye kiwanda cha karatasi Mgololo kilichoko Mufindi  mjini Iringa. mama huyo alitoa ushuhuda wa huduma anayopata kutoka WCF wakati wa kutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijini Mbeya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, akifungua mkutano  baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini uliofanyika jijinmi Mneya Mei 26, 2018 kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.

SERIKALI ilianzisha Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata mafao bora na stahiki ya fidia tofauti na sheria ya zamani iliyotoa viwango vya chini vya fidia,  lakini pia kuwawezesha waajiri kupata muda zaidi kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendeshaji.



Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde, jijini Mbeya leo Mei 26, 2018 wakati akifungua mkutano baina ya Serikali na wadau wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, (TPSF) na Chama cha Wafanyabiashara ya Viwanda na Kilimo (TCCIA) Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kwa lengo la kujadiliana namna bora zaidi ya utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi.



Mhe. Mvunde alisema viwango vya juu vya malipo ya fidia kwa wafanyakazi walipokuwa wanaumia kazini kabla ya sheria ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, ilikuwa ni shilingi 108,000/=kwa mfanyakazi aliyepata ajali au kuumia kazini, lakini pia sheria inasema kulikuwa na malipo mengine ya shilingi 83,000/= kwa mfanyakzi aliyefariki kwa ajali au ugonjwa kutokana na kazi aliyokuwa akifanya na malipo hayo yalitegemea pia mkataba wa ajira yake unasemaje.

“Serikali ilikuja na sheria mpya baada ya kuona viwango hivi kwa ubinadamu na kwa hali halisi, vilikuwa vimepitwa sana na wakati na wafanyakazi walikuwa wanapata fidia hiyo kwa kadhia kubwa sana na viwango hivyo haviendani na ukuaji wa uchumi na kwa wakati tulionao.” Alifafanua Mhe. Naibu Waziri.

Aidha Mhe. Mavunde alisema, Mfuko unafaida kubwa sio tu kwa wafanyakazi bali pia kwa waajiri na taifa kwa ujumla ambapo  wafanyakazi sasa wanauhakika wa kupata kinga ya kipato kutoakana na majanga ambayo yatasababishwa na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi wanazofanya, lakini waajiri nao watapata muda zaidi wa kushughulikia masuala yao ya uzalishaji na uendelevu wa biashara na shughuli zao kwani Serikali kupitia Mfuko itabeba  mzigo wote wa gharama pindi mfanyakazi atakapofikwa na janga lolote awapo kazini.

“Pamoja na uchanga wake, Mfuko huu ambao umeanzishwa mwaka 2015 umeonyesha mafanikio makubwa katika kipindi kifupi kwani hadi sasa waajiri ambao wameshajisajili kwenye mfuko wetu ni 13,500 na wafanyakazi wao ambao wamepatwa na majanga wakiwa kazini wameshalipwa fidia na Mfuko fedha zisizopungua shilingi bilioni 2.52 kufikia Februari 2018.” Alibainisha.

Alisema Mfuko umekuja wakati muafaka kwani nchi inakwenda kwenye uchumi wa viwanda bila shaka kutakuwepo na ongezeko la ajali na magonjwa yanayotokana na uendeshaji wa shughuli katika viuwanda vyetu hivyo ni lazima kiwepo chombo kitakachosimamia majukumu haya ya fidia ili kuwapa nafasi pana waajiri kuendelea na shughuli zao za uzalishaji. 

“Rais wetu wa Jamhuri ya uungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kila wakati tunapokutana kwenye baraza la Wafanyabiashara Tanzania amekuwa akituagiza sisi wasaidizi wake, kama kuna jambo lolote linajitokeza na sekta binafsi inafikiri kwamba jambo hili bado halijaeleweka na haliko sawasawa ni wajibu wetu sisi mawaziri kuchukua hatua haraka za kukutana na kujadiliana na wadau na kushauriana na wadau husika ili kufikia muafaka na kuelewana ili kwenda pamoja na ndio maana leo tuko hapa.” Alifafanua Mhe. Naibu Waziri Mavunde

Wakitoa ushuhuda mbele ya washiriki wa mkutano huo, Wafanyakazi waliopatwa na majanga ya kuumia au kufiwa na wenza wao, wameipongeza Serikali kwa kuanzisha Mfuko huo kwani umekuwa ni mkombozi kwa wafanyakazi.

“Mimi nilikatika vidole vya mkono wangu wa kushoto wakati nikitekeleza majukumu yangu ya kazi kwenye kiwanda cha Lake Cement kinachozalisha saruji ya nyati (Nyati cement) huko Kimbiji jijini Dar es Salaam na WCF imenilipa fidia ya mkupuo ya kiasi cha shilinhgi milioni 11, alisema Bw. Jimmy Samson Malumbo mbele ya Mkutano huo.



Mwingine aliyetoa ushuhuda wa faida ya Mfuko kwa wafanyakazi, ni mama mjane, Bi. Atulehemu Kiduko wa huko Mafinga Mkoani Iringa, alisema mumewe ambaye alikuwa mfanyakazi wa kiwanda cha karatasi Mgololo Mufindi Papers baada ya kuangukiwa na gogo wakati akitekeleza majukumu yake. Hivi sasa mama huyo mjane anapokea malipo ya fidia kila mwezi shilingi 110,000/= na watoto wake wawili kila mmoja analipwa shilingi 55,000/= kila mwezi.

“Kwakweli nimefarijika sana kwa malipo haya, ingawa nimeshampoteza mwenzangu, lakini fidia hii ninayolipwa imekuwa ikinisaidia sana katika kuhudumia familia yangu kijijini ikiwa ni pamoja na kumsomesha motto wangu  mmoja aliye darasa la tatu.” Alisema Bi. Atulehemu.

  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba alisema Mfuko unaendeshwa kwa msingi wa utatu ambapo katika bodi ya wadhamini ambayo ina uwakishi wa serikali, wafanyakazi na uwakilishi wa waajiri kama ambavyo Shirika la Kazi Duniani linavyotaka katika masuala haya ya fidia kwa wafanyakazi.

Alisema, katika mfumo wa zamani, mfanyakazi anapotoka au kwenda kazini endapo atapatwa na tatizo njiani sheria ya zamani haikumtambua, tofauti na sheria ya sasa ambapo inaeleza mfanyaakzi akiumia au akifikwa na umauti wakati akitoka kazini au akielekea kazini sheria ya sasa inataka afidiwe.

“Alisema Mfuko umeweka utaratibu ili kuhakikisha mfumo wa usajili wa waajiri unakuwa wa haraka na rahisi lakini pia kushughulikia masuala ya ulipaji fidia katika kipindi kifupi.” Alisema.

Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala, Wizara ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Bw.Peter Kalonga, kwa niaba ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Bw. Eric Shitindi, akitoa hotuba
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba akizungumza. 

 Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
  Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
  Sehemu ya waliohudhuria mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Uendeshaji, wa WCF, Bw. Anselkim Peter, akiwasilisha mada kuhusu shughuli za Mfuko.
 Mkurugenzi wa huduma za Tiba na Tathmini wa WCF, Dkt. Abdulsalaam Omar, akitoa mada kuhusu namna tathmini inavyofanyika kwa Mfanyakazi aliyepatwa na madhara wakati akitelekeaza wajibu wake wa kazi.
 Mwakilishi kutoka chama cha waajiri Tanzania, (ATE), Bi. Patricia Chao, akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Mbeya, Dkt. Lwitiko Mwakalukwa, akizungumza kwenye mkutano huo.
 Washiriki wakipiatia taarifa mbalimbali za WCF.



 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, (kushoto), Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mfuko huo, Bw. Anselim Peter, (wapili kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (aliyeipa mgongo camera), wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge
 Emiliana Gwagilo, Afisa Matekelezo wa WCF, akiandaa taarifa kwenye meza kuu

 Afisa Matekelezo wa WCF, Bw. George Faustin, akijibu baadhi ya hoja zilizojitokeza kutoka kwa washiriki wa mkutano.
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF , akibadilkishana mawazo na Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bw. Anselim Peter, (kulia), Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, Dkt. Abdulsalaam Omar, (kushoto) na Afisa Matekelezo, Bi. Emiliana Gwagilo.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF, Bw. Anselim Peter, (kushoto), na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, wakiwajibika kwenye mkutano huo.
Naibu waziri Mavunde, akisindikizwa na Bw. Mshomba wakati akiondoka kwenye eneo la mkutano.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube