BREAKING

Thursday 10 May 2018

WABUNGE WA SIMBA DODOMA KUTIA UBANI KWA KIKOSI CHA SIMBA KABLA YA KUWAVAA SINGIDA UNITED WIKENDI HII,NAMFUA



Kikosi cha Simba kimeanza safari ya kuelekea Singida kwa ajili ya mtanange wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Singida United.

Simba itapitia katika Makao Makuu ya nchi, Dodoma, kuweka kambi fupi kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea mjini Singida.

Taarifa kwa mujibu wa Meneja wa kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi, Richard Robert, amesema kuwa kikosi kitapita jijini hapo ili kuweka kambi fupi kabla ya kuendelea na safari.

Inaelezwa kuwa Simba wamepanga kupitia Bungeni kwa ajili ya kupata baraka za kuelekea mechi yao na Singida itakayopigwa Mei 12 kwenye Uwanja wa Namfua.

Tayari kikosi hicho kipo njiani hivi sasa kuelekea jijini humo na kesho kitaanza tena safari ya Singida.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube