BREAKING

Wednesday, 23 May 2018

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa(kushoto), akifurahia jambo na Wazitri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, (watatu kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua, (wane kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TANESCO), Dkt. Alexander Kyaruzi, na Mkuriugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, wakati alipowasili kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi asilia (Mtwara Gas Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018. Kituo hizo sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.


 Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, akitoka eneo la mitambo mipya miwili ya kuzalisha umeme wa Megawati 4 kila mmoja baada ya kuizindua, kwenye Kituo cha Kufua umeme wa Gesi Mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
Wabunge wa Mikoa ya Kusini, wakiwa na mwenyekiti wao, Mhe. Selemani Bungara(wapili kushoto)
 
NA MWANDISHI WETU, MTWARA-MEI 22, 2018

WABUNGE wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara, wameimwagia sifa Serikali hususan Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme TANESCO kufuatia kumaliza adha ya umeme iliyodumu kwa takriban miaka 10 kwenye mikoa hiyo.

Pongezi hizo wamezitoa mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, baada ya kuzindua Kituo cha Kuzalisha umeme wa gesi asilia (Mtwara Gas Plant), mkoani Mtwara Alasiri ya Mei 21, 2018.

Wa kwanza kutoa pongezi hizo alikuwa Mbunge wa Mtwara Mjini kupitia chama cha Wananchi CUF, Mhe Maftah Nachuma ambaye yeye alienda mbali zaidi na kufikia kusema atamuandalia Mhe. Waziri Mkuu mkutano mkubwa wa hadhara ili kuwaeleza wananchi wa jimbo lake, mafanikio yaliyoletwa na serikali.

“Mheshimiwa Waziri Mkuu, leo ninayofuraha kubwa sana, kwani kilio cha muda mrefu cha wana Mtwara, cha kukosa umeme wa uhakika, hatimaye kimepatiwa ufumbuzi na kwetu sisi hii ni sherehe kubwa, ningetamani mkutano huu ungewaalika na viongozi wengine wa vyama vya siasa, na mimi binafsi nitakuandalia mkutano mkubwa wa hadhara ili uje uwaeleze wananchi maendeleo haya yaliyoletwa na serikali.” Alisema Mhe. Nachuma.

Naye Mwenyekiti wa wabunge kutoka Mkoa wa Lindi, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara, alisema maendeleo haya ambayo serikali inawafikishia wananchi ni kwa sababu bunge linaisimamia vema serikali.

“Siku zote tunasema Kusini kwanza mambo mengine baadaye, na mimi niwaambie, tutaendelea kupiga kelele hadi kero zote zitatuliwe, na niishukuru serikali kwa kumaliza hii kero ya umeme iliyudumu kwa muda mrefu.” Alisema Mhe. Bungara

Naye Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia, yeye pia aliipongeza serikali kwa kumaliza kero ya umeme Mkoani Mtwara, kwani sasa Mkoa wa Mtwara umekamilika kwa kila eneo katika Nyanja ya uwekezaji.

“Mikoa yetu ya Kusini tuna kila kitu, Gesi iko hapa, Bandari tunayo, Ardhi ambayo wala haihitaji fidia nayo ipo, na sasa tunao umeme wa uhakika unaopatikana masaa 24, hii ni fursa nzuri kwetu sisi tunaotoka mikoa ya Kusini.” Alisema Mhe. Hawa Ghasia.

Akitoa taarifa fupi ya kituo hicho mbele ya Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka alisema. Kituo cha kufua umeme kwa Gesi Asilia cha Mtwara kilianza rasmi kufanya kazi mwaka 2007, kwa sasa kituo hiki kinazaidi ya miaka kumi(10) na kina uwezo wa kuzalisha Megawati 18 za umeme na ndio chanzo pekee cha Nishati ya umeme kwa eneo lote la Mikoa ya Lindi na Mtwara, isipokuwa kwa baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Kilwa na Liwale ambayo yanapata umeme kutoka kwenye vituo vyao vidogo.

Mahitaji ya juu ya Nishati ya Umeme kwa eneo lote la Mikoa ya Lindi na Mtwara ni takribani Megawati 16.5” Alisema Dkt. Mwinuka.

Alisema, Katika kukabiliana na changamoto ya kukua kwa mahitaji ya umeme katika mikoa ya Lindi na Mtwara, serikali kupitia TANESCO ilifanya maamuzi ya upanuzi wa kituo hiki cha kuzalisha umeme ili kukiongezea uwezo wake. Hatua hii inahusisha usimikaji wa Mitambo miwili ya kufua umeme kila mmoja ukiwa na uwezo wa kuzalisha Megawati 2, na hivyo kufanya ongezeko la jumla la Megawati nne (4)

Hatua hii itaongeza uwezo wa kituo kuwa ni Megawati ishirini na mbili (22) ambao utatosheleza mahitaji ya sasa ya eneo hili na kuwa na ziada.

Akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza kwenye hafla hiyo, Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani alisema, Hatua hii ni ya awali katika mpango endelevu unaolenga katika kuimarisha upatikanaji wa nishati ya umeme  katika mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo kiasi cha Megawati nyingine nne (4) zitafuatia katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019, pia upo mpango mkubwa wa ujenzi wa mtambo wa Megawati 300 kwa msaada wa Shirika la Maendeleo la Watu wa Japani JICA, unaotarajiwa kukamilia ifikapo mwaka 2020.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, aliwapa changamoto wakazi wa Mkoa wa Mtwara kutumia umeme huo kikamilifu katika kujiletea maendeleo kwani sasa umeme ni bora na wa uhakika.

“Nitoe wito kwa vijana, sasa mnaweza kufanya shughuli za kunyoa(saloon), kuchomelea vyuma, kuranda mbao, kuuza juice, na hata wengine kuchaji simu na kuweka miziki kwenye simu kwa kutumia computer, mnayo fursa kubwa ya kufanya shughuli zenu ndogo ndogo za kiuchumi kupitia umeme huu ambao sasa unawaka masaa 24.” Alisema.

Waziri Mkuu aliipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara, kwa kuchangamkia haraka uwepo wa umeme wa kutosha kwa kuanza kuweka taa za barabarani na hivyo kuufanya mji wa Mtwara kung’aa majira ya usiku.

 Mbunge wa jimbo la Kilwa Kusini, Mhe. Selemani Bungara, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
 Mbunge wa Mtwara Mjini Mhe.Maftah Nachuma, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa upanuzi wa Kituo cha Kufua umeme wa Gesi mkoani Mtwara Mei 21, 2018.
 Mbunge wa Mtwara Vijijini, Mhe. Hawa Ghasia
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa hotuba yake.
 Waziri Mkuu akipitia hotuba yake kabla ya kuhutubia.
 Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme wa Gesi Mkoani Mtwara, Mhandisi Mpulungwa Chilumba, (kushoto), akitoa maelezo ya kiutendaji ya Kituo hicho mbele ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, (katikati), Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, (kulia) na viongozi wengine wa Mkoa wa Mtwara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi cha Mtwara (Mtwara Gas Plant) Alasiri ya Mei 221, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. . Kituo hizo sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa, akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa upanuzi wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi cha Mtwara (Mtwara Gas Plant) Alasiri ya Mei 221, 2018. Kushoto ni Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani. . Kituo hizo sasa kitazalisha Megawati 22 kutoka za sasa Megawati 18.

 Waziri Mkuu, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi na viongozi wa juu wa Wizara ya Nishati na Shirika hilo, wakati alipowasili kwenye Kituo cha Kufua umeme wa Gesi cha Mtwara Mei 21, 2018.
 Wananchi wakishangilia
 Mama akiwa ma mwanaye huku akifurahi 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka, (wapili kushoto), akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Dkt. Alexander Kyaruzi, (kushoto), Naibu Mkurugenzi wa Shirika hilo anayeshughulikia uzalishaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa, (kulia) na Meneja wa Kituo cha Kuzalisha Umeme wa Gesi Mtwara, Mhandisi Mpulungwa Chilumba.
 Dkt. Kalemani akimnong'oneza kitu Meneja wa Kanda ya Kusini wa TANESCO, Mhandisi Aziz Salum.
 Wafanyakazi wa TANESCO Mtwara
 Waziri Mkuu Majaliwa na viongozi wengine wakifurahia burudani ya kwaya
 Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, wakiwa wenye furaha wakati vikundi vya burudani vikitoa burudani
 Picha ya pamoja

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube