BREAKING

Monday, 12 March 2018

MAJANGA! KANE AUMIA WAKATI TOTTENHAM IKITOA DOZI NENE YA 4-1 DHIDI YA BOURNEMOUTH


Inawezekana ikawa pengo kubwa kwa Tottenham Hotspurs baada ya Mshambuliaji wake hatari, Harry Kane, kuumia leo katika mchezo wa ligi dhidi ya Bournemouth.

Tottenham imeibuka na ushindi wa mabao 4-1, matokeo ambayo yameifanya timu hiyo ipande mpaka nafasi ya 3 kwenye msimamo wa ligi.

Kane alitolewa dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza baada ya kugongana na kipa wa Bournemouth, Asmir Begovic, na kupelekea kuumia enka ya mguu wa kulia.

Kufuatia tukio hilo, Kane alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Erik Lamela.

Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino, amesemakuwa anadhani hajaumia japo itabidi wasubiri majibu kutoka kwa daktari.

Kane ameumia huku klabu yake ikiwa katika maandalizi ya kucheza na Swansea City kwenye Kombe la FA, vilevile timu yake ya taifa, England itakipiga dhidi ya Netherlands Ijumaa ya wiki litakalofuata, Machi 23 2018. 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube