Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa Jully Sawani na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) manispaa ya Iringa wakifurahia kukabidhiwa kwa hati kwa diwani wa chama hicho tukio hilo lilifanika katika ofisi ya kata ya kihesa likihudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na mamia ya wananchi na wanachama wa chama hicho.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa Jully Sawani wakizungumza na wananchi waliohudhulia tukio hilo
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas,diwani halali wa kata ya kihesa Jully Sawani wakiwapokea wanachama wapya kutoka chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wa kata ya kihesa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas akiongea na wananchi walijitokeza kushudia tukia na kupewa cheti diwani wa kata hiyo Jully Sawani
KATA ya kihesa manispaa ya
Iringa imeanza kupata neema ya mamilioni ya fedha za kimaendeleo mara baada ya
kumpata diwani mpya kupitia chama cha mapinduzi (CCM) baada ya kupita bila
kupigwa kutoka na vyama vingine vya siasa kutoweka wagombea.
Akikabidhiwa hati ya utambulisho
wa kuwa ndio diwani halali wa kata ya kihesa,Jully Sawani alielezea mikakati ya
kimaendeleo ya kata hiyo ambayo ataanza nayo ni kukarabati miundombinu ya
barabara kwenye baadhi ya mitaa ya kata hiyo.
“Ukipita kwenye mitaa yetu
utagundua kuwa mtaa kama mtaa wa mafifi miundombinu ya barabara sio nzuri
kabisho akahidi kuwa ndani ya wiki hii atapeleka kata pila lianze kazi ya
kuzikarabati bara bara hizo ili kurahisisha usafiri kwa wananchi wake kwa kuwa
wamemtuma kufanya kazi” alisema Sawani
Sawani aliongeza kwa kusema
kuwa amejianda kuhakikisha anatatua kero za wananchi kwa kushirikiana na serikali
ya manispaa ya Iringa ambayo inatekeleza sera za chama cha mapinduzi (CCM) ya
mwaka 2015 huku ikiwa na kauli mbiu inayosema kuwa hapa kazi tu.
“Naomba niseme ukweli wananchi
wangu wote wa kata ya Kihesa sasa ni wakati wa kufanya kazi na sio mchezo
mchezo mliokuwa mnaufanya nimeomba kuwa diwani kwa lengo la kuhakikisha kila
mwananchi wa kata hii anafanya kazi kwa kuhakikisha kuwa familia yake haiwi
masikini,ninasema kuwa kila ukilala hakikisha unaukataa umasikini kwa kuutamka
wakati unalala tena kwa zaidi ya mara tisa hapo ndio utafanya kazi” alisema Sawani
Aidha Sawani alitoa kilio chake
cha kwa kuomba msaada wa kimaendeleo kwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya
Chama cha Mapinduzi (CCM) MNEC Salim Asas ambapo
alimwambia kuwa wananshida ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya
sekondari ya Kihesa na kusaidiwa kumalizia ujenzi wa jingo la kibiashara ambalo
lipo jirani na ofisi za kata ya hiyo.
“Mheshimiwa MNEC Salim Asas
nipo hapa naomba utusidie msaada wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule
ya sekondari ya Kihesa na jingo hili ambalo lipo mbele yetu unaliona linahitaji
kumaliziwa ili kuweza kuongeza ajira kwa wananchi wa kata yangu hivyo naomba
sana msaada wako kukamilisha hivi vyote kwa awamu hii ya kwanza” alisema Sawani
Akihutubia mamia ya wananchi
walijitokeza katika hafla hiyo ya kukadhiwa cheti cha kuwa diwani wa kata hiyo Jully
Sawani, MNEC Salim Asas alisema kuwa atatoa mifuko miambili ya saruji kwa ajili
ya kutatua kero hiyo ya ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Kihesa na
kuahidi kuwa ataitembelea shule hiyo kujua changamoto nyingine.
“Leo naanza kwa kutoa mifuko miambili
ya saruji lakini nitakuja hapo shule kujionea changamoto nyingine za shule hiyo
ili niweze kuzitatua kabisa na kuwaacha wananfunzi wakisoma kwa uhuru kwa lengo
la kukuza kizazi chenye elimu bora na kuja kusaidia taifa katika kuleta
maendeleo wote tunajua kuwa bila elimu huwezi kupata maendeleo hivyo nitasaidia
sana kwenye elimu” alisema Asas
Asas aliwakata viongozi wa kata
hiyo kuandaa bajeti ya kumalizia jingo hilo ambalo litaongeza ajira kwa
wananchi wa kata hiyo ambao kwa sasa hali zao za kiuchumi zimedolola hivyoa
atafanya linalowezekana kuhakikisha kuwa wananchi wa kata hiyo wanabadili na
kuacha kuishi kimazoea.
“kata ya Kihesa anayoijua yeye ni ile yenye
vijana wengi wasio na ajira ambao kwa bahati mbaya wamekuwa wakishughulishwa
kwenye siasa badala ya kuhamasishwa kufanya shughuli za maendeleo” Alisema Asas
Asas alisema vijembe na
malumbano ya kisiasa katika kata hiyo yanatosha na akawataka vijana hao kuunda
vikundi vya ujasiriamali vitakavyowawezesha kufikiwa kirahisi na mipango
mbalimbali ya maendeleo
No comments:
Post a Comment