BREAKING

Monday, 8 January 2018

STANBIC BANK YAJA NA AKAUNTI YA HATUA


Baadhi ya watoto na wazazi wakifurahi wakati wa hafla ya uzinduzi wa akaunti mpya ya HATUA ya benki ya Stanbic jijini Dar es salaam. Akaunti hiyo mpya ni kwa ajili ya watoto na ina lengo la kuwasaidia wazazi na walezi katika mahitaji ya watoto kama vile ada za shule na pia kuwajengea watoto utamaduni mzuri wa kujiwekea akiba.









Stanbic Bank Tanzania imezindua akaunti mpya ijulikanayo kama HATUA, ambayo ni kwa ajili ya watoto yenye lengo la kuwasaidia wazazi kuwawekea akiba watoto wao huku wakiwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba.
Kwa kuanzishwa kwa aina hii mpya ya akaunti, Stanbic bank inaendelea kuwapatia wateja wake huduma mpya na bora za kibenki kila siku kuendana na mahitaji ya wateja an hali halisi ya soko.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa akaunti hiyo uliofanyika katika makao makuu ya benki hiyo Kinondoni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, mkuu wa mauzo wa benki hiyo Shangwe Kisanji amesema kuwa benki hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kuwapatia wateja wake huduma mpya kila mara na nyakati zote huduma hizo huendana na mahitaji ya wateja na mahitaji ya jumla ya soko la huduma za kibenki hapa nchini.
“Wakati wote tumekuwa tukiangalia njia mbalimbali za kuwahudumia vyema wateja wetu katika kutunza fedha zao ikiwemo kuwawekea watoto akiba kwa manufaa yao ya baadae na pia kuwajengea utamaduni wa kujiwekea akiba wawapo wakubwa, utamaduni ambao ni muhimu sana kwa uchumi na maisha yao”
Ameeleza kuwa akaunti hiyo ya HATUA ni muendelezo mzuri wa kuwatoa watoto kwenye utamaduni wa kujiwekea akiba kwenye vibubu na badala yake kuanza utamaduni wa kujiwekea akiba kwa njia rasmi zaidi.

Amesema akaunti hiyo haina makato ya huduma na kiwango cha chini cha amana ni shilingi 20,000 tu. Amebainisha kuwa akaunti hiyo haina masharti magumu ya kuiendesha  na inaruhusu kutolewa kwa fedha mara moja kwa robo ya mwaka ili kusaidia katika majukumu yanayowahusu watoto kama vile ada za shule, sare na kadhalika. Amesema pia akaunti hiyo hujipatia riba kulingana na amana iliyopo.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube