BREAKING

Wednesday, 3 January 2018

MKUTANO WA FIFA KUFANYIKA TANZANIA, RAIS WA CAF DAR ...




Tanzania inataraji kuwa wenyeji wa mkutano mkubwa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA (Fifa Summit) utakaofanyika February 22, 2018 kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere.

Mkutano huo mkubwa wa pili unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania unashirikisha nchi 19 Wanachama wa Fifa.

Mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa FIFA Gian Infantino pia utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF) Ahmad Ahmad, Makamu wa Rais wa Fifa,Katibu mkuu wa Fifa na viongozi mbalimbali wa FIFA na CAF ikiwemo wajumbe wa kamati ya utendaji.

Wageni kutoka nchi mbalimbali duniani watakaohudhuria mkutano huo wataanza kuwasili Tanzania Februari 20, 2018

Ajenda za mkutano huo mkubwa wa Fifa ni miradi mbalimbali ya Fifa zamani ikifahamika kama Goal Project na sasa ikifahamika Fifa Forward Programme,ajenda ya soka la vijana,Wanawake na klabu wakati ajenda nyingine ya mkutano huo ni kujadili kalenda ya kimataifa ya Fifa,kuboresha masuala ya uhamisho na vipaumbele vyake

Nchi zitakazoshiriki ni Bahrain,Palestina,Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu(UAE),Algeria,Burundi,Africa ya Kati,Ivory Coast,Mali,Morocco,Niger,Tunisia,Bermuda,Monserrat,St,Lucia,Us Virgin,Maldives,Congo na wenyeji Tanzania.

Akizungumzia Mkutano huo unaofanyika kwa mara ya kwanza Tanzania Rais wa TFF Ndugu Wallace Karia alisema TFF inajivunia kupata uwenyeji huo mkubwa wa mkutano wa FIFA na hiyo inachangiwa na mahusiano mazuri na wadau mbalimbali ambayo yamezaa matunda.


Rais Karia ameongeza kuwa hiyo ni fursa kubwa kwa Serikali kupitia Wizara zake kuweza kutumia fursa hiyo ambayo inaweza kusaidia katika upande wa Uchumi.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube