BREAKING

Monday 8 January 2018

ATHUMAN CHAMA 'JOGOO' AFARIKI DUNIA


Beki wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Juma ëChamaí aliyeweika klabu za Pamba FC ya Mwanza na Yanga ya Dar es Salaam amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kwa matibabu ya ugonjwa wa Kiharusi.
  
Chama ni jina la utani ambalo marehemu Athumani Juma alipewa kutokana na beki wa zamani wa kimataifa wa Zambia, Dick Chama ambaye naye ni marehemu aliyecheza kwa mafanikio timu ya taifa ya kwao kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia 1967 hadi 1976 na klabu za za Mufulira Wanderers, Green Buffaloes na Bancroft Blades.

Athumani alipewa jina hilo baada ya kujiunga na Yanga mwaka 1981 akitokea Pamba ya Mwanza na mashabiki wa timu hiyo ya Jangwani walimbatiza Juma jina hilo baada ya beki wao mwingine, Rashid Idd aliyekuwa akiitwa Chama pia kuhamia Pan Africans baada ya kudumu tangu Jangwani tangu 1979.

Na umaarufu wake zaidi Jangwani ukaja kutokana  na alivyoweza kumdhibiti mshambuliaji hatari wa mahasimu enzi hizo, Simba, Zamoyoni Mogela ëGolden BoyíKisoka, Chama aliibukia Pamba FC ya Mwanza alikozaliwa na kukulia kabla ya kujiunga na Yanga na aliocheza nao wakati huo ni akina Joseph Fungo, Yussuf Ismail Bana, Ahmed Amasha ëMathematicianí, Isihaka Hassan Chukwu, Juma Mukambi ëJeneralií, Hussein Iddi, Charles Boniface Mkwasa, Abeid Mziba ëJJ Masigaí, Elisha John, Ali Mchumila, Makumbi Juma ëHoma ya jijií, Omar Hussein ëKeeganí, Juma Kampala na wengineo.

Chama pia alikuwa akijulikana kwa jina lingine la utani, Jogoo ambalo alipewa mwaka 1981 kwenye michuano ya CECAFA Challenge nchini Kenya kutokana na mchezaji mmoja wa Harambee Stars, Sammy Onyango ëJogooí.

Chama alistaafu soka mwaka 1990 na kujikita kwenye biashara zake ndogo ndogo kabla ya kuanza kusumbuliwa na maradhi mwaka 2014 na kujikuta anashindwa kufanya shughuli yake hadi umauti wake.

Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Chama. Amin. 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube