BREAKING

Thursday, 31 August 2017

MANGULA AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA CPC

 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philipo Mangua akimkaribisha Naibu Waziri za Mambo ya Nje 
wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya 
CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017. Katikati ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole. 
 Makamau Mwenyekiti wa CCM-Bara Philipo Mangua (kulia) akiongoza mazungumzo  baina yake na 
Naibu Waziri za Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC) Xu Luping (kulia) katika 
Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, Dar es Salaam, leo Agosti 31, 2017.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Ujenzi ya IDCPC Kanda ya Afrika,  Wang Heming 
akipigapicha mandhari ya eneo kitakakojenjwa Chuo Kikuu cha Viongozi wa Siasa cha Mwalimu 
Nyerere, Kibaha mkoa wa Pwani, alipotembelea eneo hilo, jana, Agosti 30, 2017. Kushoto ni Katibu wa 
NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngemela Lubinza.

Tuesday, 29 August 2017

MULTICHOICE YATANGAZA NEEMA KWA WATEJA WA DSTV! YAFYEKA BEI ZA VIFURUSHI VYOTE

 
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande akitangaza punguzo kubwa la bei kwa vifurushi vyote vya DStv bei zitakazoanza kutumika rasi Septemba mosi 2017.



PANGA LA BEI LAFYEKA;  DStv Premium kwa 8.15%, DStv Compact Plus kwa 11.02%, DStv Compact kwa 16.11%, DStv Family kwa 9.09% and DStv Access (Bomba) kwa 4.88%
 Katika kuhakikisha kuwa wateja wake wote na watanzania kwa ujumla wanaendelea kufurahia huduma za DStv, kampuni ya Multichoice Tanzania imetangaza neema kubwa kwa wateja wake kwa kufyeka bei za vifurushi vyake vyote, huku pia ikiboresha maudhui na vipindi katika vifurushi vyake hususan vile vya bei ya chini!
Habari hiyo njema imetangazwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam ambapo amesema bei hizo mpya zitaanza kutumika rasmi Septemba mosi 2017.

“Kumjali na kumsikiliza mteja ni nguzo ya uendeshaji wa biashara yetu. Tumesikia maoni ya wateja wetu na wananchi kwa ujumla kutusihi tuangalie uwezekano wa kupunguza bei, tumechanganua kwa kina na tumeamua kutekeleza matakwa yao, leo hii tumepitisha panga kwenye bei za vifurushi vyetu vyote!” alisema Maharage.

Akifafanua kuhusu punguzo hilo, Maharage amesema  kumekuwa na punguzo la hadi asilimia 16, ambalo ni punguzo kubwa sana na litakalowapa ahueni kubwa watumiaji wa DStv. Amezitaja bei mpya kuwa ni;







Monday, 28 August 2017

HIZI NDIO MECHI KUBWA ZA WATANI WA JADI BARANI AFRIKA



Miongoni mwa matukio yanayosisimua zaidi kwenye mchezo wa soka ni mipambano ya watani wa jadi. Katika nchi nyingi barani Afrika ukiwauliza kwa harakaharaka mashabiki wengi wa soka ni mechi zipi huwa wanazisubiria sana utawasikia wanakutajia michezo kama vile Real Madrid na Barcelona, Manchester United na Manchester City, Inter Milan na AC Milan, Liverpool na Manchester United, Chelsea na Arsenal au Bayern Munich na Borussia Dortmund.
Kutokana na umaarufu wa soka la nchi za Ulaya imekuwa ni rahisi kwa mechi zao kufuatiliwa kwa urahisi ukilinganisha na huku Afrika. Lakini hiyo haimaanishi kwamba bara la Afrika nalo halina michezo ya namna hiyo ambayo ikiwa inakaribia homa miongoni mwa mashabiki huwa juu kuliko kawaida.

Ukweli ni kwamba mechi za namna ya mifano iliyotajwa hapo juu zipo na zimekuwa zikichezwa kwa miaka mingi tu.kw au pengine inawezekana ukawa unazisikia tu lakini haujui umuhimu uliopo pindi zinapokutana. Jumia Travel imekukusanyia orodha ya mechi kali za mpira wa miguu ambazo timu zikikutana kunakuwa ni patashika, presha na vimbwanga vya kila aina.  
Orlando Pirates dhidi ya Kaizer Chiefs (Afrika ya Kusini) -  Soweto derby. Kama yalivyo mapambano mengine ya watani wa jadi, mchezo huu ni zaidi ya mpira wa miguu kwani ni uhasama hasa. Mchezo ambao umpewa jina la ‘Soweto derby’ huzikutanisha timu za Orlando Pirates na Kaizer Chiefs mara kadhaa ndani ya mwaka katika jiji la Johannesburg. Uhasama wa timu hizi mbili unakuja kutokana na kuwa zote zinatokea sehemu moja. Kaizer Chiefs ilianzishwa na aliyekuwa mmojawapo wa wachezaji wa Orlando Pirates, Kaizer Motaung.
   
Wydad Casablanca dhidi ya Raja Casablanca (Morocco) - Casablanca derby. Hakuna ubishi kwamba nchi za Afrika ya Kaskazini zimebarikiwa kuwa na vipaji lukuki vya mpira wa miguu ambapo mpaka hivi sasa vinaliwakilisha vema bara hili sehemu mbalimbali duniani. Katika mji wa Casablanca kwenye nyakati tofauti za mwaka kunakuwa na mchezo mkali ambao huzikutanisha timu za Wydad Casablanca na Raja Casablanca ambao pia hujulikana kama ‘Casablanca derby’. Mchezo wa watani wa jadi hawa mara nyingi hupigwa katika uwanja wa Mohammed V Stadium ambapo licha ya kuonyesha nani ni fundi wa kusakata kandanda lakini pia ni juu ya nani ni bora katika anga za kuliwakilisha jiji na nchi kwa ujumla.  
Al Ahly dhidi ya Zamalek (Misri) - Cairo derby. Linapokuja suala la mchezo wa soka basi mashabiki wa timu za Al Ahly dhidi ya Zamalek ni nambari moja kwa kuzishangilia timu zao. Mojawapo ya mitanange mikali kabisa ya soka ambayo hutawaliwa na presha na msisimko mkubwa ni pindi timu hizi zinapokutana ambao pia umepewa jina la ‘Cairo derby.’ Inapofikia siku ya mechi hii hali ya hewa ya jiji zima la Cairo hubadilika kutokana na homa ya mchezo huo. Mbali na kuwa ushindani huwa ni wa kisoka lakini kwa upande mwingine ni wa kisiasa zaidi.
    
Club Africain dhidi ya Espérance Sportive de Tunis (Tunisia) - Tunis derby. Katika jiji la Tunis kwenye ratiba tofauti za mchezo wa soka huzikutanisha timu mbili zinazowakilisha jiji hilo za Club Africain na Espérance Sportive de Tunis. Ushindani mkubwa katika mchezo huu umekuwa na historia tofauti ambapo hapo awali ulihusishwa na matabaka kama vile ilisemekana timu ya Espérance ilikuwa ikimilikiwa na serikali na tabaka la juu la watu wa mji wa Tunisia huku Club Africain ikimilikiwa na watu maarufu wa matabaka tofauti. Lakini hiyo imebadilika na ikawezekana kutokuwa na ukweli ndani yake kwani unaweza kukuta watu wa familia moja wanashabikia hizo kwa wakati mmoja.
  
Simba S.C. dhidi ya Young Africans S.C. (Tanzania) - Dar es Salaam au Kariakoo derby. Tukiachana na umaarufu wa mchezo wa mpira wa miguu katika nchi za Afrika ya Kuskazini pia katika kalenda za soka barani Afrika huwa inapigwa mechi kali sana kwenye ukanda wa Afrika ya Mashariki baina ya timu za Simba na Young Africans au Yanga ambazo zote hutokea jiji la Dar es Salaam. Mbali na timu hizo kukutana katika michezo kadhaa ya ligi kuu pia kuna michezo mingine ni pamoja na ngao ya jamii, kombe la shirikisho la mpira wa miguu, kombe la mapinduzi ne mingineyo. 
Kama ni mgeni kwenye jiji la Dar es Salaam basi ikifika siku ya mchezo huo utajua homa ya watani wa jadi wa timu hizo mtaani kwani utawatambua mashabiki wa timu hizo kwa mbwembwe, tambo na shamrashamra kwa kuvalia jezi za rangi nyekundu na nyeupe (Simba) huku Yanga ni (kijani na njano). 

Uhasama wa timu hizo ambazo zinatokea katika eneo moja la Kariakoo si tu kuhusu mpira bali ni heshima juu ya nani ni mfalme na bingwa wa kusakata kandanda nchini Tanzania na kuliwakilisha taifa kwenye anga za kimataifa. Mchezo baina ya timu hizi mbili huwa unapigwa kwenye uwanja wa taifa ambao unao uwezo wa kukusanya mashabiki takribani 60,000.
USM Alger dhidi ya MC Alger (Aljeria). Mchezo huu wa watani wa jadi kama ilivyo mingine huzitenganisha familia na majirani na wakati mwingine huisha kwa ugomvi na vurugu baina ya mashabiki wa pande mbili. Uhasama baina timu ya hizi mbili unahusishwa kwa kiasi kikubwa na historia ya nchi hiyo wakati wa harakati za kudai uhuru. Katika sehemu mbalimbali za nchi ya Aljeria mchezo baina ya timu hizi mbili hubakia kuwa ni tukio la kitaifa kutokana na kuzungumziwa na kupewa nafasi kubwa kwenye vyomo tofauti vya habari.

TP Mazembe dhidi ya FC Lupopo (R.D Congo). Jina la TP Mazembe sio geni miongoni mwa mashabiki wengi wa soka nchini Tanzania kutokana na wachezaji wa hapa nyumbani Mbwana Samata ambaye alifanikiwa kujitwalia taji la mchezo bora wa ndani wa Afrika na Thomas Ulimwengu kuchezea pale. Katika jiji la Lubumbushi kila mwaka kunakuwa na tukio kubwa la mchezo wa soka ambalo huwakutanisha watani wa jadi kati ya TP Mazembe na FC Lupopo.

Gor Mahia dhidi ya AFC Leopards (Kenya) - Nairobi au Mashemeji derby. Shamrashamra na tambo za mashabiki wa mchezo wa mpira miguu katika mitaa mbalimbali ya jiji la Nairobi huonekana wazi pindi timu za Gor Mahia na AFC Leopards zinapokutana. Mchezo huu ambao una historia ya muda mrefu kwenye soka nchini Kenya huchukuliwa kama ni siku kubwa ambapo mashabiki licha ya kuonyesha uhasama mkubwa lakini ni sherehe, likizo na huchukuliwa kama siku maalum.
Asec Mimosas dhidi ya Africa Sport Abidjan (Ivory Coast) - Abidjan derby. Miongoni mwa tukio baya kutokea pindi timu hizi mahasimu zinazotokea katika jiji la Abidjan nchini Ivory Coast ni mwaka 2001 ambapo vurugu zilitokea ambapo mtu mmoja alifariki huku 30 wakijeruhiwa. Timu ya Asec Mimosas inajivunia kwa kutoa vipaji vikubwa kabisa vya soka nchini humo na duniani wakiwemo Kolo Toure, Didier Drogba na Gervinho.

Al-Merreikh dhidi ya Al-Hilal (Sudani). Uhasama wa timu hizi mbili zinazotokea kwenye jiji la Omdurman nchini Sudan ambapo mnamo mwaka 1934 timu ya Al-Merreikh iliifunga Al-Hilal kwa mabao 2 bila ya majibu ambapo kulikuwa hakuna uwanja enzi hizo. Uhasama baina ya timu hizo mbili pia huchochewa kwa kiasi kikubwa na idadi ya wachezaji kila timu iliyo nayo kwenye kikosi cha timu ya taifa.      
Ipo michezo mingine mingi tu ya watani wa jadi kwenye soka lakini hiyo ndiyo mikubwa ambayo inasubiriwa na kuangaliwa zaidi. Jumia Travel inaamini kwamba sasa utakuwa umeijua na utaanza kuifuatilia kwani kuna burudani nyingi ulikuwa ukiikosa kwa kutoifuatilia. Mechi hizo kutokupewa nafasi kubwa na vyombo vya habari tofauti barani Afrika kama ilivyo kwa ile ya Ulaya haimaanishi kwamba haina ushindani mkubwa.

Friday, 25 August 2017

GSM MALL WAJA NA PROMOSHENI YA WIN GSM MALL EID FAMILY TRIP TO ZANZIBAR











Kampuni ya GSM imetoa promosheni kwa wateja wake watakaonunua bidhaa  kwa shilingi laki moja ambao wataingizwa kwenye droo maalumu itakayoa washindi atakaosafiri kwenda Zanzibar.

Wateja watakaoflka katika maduka yao kununua bidhaa mbalimbali zenye mapunguzo kama nguo za watoto ambazo bei yake imepunguzwa kwa asilimia 15, wataingizwa kwenye droo maalumu na mshindi kupatiwa zawadi.

Wednesday, 23 August 2017

JIONEE PICHA MBALIMBALI ZA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA, SIMBA WAKITWAA UBINGWA WA NGAO YA JAMII, YAICHAPA YANGA KWA PENATI 5-4 UWANJA WA TAIFA, TSHIMBI ANG'ARA



DKT. KALEMANI AITAKA TANESCO KUUNGANISHA NGUVU KUKAMILISHA MIRADI YA UMEME YA KURASINI NA KIMBIJI



NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani,(pichani anayeongea), amelitaka Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kuunganisha nguvu ili kuhakikisha wanakamilisha mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza na kusamabaza umeme kinachotarajiwa kujengwa huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Dkt. Kalemani ametoa maelekezo hayo leo Agosti 22, 2017, wakati alipofanya ziara kukagua miradi ya umeme kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kurasini, Kigamboni na eneo panapotarajiwa kujengwa kituo kingine cha kupoza na kusambaza umeme huko Kimbiji wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.
“Hakikisheni mradi wa uejenzi wa kituo hiki cha Kimbiji unakamilika ifikapo Machi 30, mwakani,(2018), na kuwaondolea adha ya upatikanaji wa umeme wananchi wa Kigamboni, chukueni mafundi waliokamilisha kazi ya kujenga kituo cha umeme kule Mtwara waje hapa, muwaache wale wanaojenga transition (njia ya kusafirisha umeme) wajenge, lakini wale mafundi wengine waleteni hapa ili mradi huu ukamilike.” Alifafanua.
Akiwa kwenye kituo cha kupoza na kusamabza umeme cha Kurasini jijini Dar es Salaam, Dkt. Kalemani aliipongeza TANESCO kwa juhudi kubwa walizofanya kwa hatua ujenzi waliyofikia ambapo sasa wameanza kufunga mashine kubwa. Kituo cha Kurasini ndicho kinachotegemewa sana na watu wa Mbagala, Kurasini na Kigamboni.
Ongezeko la haraka la wakazi kwenye maeneo ya Mbagala, na Kigamboni kumepelekea uhitaji mkubwa wa umeme ambapo umeme unaopatikana kwa sasa umekuwa haukidhi mahitaji ya wakazi wa maeneo hayo.
“Naomba niwaambie, mradi huu umechelewa sana, hivyo basi ongezeni kasi ili ifikapo Agosti 30, mwaka huu, mradi ukamilike nataka watu wa Mbagala, watu wa Kurasini, na watu wa Kigamboni wanaondokana na kero hii ya umeme, na mimi nitawaambia washeshimiwa wabunge wa Kigamboni Mheshimiwa Ndungulile (Dkt. Faustin Ndungulile) na Mheshimiwa Mangungu (Murtaza Magungu) Mbunge wa Mbagala kuhusu habari hii ili wawaambie wananchi wa maeneo haya wawe wavumilivu kwani mradi huu sasa utakamilika.” Alisema.
Dkt. Kalemani pia aliwaagiza viongozi wa TANESCO, kuhakikisha wanakusanya nguvu kwa maana ya vifaa kutoka ofisi zote za TANESCO mkoa wa Dar es Salaam, ili kuhakikisha wananchi wote wa Kigamboni wanaofikia 350 waliolipia ada za kuunganishiwa umeme wawe wamepelekewe umeme ifikapo mwisho wa mwezi huu wa Agosti.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, aliwaambia waandishi wa habari kuwa maelekezo ya Mheshimiwa Naibu waziri yatafanyiwa kazi kwa haraka ili kuhakikisha kero hiyo inaondoka.
Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam

 Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James,(kulia), akimpatia maelezo Naibu waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme Kurasin jijini Dar es Salaam
 Dkt. Kalemani (katikati), akitoa maagizo kwa wakandarasi wanaotekeleza mradi huo wa Kurasini.

Meneja Mwandamizi wa TANESCO Kanda ya Dar es Salaam na Pwani, Mhandisi Mahende Mgaya, (watatu kushoto), akimpatia maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha umeme cha Kigamboni, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wapili kushoto)

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka, (kulia), akiwa na  Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia miradi, Mhandisi Khalid James, (kushoto), akiongea na waandishi wa habari.



Tuesday, 22 August 2017

FLOYD MAYWETHER Jr. vs CONOR MACGREGOR JUMAPILI HII LIVE DSTV


DStv Inakuletea chaneli maalum itakayorusha Matukio kuhusu  pambano la “The Money Fight”
Ule mpambano unaosubiriwa kwa hamu dunia nzima uliopewa jina la “The Money Fight” kati ya Floyd Mayweather Jr. vs Conor McGregor upo karibuni na Dstv kwa kuwajali wateja wake kwa namna ya kipekee sana ambapo imewaletea  chaneli maalum ya muda (pop-up channel) kabla ya pambano kubwa la The Money .
Chaneli hii itapatikana kwenye DStv namba 213 inapatikana sasa kwa wateja wote wa DStv kuanzia kifurushi Premium 184,000 mpaka kifurushi Bomba sh.19, 975 na chaneli hiyo itaanza siku ya  Jumamosi, 19 Agosti  na kuruka kila siku kuanzia saa 12:00 jioni - 08:00 usiku na kuendelea mpaka usiku wa pambano lenyewe siku ya Jumapili, Agosti 27 kabla ya pambano hili kuanza.

Chaneli hiyo (Dstv 213) itakuwa na ratiba kabambe ya mapigano mengi ya Mayweather, ziara yake ya Afrika mwaka 2014.
Kutakuwa na Nguo za thamani, maburungutu ya fedha, magari na lugha za kebehi. Hiyo yote ni kuleta mvuto kwenye pambano hili .

Kumbuka Pambano hili litarushwa LIVE na Dstv pekee kupitia SS2 Dstv 202 kuanzia kifurushi Premium sh.184,000 tu saa 8:00 usiku-2:30 asubuhi!

Wasiliana nasi kwenye mitandao ya kijamii, Facebook, Twitter na Instagram tunapatikana kwa jina @DstvTanzania.

Monday, 21 August 2017

WANACHAMA 1,216 WAPITISHA UAMUZI WA KLABU YAO KUANZA KUENDESHWA KIMFUMO WA HISA...










Wanachama 1,216 wa klabu ya Simba, leo wamepitisha uamuzi wa klabu yao kuanza kuendeshwa kwa mfumo wa hisa.

Mwanachama mmoja pekee katika mkutano huo, ndiye alionyesha hisia zake kwa kupinga mfumo huo.

Wanachama bado wataendelea kubaki kuwa wamiliki wa klabu hiyo kwa asilimia 50 huku wawekezaji nao wakilimiliki kwa asilimia 50 pia.

Mbadiliko yaliyopitishwa na wanachama wa Simba yako hivi, wanachama watamiliki klabu yao kwa 50% huku 50% zikilikiwa na wawekezaji.

Wawekezaji au mmoja, wawili au watatu watatakiwa kutoa Sh bilioni 20 katika uwekezaji huo sawa na wanachama.

Kwa wanachama, kwa kuwa wanaonekana si wenye uwezo wa kutosha kifedha, wao watatakiwa kuchangia Sh bilioni 4 tu ambazo nia silimia 10 huku 40 ambayo ni bilioni 16 zitawekwa kando kwa kuangalia uwezo wao.

Suala la nani atakuwa mwekezaji itaundwa kamati baada ya watu kujitokeza, nayo itaandaa mkutano kuwaita wanachama kuwaeleza waliojitokeza katika uwekezaji ni akina nani.


Wawekezaji wanaweza kuwa wawili, watatu au vinginevyo na mgawanyo wa hisa kwa maana ya thamani na asilimia ndiyo utakaohusika.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube