BREAKING

Friday, 21 August 2015

STARS KUELEKEA UTURUKI JUMAPILI



Kikosi cha wachezaji 22 kinachounda timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars' kinatarajia kuondoka nchini Jumapili wiki hii  kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mechi yake dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam,Afisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Baraka Kizuguto amesema kuwa kikosi hicho kitaweka kambi ya wiki moja nchini Uturuki katika jiji la Estanbull pamoja na kucheza michezo miwili ya kirafiki ikiwemo dhidi ya Libya

Aidha kizuguto amesema kuwa timu hiyo itawakosa baadhi ya nyota wake watano wa kimataifa akiwemo mchezaji Mbwana Samata,Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa , Hassan Seif, Pamoja na mshambuliji Haji Yusuph.

Kikosi hicho cha kocha mzawa  Charles Boniface Mkwasa inakibarua kizito dhidi ya kikosi cha Nigeria chini ya kocha wake mpya Sunday Olise September 5 mwaka huu kwa jili ya kufuzu michuano ya AFCON.

MECHI ZA LIGI KUU YA UINGEREZA

 

Latest Football

 
 
Louis van Gaal, Roberto Martinez, Arsene Wenger
JUMAMOSI  22 Aug 2015 - Premier League
  • Man Utd v Newcastle 12:45
  • Crystal Palace v Aston Villa 15:00
  • Leicester v Tottenham 15:00
  • Norwich v Stoke 15:00
  • Sunderland v Swansea 15:00
  • West Ham v Bournemouth 15:00
JUMAPILI  23 Aug 2015 - Premier League
  • West Brom v Chelsea 13:30
  • Everton v Man City 16:00
  • Watford v Southampton 16:00
JUMATATU  24 Aug 2015 - Premier League
  • Arsenal v Liverpool 20:00
Sat 29 Aug 2015 - Premier League
  • Newcastle v Arsenal 12:45
  • Aston Villa v Sunderland 15:00

Thursday, 20 August 2015

OTAMEND KUJIUNGA NA MANCHSTER CITY

http://images.football365.com/15/06/800x600/Nicolas-Otamendi_3314055.jpg

Manchester City wamemsajili mlinzi wa kimataifa wa Argentina Nicolas Otamendi kutoka klabu ya Valencia kwa mkataba wa miaka mitano.

 Mchezaji huyo mwenye miaka 27 alitajwa katika kikosi bora cha La Liga msimu wa 2014-15 na aliisaidia nchi yake kufika fainali ya Kopa Amerika mwaka huu.

Akizungumza mudfa mfupi baada ya kunayiwa vipimo vya afya  otamendi amesema kuwaa ndani ya klabu hiyo ambao nui matajiri pekee katika jiji la manchster kunamfanya ajione kuwa ni miongoni mwa  wachezaji  muhimu katika ramani ya soka 

kwa upande wake kocha wa kikosi mancheter  City Manuel Pellegrini amesesema kwa sasa ana imarisha safu yake ya ulinzi ili kukaba;liana na wapinzani wake katika mbio za kuwania ligi kuu uingetreza msiomu huu

Kikosi hicho cha city wiki iliyopita kilishushia kikchapo kikali cha bao 3-0 matajiri wa jiji la london chelsea thew blues

MWANARIADHA MLEMAVU OSCAR PISTORIUS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE C

 
 
Michael Masutha ambaye ni waziri wa sheria nchni Afrika kusini amasema kuwa uamuzi wa kumuachilia mwanariadha huyo umechukuliwa mapema mno

Oscar Pistorius amekaa gerezani kwa muda wa miezi kumi baada ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp na alitarajiwa kuachiliwa ili atumikie kifungo chake cha nyumbani kuanzia kesho
 
Mwanariadha huyo mwenye ulemavu raia wa Afrika Kusini alipatikana na hatia ya mauaji ya mpenzi wake ambapo anatarajiwa kuwa huenda  akaachiliwa huru hapo kesho Agosti 21.

Kwa mujibu wa taarifa za idara ya magereza ya Afrika Kusini mwanariadha huyo aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huenda akasamehewa na kutumikia kifungo cha nje.

Oscar alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela katika kesi iliyovuta hisia kali kote  ulimwenguni ambapo inadhaniwa kuwa alimpiga risasi mpenzi wake akidai kuwa alidhani ni wezi wanaingia kwake katika siku ya wapendanao yaani Valentines Day

TIMU YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 15,KUANZA ZIARA BARANI AFRICA.

 Jamali Malinz akizungumza na waandshi wa Habari, wa kwanza kulia nai Ayub Nyenzi Mwenyekiti wa timu za Vijana.


 Timu ya soka taifa chini ya miaka ya 15 inatarajia kuanza ziara yake ya kimataifa barani Afrika mwezi desemba mwaka huu kwa ajili maandalizi ya kufudhu kwa michuano ya afrika chini ya miaka 17 itakatofanyika madagascar 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Rais wa shirikisho la soka Tanzania Tff Jamal Malinzi amesema timu hiyo itaanza ziara yake mwishoni mwa mwaka katika nchi za zambia , Zimbabwe, Botswana pamoja na nchi za kusini mwa afrika

Aidha malinzi amesema kuwa Tff imeingia mkataba na kituo cha ukuzaji wa vipaji cha Alliance cha jjini mwanza kwa ajili ya kuwatunza vijana 20 waliopatikana kwenye mashindano ya taifa chini ya miaka 15.

Katika hatua nyingine malinzi ameeleza kuwa shirikisho hilo limewatafutia nafasi vijana watano kujiunga  na klabu maarufu ya Orlando Pirates inayoshiriki ligi kuu soka ya Afrika kusini.

Wednesday, 19 August 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE, AMTAMBULISHA MGOMBEA URAIS NA MGOMBEA MWENZA WA CCM, KWA WAZEE WA DAR ES SA

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha Mhe Samia Suluhu Hassan, Mgombea mwenza wa ugombea Urais kwa tiketi ya Chama hicho tawala Dkt John Pombe Magufuli leo Agosti 19, 2015 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
 Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam leo Agosti 19, 2015.
 Meza Kuu ikimfurahia Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wazee wa Dar es salaam leo katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

 Mwenyekiti wa Wazee wa CCM wa Dar es salaam akipeana mikono na Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM  tawala Dkt John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza Bi Samia Suluhu Hassan baada ya kuongea na wazee wa Dar es salaam.
   Meza Kuu Ikifurahia Jambo.

BODI YA LIGI YATANGAZA RATIBA YA LIGI KUU YA TANZANIA BARA SIMBA NA YANGA USO KWA USO SEPTEMBER 26

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara Boniface Mgoyo Wambura akizungumza na waandishi wa habari,kushoto kwake ni Afisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania TFF Baraka Kizuguto.

Wababe wa soka wenye upinzani mkubwa wa soka nchini Tanzania Timu ya Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara September 26, mwaka huu.

Boniface Wambura ni Mtendaji Mkuu wa bodi ya Ligi Kuu, ametaja ratiba lakini mvuto wa ratiba hiyo umekuwa kwa timu hizo mbili ambazo zinaupinzani mkubwa wa kisoka kuanzia kwa mashabiki na soka Uwanjani.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube