BREAKING

Thursday, 7 January 2016

MKAPA NA JAJI WARIOBA WAMTEMBELEA RAIS MAGUFULI IKULU, WAMTAKIA MWAKA MPYA NA MAJUKUMU MEMA


Tuesday, 5 January 2016

KOCHA MPYA WA REAL MADRID ZINEDINE ZIDANE AANZA KUKINOA KIKOSI CHAKE, MUDA MFUPI BAADA YA KUTANGAZWA

 Zidane akiwa katika mazoezi ya kwanza na kikosi cha Madrid , hapa akimwelekeza mshambuliji KarimBenzema, jambo.


 Zidane akifuatilia kwa makini mazoezi ya Madrid







REAL MADRID ILIVYO MUONYESHA NJIA YA KUTOKEA BENITEZ......

  Rafael Benitez Out Madrid

 Zinedine Zidane in Madrid

Mwanandinga wa zamani wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa  Zinedine Zidane ameteuliwa kuwa kocha mpya wa klabu ya Real Madrid akirithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mhispania Rafael Benitez.

Zidane almaarufu kama Zizou amechukua nafasi hiyo ikiwa ni miezi saba tangu Rafael Benitez akamatie kiti hicho na kuifanya klabu hiyo  kuwa na mwenendo mbaya ikiwemo sare ya bao 2-2 na Vallencia na kupelekeaMabingwa hao wa zamani wa la liga kushika nafasi ya 3 wakiachwa alama 4 na kinara wa ligi ya hispania klabu ya Athletico Madrid.

Zidane mwenye miaka 43 ambae alishinda mataji akiwa na Real Madrid katika ngazi ya uchezaji alitangazwa  mapema jana na Mmiliki wa klabu hiyo Florentino Perez's akittokea kukinoa kikosi B cha real Madrid.

Mfaransa huyo atakuwa kocha wa 11 katika kipindi cha miaka 12 kupata kukinoa kikosi hicho wakati kibarua chake cha kwanza kikiwa dhidi ya Deportivo la Coruna siku ya Juamosi.


Monday, 4 January 2016

WATU 4 WAMEPOTEZA MAISHA NA WENGINE 35 WAMEJERUHIWA KATIKA AJALI ILIYOTOKEA KATIKA KIJIJI CHA KINEGEMBASI WILAYANI MUFINDI MKOANI IRINGA NA KUHUSISHA BASI LA ABIRIA LA KAMPUNI YA LUWINZO PAMOJA NA LORI LA MIZIGO




WATU 4 wamepoteza maisha na wengine 35 wamejeruhiwa baadhi yao wakiwa katika hali mbaya baada ya basi la abiria mali ya kampuni ya LUWINZO linalofanya safari zake kati ya Dar Es Salaam na Njombe kuligonga kwa nyuma gari kubwa la mizigo katika kijiji cha Kinegembasi kata ya Mbalamaziwa wilayani Mufindi mkoani Iringa.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi majira ya saa 3 ambapo basi hilo lilikuwa likitokea mkoani Njombe kuelekea jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa, Peter Kakamba amezitaja nambari za usajili za magari hayo yaliyohusika katika ajali hiyo kuwa ni T 782 AZR ambalo ni basi la LUWINZO na T 718 CRV lori la mizigo lililokuwa limebeba shehena ya makaa ya mawe.

Kamanda Kakamba amesema ajali hiyo imetokea baada ya dereva wa basi hilo kujaribu kulipita lori la mizigo lililokuwa likitokea mkoani Ruvuma kuelekea mkoani Tanga na kwamba watu wawili wamepoteza maisha katika eneo la ajali na wengine wawili wamefariki wakiwa njiani wakati wakipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi.

Amewataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni Rashidi Kibalala,. Salim Changwila  ambao wote walikuwa wafanyakazi wa basi hilo.
Aidha amesema majina ya marehemu wengine wawaili bado hayajajulikana huku akibainisha chanzo cha ajali hiyo kuwa ni uzembe wa madereva na mwendo kasi.



ZOEZI LA KUWEKA ALAMA ZA X KWENYE NYUMBA ZINAZOPASWA KUBOMOLEWA LIMMEENDELEA KATIKA MAENEO YA MABONDENI JIJINI DAR ES SALAAM CHINI YA ULINZI MKALI WA JESHI LA POLISI KIKOSI CHA KUTULIZA GHASIA


Zoezi la kuweka Alama za X kwenye nyumba zinazopaswa kubomolewa limeendelea leo katika maeneo ya mabondeni jijini Dar es Salaam ambapo nyumba zaidi ya 3500 zimewekwa alama hiyo katika eneo la bonde la mto Msimbazi.

**Katika kutekeleza zoezi hilo, zaidi ya askari elfu moja wa kikosi cha kuzuia ghasia FFU cha Jeshi la Polisi wameimarisha Ulinzi katika maeneo mbalimbali ya mabondeni kutokana na kushambuliwa kwa mawe hivi karibuni baadhi ya maafisa kutoka ardhi waliokuwa wakiendesha zoezi hilo katika maeneo ya jangwani ambapo wananchi pia walifunga barabara kwa matairi na kuchoma moto kupinga zoezi hilo.

Maeneo yaliyokumbwa na zoezi la kuwekwa alama za x ni pamoja na nyumba zote zilizopo eneo la jangwani, upande wa kigogo sambusa,kigogo mbuyuni pamoja na nyumba zilizopo katika eneo la sukita , ambapo utekelezaji wa kuweka alama hizo umewaacha baadhi ya wamiliki wakiangua vilio ,wengine kuanguka na kupoteza fahamu huku baadhi wakiduwaa kwa kushindwa kujua hatua gani wachukue kutokana na wengine kuwa na majengo mapya ya gharama ambayo wamejenga kando ya mto msimbazi.

Akizungumza na mtandao huu wa Shamakala360 Afisa mwandamizi kutoa baraza la taifa la usimamizi wa mazingira NEMC- Anold Kisiraga amesema zoezi la kubomoa nyumba linaanza rasmi kesho kwa wale waliopinga kubomoa kwa hiari yao huku pia akisisitiza kuwa zoezi hilo litaenda sambamba na uwekwaji wa alama za x kwenye nyumba ambazo zitakumbwa na zoezi hilo.

Wakati huo huo Ombi la wakazi zaidi ya 600 wa mabondeni wakiongozwa na Mbunge wa Kinondoni ambao wamefungua kesi katika mahakama ya kuu kitengo cha ardhi kusitishwa zoezi hilo limesogezwa mbele mpaka kesho saa tano .

Tuesday, 29 December 2015

MAKONTENA MENGINE 11,884 YAGUNDULIKA KUPOTEA,Proffessa MAKAME MBARAWA,AAGIZA KUSAKWA KWA WEZI NANE WALIOKIMBIA







Wafanyakazi wanane wa mamlaka ya bandari kitengo cha makasha ya bidhaa,yaani CONTAINER'S,wamekimbia ajira zao kufuatia serikali kuwakamata wenzao 7 wanaotuhumiwa kuwa vinara wa kuikosesha serikali mapato kwa kuyapitisha kinyemela makasha hayo bila ya kulipiwa ushuru wa forodha.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo asubuhi bandarini hapo,waziri wa uchukuzi,ujenzi na mawasiliano,Proffessa MAKAME MBARAWA,alisema kuwa wafanyakazi hao walikimbia baada ya tume maalum iliyoundwa ili kufuatilia upotevu wa makasha hapo bandari na kugundua makasha 300 hayaonekani kama yamepitia njia sahihi za kutolewa katika bandari kavu,kugundua kuwa kuna mengine 11,884 yalipotea kwa mtindo uleule wa yale ya awali.

Amesema inaonekana kuwa wafanyakazi hao walikuwa na ushirikiano na mawakala wa makasha wasiokuwa waaminifu kwa kushirikiana kuidanganya mamlaka ya mapato nchini,TRA,ikishirikiana na wafanyakazi wasio waaminifu wa TRA,pamoja na mamlaka ya Bandari kuhusu ulipaji wa WHARFAGE(TOZO YA BANDARI) huku wakijua kuwa ni kosa.


Aidha amesema kuwa mawakala wa forodha 243 wamepewa siku 7 kukamilisha malipo ya makasha na magari yaliyotolewa bandarini hapo bila ya kulipiwa tozo ya bandari kufanya hivyo katika muda huo vinginevyo serikali italazimika kuwakamata na kuwafikisha polisi ili walipe na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufungiwa kufanya biashara na mamlaka ya bandari.

Kwa upande wake naibu waziri wa wizara hiyo,Injinia EDWIN NGONYANI,amesema kuwa kuna malalamiko kuwa wapo mawakala wa forodha ambao wanadai wamelipia fedha za tozo lakini bado wanahesabiwa kuwa hawajalipa,amewataka kuwasilisha nyaraka stahiki zitakazoonesha kuwa wamelipia tozo hizo kihalali ili hatua stahiki zichukuliwe.

Akihitimisha kuwasomea taarifa hiyo waandishi wa habari,waziri Professa Mbarawa amesema serikali haitamvumilia mfanyakazi yeyote wa mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini awe mkubwa au mdogo ambae ataendelea na kujihusisha na upotevu wa mapato ya mamlaka ya bandari hiyo pia inahusisha mawakala wote wa forodha ambao wataendelea kujihusisha na wafanyakazi wa mamlaka ya bandari kutoa mizigo bila ya kulipa tozo watafutiwa leseni zao.



Monday, 28 December 2015

YANGA YAVUNJA MKATABA NA NIYONZIMA,YAMUAMURU KULIPA KITITA CHA FEDHA DOLA ZA KIMAREKANI ZAIDI YA 71 ELFU





Uongozi wa Klabu ya Soka ya Yanga umetangaza kuachana na kiungo wa Yanga ambaye pia ni Nahodha wa timu ya taifa ya Rwanda Haruna Niyonzima baada ya nyota huyo kuelezwa kuwa amekuwa na utovu wa nidhamu kwa muda mrefu.

Uongozi huo umeachana na Nyota huyo, huku wakimdai kuwalipa Yanga kiasi cha Dola za kimarekani zaidi ya  elfu 71.

Kuvunjwa kwa mkataba huo na Yanga kumekuja baada ya Nionzima kushindwa kufika kwa wakati katika kambi ya timu hiyo mara baada ya kwenda kwao kuitumikia timu ya Taifa , kwani hata mara baada ya kurejea nyota huyo hakufika kambini kwa wakati.



 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube