BREAKING

Friday, 30 March 2018

USENGIMANA NA SINGIDA UNITED MAMBO MAGUMU AONDOKA KAMBINI ATUA ZAKE KIGALI, UONGOZI NAO WASHINDWA KUWEKA MAMBO HADHARANI




Kuna taarifa za kuwa mshambuliaji wa Singida United, Mnyarwanda, Danny Usengimana ameondoka ndani ya kikosi chake baada ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kummalizia fedha zake za usajili na kuamua kurejea kwao,
Rwanda.

Chanzo cha habari kimedai kuwa Usengimana aliondoka ndani ya timu hivi karibuni baada ya kushindwa kuelewana katika maslahi na inadaiwa anaidai timu hiyo kiasi cha fedha zake za usajili ambazo hajamaliziwa na si yeye
pekee bali kuna wachezaji wengine ambao wanadai fedha hizo.

Hata chanzo hicho kilienda mbali zaidi na kudai kuwa mchezaji huyo imebidi kuondoka kambini na kuweza kurejea nchini kwao Rwanda huku timu ikiwa kambini kwa maandalizi ya FA dhidi ya Yanga.

Alipotafuywa Mkurugezni wa Singida United, Fest Sanga kuweza kupata taarifa kuhusiana na mshambuliaji huyo:

“Kwa sasa timu ipo inaendelea na maandalizi hapa kambini na Danny Usengimana ni kweli hayupo amerejea kwao kwa ruhusa maalum baada ya kuwa na matatizo ya kifamilia
akimaliza ataungana na wenzake inaweza kuwa kabla ya mchezo na Yanga au baada ya mchezo huo.”

Taarifa nyingine zimeeleza Singida United iko katika juhudi kubwa kuhakikisha inamalizana na Usengimana ili mambo yake sawa.

MAONYESHO YA YOUNG SCIENTISTS TANZANIA (YST) 2018 KUFANYIKA MWEZI AGOSTI

Mwanzilishi Mwenza wa  Young Scientists Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu maonyesho ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatakayofanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland. 
Meza Kuu pamoja na wadhamini wa maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Karimjee Jinanjee Foundation (KJF), Yusuf Karimjee akizungumzia udhamini wao 
Patricia Mhondo kutoka Kampuni ya Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) akizungumza kwenye mkutano huo.
Joseph Clawry kutoka nchi ya Iland akizungumzia kazi za ubunifu na jinsi nchi yao inavyowawezesha wanafunzi waliofanya vizuri katika miradi yao.
Muonekano wa chumba cha mkutano huo.
MAONYESHO ya Young Scientists Tanzania (YST) 2018 yatafanyika mwezi Agosti mwaka huu Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre (JNICC) jijini Dar se Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mwanzilishi Mwenza wa YST, Dk. Gosbert Kamugisha alisema maonesho hayo yatafanyika kuanzia tarehe moja hadi mbili mwezi huo.

"Wanafunzi wote wanaopenda kushiriki wanashauriwa kutuma kazi za miradi yao kwenda YST kabla ya tarehe 21 Aprili 2018" alisema Kamugisha.

Kamugisha alisema wanafunzi 200 watakaochaguliwa wataonyesha kazi za teknolojia na ugunduzi wa kisayansi kwenye onesho hilo la mwaka huu na kuwa na wanafunzi watakaochaguliwa watapewa mafunzo kutoka kwa washauri wa sayansi wa YST kuhusu namna ya kutengeneza kazi zao za kisayansi.

Alisema onesho hilo pamoja na mpango wa kuzitembelea shule na wanafunzi kuwapatia ushauri wa kisayansi vinawezeshwa na wadhamini wakuu wa YST ambao ni Shell Explorstion snd Production Tanzania Ltd (shell) na Karimjee Jinanjee Foundation (KJF)

"Tunapenda kuwashukuru wadhamini wetu tangu mwaka 2012. Mwaka huu wa 2018 KJF wameongeza kiwango cha udhamini na kuwa mmoja wapo wa wadhamini wakuu wa YST kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Alisema udhamini huo utaiwezesha programu ya YST kuwa endelevu na kuwawezesha vijana kufanya ubunifu na kufanya tafiti za kisayansi ili kuleta maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kamugusha aliongeza kuwa wanasayansi chipukizi wakaoshiriki onesho la YST mwaka huu kwa sasa wanaendelea kutengeneza kazi za miradi yao katika nyanja mbalimbali za kisayansi kama kemia, fizikia na hesabu, biolojia na ekolojia, saynsi ya jamii na teknolojia na kuwa kazi miradi nyingi zimejikita katika sekta ya afya,kilimo na usalama wa chakula, mawasiliano na usafirishaji, nishati,elimu, mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Alisema wanafunzi watakajituma na kufanya ugunduzi mzuri watazawadiwa pesa taslimu, medali, vikombe na uimarishaji wa maktaba ya shule yao kama ambavyo wamefanya kwa miaka sita iliyopita KJF watawazadia wanafunzi wenye ugunduzi mzuri zaidi zawadi za udhamini wa masomo ya chuo kikuu ili kuwawezesha kusoma masomo ya sayansi na teknolojia katika ngazi ya chuo kikuu.

Wednesday, 28 March 2018

MBWANA SAMATTA ASEMA TANZANIA ITAVUMA KIMATAIFA ZAIDI KUTOKANA NA WACHEZAJI VIJANA KUWA WENGI KWA SASA


Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ambaye pia anasakata kandanda la kulipwa Ubelgiji Mbwana Ally Samatta, amesema vipaji Tanzani vipo nabado muda mchache Tanzania itafanya vyema kimataifa.

Nyota huyo amesema hayo mara baada ya timu ya Tanzania kuonyesha kiwango kikubwa katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki baada ya kuifunga Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mabao 2-0 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Pongezi kwa wafungaji wa mabao hayo, Nahodha Mbwana Ally Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji na Shiza Ramadhani Kichuya wa Simba.

Huo unakuwa ushindi wa kwanza Tanzania tangu Julai 7 mwaka jana ilipoichapa kwa matuta Lesotho baada ya sare ya 0-0 kwenye Kombe la COSAFA mjini Rusternburg, Afrika Kusini.

MBUNGE ROSE TWEVE KUWAWEZESHA WANAWAKE WA UWT MKOA WA IRINGA

 Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose tweve akiwa na naibu katibu mkuu bara wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi (UWT) taifa Eva Kihwele pamoja na katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizerwakiangalia shughuli zinazofanywa na vikundi vya wanawake wa UWT tafasa ya mazombe
Attachments area Preview YouTube video MBUNGE ROSE TWEVE KUWAWEZESHA WANAWAKE WA UWT MKOA WA IRINGA

Wednesday, 14 March 2018

UNAZIFAHAMU HOTELI TANO ZA KUVUTIA ZAIDI ZINAZOPATIKANA PEMBEZONI MWA TANZANIA?


Zimebaki takribani wiki tatu kabla ya sikukuu ya Pasaka kusherehekewa duniani kote, je umeshafahamu utakwenda kupumzika wapi? 

Pasaka ni miongoni mwa sikukuu zinazopendwa na watu wengi kwa sababu husherehekewa kwa takribani wiki moja. Wakati wa sherehe hizi watu huitumia fursa hiyo kwa kufanya mapumziko ya muda mfupi kabla ya kurejea kwenye shughuli zao za kila siku.

Katika kukusaidia sehemu za kwenda kutembelea sikukuu hii, Jumia Travel imekukusanyia hoteli tano za kuvutia zilizopo pembezoni mwa Tanzania ambazo unaweza kwenda kupumzika kipindi cha likizo hii fupi.

Lupita Island Lodge. Ni hoteli ya kuvutia na tulivu inayopatikana kwenye kisiwa kinachomilikiwa na mtu binafsi ndani ya ziwa Tanganyika. Hoteli hii ina kiwanja binafsi cha ndege na boti ambazo huwachukua wageni kutoka nchi kavu mpaka kisiwani. Hii ni sehemu ambayo unapaswa kwenda kwa ajili ya mapumziko kwa sababu hata namna ya muundo wa vyumba na mazingira yake yamewekwa kumpatia mtu utulivu na usiri akiwa mapumzikoni. Miongoni mwa shughuli za kuvutia ukiwa kisiwani hapa ni pamoja na kutembelea kijiji cha wavuvi, kutalii ziwani kwa kutumia boti na burudani za maonyesho ya kiasili kutoka kwa wanakijiji.  

Katuma Bush Lodge. Ikiwa inapatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Katavi, hoteli hii imejengwa katika mtindo wa kuvutia na kustarehesha kwa kutumia mahema. Eneo hili linatoa wasaa mzuri kwa wateja kutembelea mbuga yenye mandhari nzuri ya uwanda wa Katisunga. Kwa kuongezea, ni sehemu nzuri kwa watalii ambao wangependa kutembelea na kujionea mazingira mapya tofauti na yale waliyokwishayazoea.  

Wag Hill Lodge & Spa. Hoteli ina mazingira tulivu na vifaa vya kisasa, sehemu kwa ajili ya michezo ya watoto na mandhari nzuri ya Ziwa Victoria, inafaa zaidi kwa mapumziko ya kifamilia na watalii wanaotafuta sehemu nzuri ya kustarehe. Inapatikana kwa mwendo wa dakika 30 kwa kuendesha gari kutokea jijini Mwanza.  

Kigoma Hilltop. Ikiwa ni kituo cha kuvifikia kwa wepesi vivutio vya kitalii katika ukanda wa Magharibi, hoteli hii ya kisasa imejengwa mbali kidogo na mji, kwenye eneo kubwa la milima linalotazamana na Ziwa Tanganyika. Ukiwa hotelini hapa utafurahia mandhari nzuri ya kuvutia ya Ziwa Tanganyika, lenye sifa ya urefu na kina kirefu Afrika na duniani, kutoka kwenye kila chumba. Shughuli za kitalii zipo lukuki mkoani Kigoma kama vile safari za boti ziwani, kupiga mbizi ziwani, kutalii miji ya kihistoria ya Ujiji na Livingstone pamoja na safari ya siku nzima ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Gombe.   

Kungwe Beach Lodge. Ni hoteli ya kifahari yenye ufukwe wa kuvutia inayopatikana kwenye Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Mahale. Ukiachana na mazingira tulivu na vyakula mbalimbali, mgeni anaweza kufurahia shughuli kama vile ziara ya kwenda kuwaona sokwe, kutazama ndege wa mwituni, kutalii mbugani, safari ya boti ziwani, uvuvi, pamoja na matembezi binafsi kwenye fukwe safi pembezoni mwa Ziwa Tanganyika.

Maeneo ya kutembelea ni mengi na yanafikika kwa urahisi zaidi na gharama nafuu endapo utaanza kufanya maandalizi mapema. Sikukuu zinakaribia, naamini miongoni mwenu mtakuwa na mapumziko mafupi. Hivyo ni vema kukitumia kipindi hiko kufanya kitu ambacho kitaacha kumbukumbu katika mwaka huu. Unaweza kufahamu mengi zaidi juu ya sehemu hizo kupitia mtandao wa Jumia Travel.

MAN UNITED GONJWA LAKE NI KUBWA, YACHAPWA MABAO 2-1 NYUMBANI NA SEVILLA,MOURINHO AWA TATIZO...
































Tuesday, 13 March 2018

MAN CITY HAISHIKIKI LIGI YA UINGERZA YAICHAPA STOKE CITY BAO 2-0

 David Silva akiifungia bao la kwanza Manchester City kati ya mabao mawili aliyofunga ambalo la kwanza alifunga dakika ya 10 na la pili dakika ya 50 katika ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Stoke City kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England usiku wa jana Uwanja wa Bet365. 

Man City inafikisha pointi 81 baada ya kucheza mechi 30, ikifuatiwa kwa mbali na Manchester United yenye pointi 65 za mechi 30, kocha Pep Guardiola atahitahji kushinda mechi mbili zaidi kujihakikishia ubingwa wa England






























 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube