BREAKING

Wednesday 5 December 2018

MRADI WA LTA WAMALIZA MIGOGORO YA ARDHI KATIKA KIJIJI CHA MAGUBIKE KWA KUTOA HATI MILIKI ZA KIMILA


Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakati wa kukabidhi hati miliki za kimila kwa wananchi wa kijiji cha Magubike kilichopo kata ya Nzii mkoani Iringa 
 Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakimkabidhi hati mmoja wa wananchi wa kijiji cha Magubike
Mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa akiwa na mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa wakicheza nyimbo za asili pamoja na wananchi wa kijiji cha Magubike wakati wa ugawaji wa hati za kimila

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Migogoro ya ardhi katika kijiji cha magubike kata ya nzii wilaya ya iringa imebakia kkama historia baada ya mradi wa feed the future (LTA) kufanikiwa kupima ardhi na kuwakabidhi hatimiliki ya kimila kwa wananchi wa kijiji hicho.

Akizungumza wakatika wa kukabidhi hati hizo za kimila mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Stephen Mhapa alisema kuwa kutolewa kwa hatimikili za kimila kunamaliza migogoro ya ardhi kwa wananchi wote waliopata hati hizo.

“Sasa tunaelekea kipindi cha kilimo ambapo ndio kuna kesi nyingi za mipaka ya ardhi, hivyo uwepo wa mradi huu wa LTA umetusaidia kumaliza kabisa migogoro ya ardhi naomba kuchukua nafasi hii kwa niaba ya serikali kuwashukuru kwa kazi mliyoifanya” alisema Mhapa

Mhapa aliwaomba viongozi wa mradi wa LTA kuhakikisha wanapima vijiji vyote vya halmashauri ya wilaya ya Iringa ili kuondoa migogoro yote ambayo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi.

“Kama serikali ikisema ipime ardhi yote ni kazi nzito,kazi hii ilitakiwa kufanywa na serkali kutokana na ukosefu wa rasilimali fedha na rasilimali watu imekuwa tatizo kubwa kwa serikali hivyo lazima mpongezwe kwa kazi yenu mnayoifanya” alisema Mhapa

Aidha Mhapa alisema kuwa kutolewa ka hati miliki za kimila zinaondoa kabisa mfumo dume kwa kuwa kwa sasa wanawake nao wamepewa hati kutoka kwa waume zao.

“Akina mama walikuwa hawatambuliwi kutokana na mila zetu zilivyo lakini hii leo kupitia mradi wa feed the future (LTA) wanawake hii leo wanamiliki ardhi na kuondoa kabisa mfumo dume kwenye sekta ya ardhi na kuwa na maamuzi ya matumizi ya ardhi yao” alisema Mhapa

Mhapa aliwataka wananchi wa kijiji cha Magubike wazingatie kuzitunza hati miliki za kimila kwa kuwa sasa ni dhamana ya maisha yetu hivyo mnatakiwa kuwa makini kwa kuzitunza vilivyo hati hizo.

Naye naibu mkurugenzi wa mradi wa feed the future Malaki Msingwa amesema kuwa kupatikana kwa hati hizo kunawakuwa na uhakika wa kumili ardhi ambayo huwezi kusumbuliwa na mtu yeyote Yule.

“mradi huo umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutoa Hati kwa usawa Wanawake na Wanaume” alisema Msigwa

Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Magubike kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.

“Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa

Msigwa alisema kati ya vijiji hivyo 41 vitakavyotayarishiwa mipango ya matumizi bora ya ardhi na kila mwenye ardhi kupimiwa na kupewa hati miliki za kimila, vijiji 36 vipo wilayani Iringa na vitano vipo wilayani Mbeya.

“Baada ya kukamilisha zoezi la upimaji mashamba na urasimishaji wa kijiji chote cha Lupembelwasenga, hivi sasa mradi unaendelea na upimaji mashamba katika vijiji vya mradi ambavyo vipo wilayani Iringa” alisema Msigwa

Thursday 22 November 2018

MAAJABU YA SERIKALI YA QATAR KUELEKEA KOMBE LA DUNIA MWAKA 2022.....NCHINI HUMO



Tayari Serikali ya Qatar imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa viwanja na miundombinu kadhaa ikiwemo ya usafiri kama treni.

Michuano hiyo ikiwa imebadilishwa katakana na joto, itaanza November 21, 2022 hadi  Desemba 18 ikiwa ni jumla ya siku 28.

Viwanja vinane vya michuano hiyo vino ndani ya mail 21 za jiji kubwa la Doha na hii itawawezesha baadhi ya mashabiki kutazama mechi mbili kwa siku katika viwanja tofauti.











WAZIRI MKUU MSTAAFU EDWARD LOWASSA MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI WA ALBAMU YA MARIAM KILYENYI


 Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi, utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi ambaye atazindua albamu yake skiku ya tarehe 2 mwezi wa 12 mwaka huu
Na mwandishi wetu, Dar es Salaam. 

Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ya mwimbaji wa muziki wa Injili Mariam Kilyenyi, utakaofanyika Disemba 2, 2018 katika Kanisa la Kiinjili la Kirutheli Tanzania (KKKT)-Sinza Mapambano, jijini Dar es Salaam.

Mbali na Lowassa, waimbaji watakaosindikiza uzinduzi wa albamu hiyo inayoitwa ‘Hakimu wa Haki’ ni Bahati Bukuku, Dk Tumaini Msowoya, Tumaini Njole, Tumaini Mbembela,  Madamu Ruth ,Iren Mwamfupe, Bony Mwaitege, Margie Muliri, Juvenalista Mabuma  Edson Mwasabwite.

Akizungumza na Mwananchi, Mariam alisema amemualika Lowassa kwa sababu ndiyo aliyeanza kuibu kipaji chake, alipompa nafasi ya kuimba siku ya sherehe yake ya kuzaliwa.
“Lowassa ni baba yangu, aliibua kipaji change ndio maana nikatamani awe mgeni rasmi na amekubali, namshukuru sana Mungu kwa sababu hii,” alisema.

Alitaja nyimbo zilizo kwenye albamu yake kuwa ni Hakimu wa Haki, Pam Pam tukuza, Natafuta Mshauri, Chereko leo, Nasikia Kuitwa, Agano Langu, Ushindi Lazima na Mapambazuko.

“Nasikia kuitwa ndio wimbo ambao niliimba wakati nikianza mbele ya baba Lowassa, kwa hiyo ilipofika hatua ya kuandaa albamu yangu niliuweka na huo kwa sababu ndio ulionifungulia njia,” alisema.

Akizungumzia changamoto alizokutana nazo kwenye muziki huo, Mariam alisema ni gharama kubwa ya uandaaji wa muziki pamoja na kusambaza kazi hiyo.

“Naimba muziki kwa sababu nasikia kuitwa kwa ajili ya kazi hiyo, kusema kweli gharama za uandaaji wa kazi nzuri ni kubwa hata hivyo namshukuru Mungu kwa sababu nimeshakamilisha hatua ya kwanza,” alisisitiza.

Hata hivyo alisema, imekuwa rahisi kwake kufikia ndoto ya mafanikio kwa sababu ya sapoti kubwa kutoka kwa waimbaji waliotangulia.

Mariam amesema tayari tiem ya wacheza show ‘dancers’ imeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya siku hiyo.

“Mara nyingi waimbaji wa muziki wa injili huwa tunapuuzia wacheza shoe lakini ni watu muhimu na hawa ndio huwa wanafanya watu wafurahie matamasha, kwa hiyo tayari nimeshawaingiza kambini,” alisema.

Akizungumzia uzinduzi huo, mwimbaji Jesca Gazuko anayetamba na wimbo wa ‘Bwana Amefanya’ alisema ujio wa Lowassa unaonyesha namba ambavyo viongozi wamekuwa wakisapoti kazi za waimbaji wanaochipukia.

Monday 29 October 2018

WATANO WAFARIKI DUNIA KWENYE HELIKOPTA YA MMILIKI WA LEICESTER CITY


Watu  watano wamefariki dunia pamoja na mmiliki wa klabu ya Leicester City ya England, bilionea Vichai Srivaddhanaprabha baada ya helikopta waliyokuwa wamepanda kuteketea kwa moto.

Mmiliki wa Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha, mwenye umri wa miaka 60, ambaye aliinunua klabu hiyo kwa Pauni Milioni 39 mwaka 2010 na kuiwezesha kutwaa taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England mwaka 2016 atakumbukwa kama mtu wa kipekee na muungwana.

Mlimbwende, Nursara Suknamai, Msaidizi wake, Kaveporn Punpare na rubani, Eric Swaffer, ambaye hapo kabla alisafirisha familia ya kifalme, na mpenzi wake na rubani mwenzake wake, Izabela Roza Lechowicz wote wamefariki kwenye ajali hiyo.





















KAGERE, OKWI, KAPOMBE WE ACHA TUU, WAMPAPASA MASAU BWIRE......TAIFA


Baada ya ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Ruvu Shooting uliochezwa jana  Uwanja wa Taifa,  umeonekana kuwachanganya viongozi wa Simba kwa furaha, Ofisa  habari wa Simba, Haji Manara amehoji ni nani mwingine anayekuja ili aweze kushushiwa mvua ya mabao.

Manara alisema kuwa kwa mwendo huu wa Simba kuna timu itapigwa mabao mengi zaidi ya hayo matano kutokana na aina ya wachezaji waliopo Simba, mbinu za  Kocha, Patrick Auusems kueleweka.

"Simba ni klabu kubwa lazima uiheshimu, nilikwambia ntakujibu baada ya dk 90, umepapapaswa halafu square unashtka, hii ndio Simba tunang'ata, nani mwingine anakuja ? kwa mwendo huu kuna mtu atapigwa nyingi sana zaidi ya bao 5," alisema.

Simba imefanikiwa kuendeleza rekodi yake ya kufunga mabao mengi kwenye ligi ndani ya mechi moja, kwani kwa mechi zote tano ambazo zilichezwa jana timu nyingi zilishinda kwa idadi ya bao 1 huku Simba ikishinda kwa mabao 5-0..

JAMII YA WABARBAIGI WAPATA HATI MILIKI ZA KIMILA ZINAZOWASAIDIA KUPATA MAKAZI YA KUDUM

Diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa utoaji wa hati hizo katika kijiji cha Kitisi ambapo jamii ya wabarbaigi wanaishi maeneo hayo nao walipewa hati miliki za kimira na kuanza kukomesha hama hama ya kabili hilo la wafugaji
Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future
 JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wakiwa kwenye picha na viongozi mara baada ya kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

JAMII ya Wabarbaigi wanaoishi katika kijiji cha Kitisi kata ya Idodi wilaya ya Iringa wameanza kuondokana na mfumo dume baada ya kukubali wanawake kupatiwa hati miliki za kimila za maeneo ambayo wanamiliki mara baada ya kupata elimu kutoka mradi wa LTA wa feed the future unaotekelezwa katika wilaya za mkoa wa Iringa na Mbeya.

Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa hati za kimira wanawake wa kibarbaigi walisema kuwa awali walikuwa hawaruhusiwi kumiliki mali yoyote ile bali mali zote zilikuwa zinamilikiwa na wanaume.

“Kwenye kabila letu mila zinawapa sana nafasi wanaume kumiliki mali na vitu vingine na kumfanya wanamke kuwa tegemezi jambo ambalo miaka ya nyuma limerudisha maendeleo nyuma ya wanawake” walisema wanawake hao wa Kibarbaigi

Wanawake hao walisema kuwa baada ya kupata elimu ya upimaji wa ardhi na kuifanya ardhi kuwa na hati miliki imesaidia wanaume wa kabila hilo kuanza kuitambua nafasi ya mwanamke na kumuwezesha mwanamke naye kumiliki mali sawa na wanaume wa kabila la wabarbaigi.

Tunaishukuru serikali na mradi wa LTA kwa elimu waliyoitoa kwa wanaume wa kabila la Barbaigi kwa kukubali wanawake wamiliki ardhi kwa kupewa hati miliki za kimira bila elimu hiyo wanawake sisi tungeendelea kuwa wakina mama wa nyumbani tu.

Naye mwenyekiti wa kabila hilo la wafugaji Shabani Ntasham alisema kuwa kupatikana kwa hati miliki za kimira kumekomesha hamahama ya jamii hiyo pamoja na kumuwezesha mwanamke wa jamii hiyo kumiliki ardhi.

“Sisi kabila letu ni watu wa kuhama hama hivyo baada ya kupata hati miliki za kimira sasa hatuwezi kuhama tena kwa kuwa tunamiki ardhi kisheria zinazotuwezesha kuboresha makazi yetu na kutufanya tuishi na kufanya shughuli zetu sehemu moja” alisema Ntasham

Ntasham alisema Mradi wa LTA wa feed the future unaofadhiwa na USD umetoa elimu kwa kabila la barbaigi na kusaidia kuanza kuondokana kwa kiasi chake mfumo dume kwa kuwawezesha wanaume wa kabila hilo kuwagawaia wanawake ardhi na kuzikatia hati miliki za kimila.

“Saizi umeona wanawake na wanaume wanafuraha kwa pamoja kwa kuwa kila mmoja anamiliki ardhi yake ambayo inamuwezesha kufanya jambo analolitaka kwa wakati wake tofauti kama ilivyokuwa hapo zamani” alisema Ntasham

Akizungumza na wanakijiji hao baada ya kukabidhi hati hizo diwani wa kata ya Idodi Onesmo Mtatifikolo alisema kuwa hati hizo zitawasaidia kutenga maeneo kwa ajili ya matumizi mbalimbali kwa kuzingatia uwezo wa ardhi kuhimili idadi hiyo na kasi ya ongezeko la watu na mifugo kwa miaka mingi ijayo.

Mtatifikolo aliongezea kuwa,hatua hiyo itasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuimarisha usalama wa miliki za ardhi na kuongeza thamani ambayo itawawezesha hata kukopesheka katika taasisi za kifedha zikiwemo benki.

“Usajili wa ardhi ni muhimu kwasababu unaongeza ulinzi wa umiliki wa ardhi, unawezesha uwekezaji, unaongeza thamani ya ardhi na unapunguza migogoro ya ardhi,” alisema Mtatifikolo

Aidha Mtatifikolo aliwaomba Feed The Future wautanue mradi huo angalau ufike umalize kupima vijiji vyote vya kata hiyo  huku akivikumbusha vijiji vyote vya kata hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwenye miradi ambayo inasaidia kukuza maendeleo ya nchi. 

“Tunataka katika kipindi ambacho Mradi wa Urasimishaji Ardhi (LTA) unaofanywa chini ya mpango wa Feed The Future kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) tuhakikishe tunapima ardhi na mipango ya matumizi bora na ipimwe ili kila mwenye kipande chake cha ardhi awe na hati yake,” alisema Mtatifikolo.

Mtatifikolo aliwataka wanakijiji wa kijiji hicho ambao hawajapimiwa maeneo yao kwa sababu mbalimbali ikiwemo ubishi na migogoro ya kifamilia kutumia vizuri muda ambao bado mradi huo upo katika wilaya hiyo na kuhakikisha nao wananufaika na zoezi hilo.

Awali naibu mkurugenzi wa Mradi wa LTA, Malaki Msigwa aliwapongeza wataalamu wa mradi huo kwa kuhakikisha wanawasaidia wananchi wa kijiji cha Kitisi kupima maeneo yao na kupata hati miliki za kimila ambazo zitakuwa msaada mkubwa kwenye maendeleo ya kiuchumi.

“Baadhi ya miradi imeibuliwa wakati wa upimaji wa ardhi hivyo ni fursa sasa kwa wananchi wenyewe kuitumia vizuri ardhi waliyopimiwa na kupewa hati miliki za kimila na kwa kuwa asilimia fulani kijiji hiki kimepimwa hivyo wanaweza kuwa kijiji cha mfano kwa kuwapa maendeleo hata wawekezaji wazuri kwa faida yao” alisema Msigwa

Friday 12 October 2018

DKT TIZEBA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI HATI YA MARIDHIANO UKOPESHAJI WA MATREKTA


Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018. 


Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB), Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Ndg Marco Mtunga na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Prof Damian Gabagambi wakionyesha hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.


Naibu Waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi katika Ukumbi mdogo wa Mikutano Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro leo tarehe 11 Octoba 2018.

Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba leo tarehe 11 Octoba 2018 ameshuhudia utiaji saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta kwa vyama vya ushirika vya msingi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika Ukumbi mdogo wa Mikutano katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA) Mjini Morogoro Waziri Tizeba amesisitiza matrekta hayo kutumika ipasavyo kwenye sekta ya kilimo ili kuongeza tija kwenye uzalishaji wa kilimo nchini jambo litakalokuwa na manufaa kwa mwananchi mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Taasisi ambazo zimeshirikiana kufanikisha utiaji saini huo ni Bodi ya Pamba ambayo ipo chini ya wizara ya kilimo, Benki ya Maendeleo ya kilimo-TADB, Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Tume ya Maendeleo ya ushirika.

Dkt Tizeba alisema kuwa Vyama vya ushirika vya msingi vinapaswa kuongeza juhudi katika kilimo ili kuakisi kulipa gharama za mkopo ambao ni asilimia 20 ya mkopo wote katika kipindi cha miaka mitatu huku asilimia zingine 80 zikilipwa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo-TADB.

Utiaji huo wa saini hati ya makabidhiano ya ukopeshaji wa matrekta 300 kwa vyama vya msingi vya ushirika unajili wakati ambapo hivi karibuni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa alimkabidhi Waziri wa kilimo Dkt Charles Tizeba jumla ya matrekta 500 ya Ursus kwa ajili ya kukopeshwa kwenye  vyama vya ushirika vya msingi ili wakulima kunufaika na tija katika kilimo hususani zao la Pamba.

Akizungumza mara baada ya kushuhudia utiaji saini Dkt Tizeba alisema kuwa sekta ya kilimo nchini bado inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo tija ndogo inayosababishwa na matumizi madogo ya pembejeo, huduma duni za ugani na matumizi ya zana duni za kilimo ambapo wakulima wengi wanatumia majembe ya mkono au kutumia maksai wakati wa kulima.

“Katika kilimo cha Pamba msimu wa mwaka 2017/2018 ushahidi unaonyesha wakulima walichelewa kuanza kuandaa mashamba kwa sababu Maksai wakati wa kiangazi wanadhoofu sana,” Alikaririwa Dkt Tizeba na kuongeza kuwa

“Mara mvua inaponyesha hawawezi kulima mpaka majani yawe mengi ndio wapate nguvu za kuanza kulima, hali hii inaondoa uwezekano wa wakulima kutumia teknolojia mpya katika kilimo kama vile kilimo hifadhi ambacho kimedhihirika kuongeza tija zaidi ya mara mbili” 

Tizeba alisema mtazamo wa mpango huo ni kuunganisha nguvu za mkulima mmoja mmoja ili kuharakisha kuleta maendeleo yao ambapo utatekelezwa kwa kutumia sehemu ya fedha zinazolipwa AMCOS kama kamisheni ya kusimamia ununuzi wa pamba ambapo matarajio ni kukusanya Bilioni 6 kama uzalishaji wa pamba utafika kilo milioni 400 kwa mwaka.

Alisisitiza kuwa Bodi ya Pamba pamoja na Tume ya Maendeleo ya ushirika zinapaswa kufuatilia kwa karibu hatua zote mwenendo wa ufanyaji kazi wa matrekta hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa punde yanapoanza kufanya kazi yawe yanafanyiwa marekebisho ya mara kwa mara.


 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube