BREAKING

Friday 2 October 2015

MAMA SAMIA MWIBARA NA SERENGETI JANA

  Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimsalimia Mgombea Ubunge Jimbo la Mwibara, Kangi Ligora, alipowasili kufanya mkutano wa kampeni kwenye viwanja vya mnadani, katika jimbo hilo, jana, Oktoba 1, 2015. Katikati ni Mkuu wa wilaya ya Bunda mkoani Mara, Joshua Mirume

 Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimia wananchi alipowasili katika viwanja vya Mnadani wa Kisorya, kuhutubia mkutano wa kampeni katika jimbo la Mwibara, wilaya ya Bunda mkoani Mara, jana, Oktoba 1, 2015

 Wananchi wakiwa wamefurika karika viwanja vya Mnadani, eneo la Kisorya katika jimbo la Mwibara mkoani Mara, wakati Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alipohutubia mkutano wa kampeni katika eneo hilo jana, Oktoba 1, 2015

  Mgomea Ubunge jimbo la Bunda Vijijini mkoani Mara, Boniface Mwita Getere akiomba kura, wakati msafara wa mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto), uiposimamishwa na wananchi katika eneo la Mugeta, katika jimbo hilo, jana, Oktoba 1, 2015
 Mwananchi mwenye ulemavu, akimshangilia mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan, aliposimama kwa muda kusalimia wananchi katika eneo la Mugeta, jimbo la Bunda Vijijini mkoani Mara, jana, Oktoba 1, 2015.


 Wananchi wakimsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan katika mkutano wa kampeni uliofanyika Mugumu, jimbo la Serengeti mkoani Mara, jana Oktoba 1, 2015
 Mgombea Ubunge jimbo Dk. Kebwe Stephen Kebwe, Serengeti mkoani Mara, akiomba kura katika mkutano wa kampeni wa Mama Samia uliofanyika katika jimbo hilo, jana, Oktoba 1, 2015. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, Christopher Sanya

  Mgombea Ubunge jimbo la Mwibara, Kangi Ligora, akionyesha machejo ya furaha, baada ya kuomba kura wananchi katika mkutano wa kampeni wa Mama Samia, uliofanyika jana, Oktoba 1, 2015, katika viwanja vya Mnadani, Kisorya katika jimbo hilo mkoani Mara

Wananchi wakiwa na bango wakati wa mkutano wa kampeni za CCM wa Mama Samia, uliofanyika ja, Oktoba 1, 2015, katika Viwanja vya Mugumu, Serengeti mkoani Mara

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube