Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kulia) akikata keki katika moja ya tawi la ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam kuzinduwa wiki ya huduma kwa wateja leo. Kampuni ya simu ya TTCL leo imezinduwa wiki ya huduma kwa wateja ambapo inaanzia Oktoba 12 hadi 16, 2015. |
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dk. Kamugisha Kazaura (kushoto) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya uzinduzi wa wiki ya huduma kwa wateja leo jijini Dar es Salaam. |
Hapa ni wakati wa kugonganisha glasi za mvinyo kutakiana afya njema na utendaji bora...! |
Akizungumza na baadhi ya wateja wa TTCL, maofisa na wafanyakazi jijini Dar es Salaam Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja TTCL, Laibu Leonard alisema ndani ya maadhimisho hayo maofisa wa TTCL watapita kuwatembelea wateja ofisini na majumbani kuwasikiliza maoni yao ikiwa ni pamoja na kupata mrejesho juu ya huduma wanazozitoa. Alisema maofisa waandamizi wa kampuni hiyo watashiriki moja kwa moja katika zoezi hilo la kutoa huduma pamoja na kuwatembelea wateja kupata maoni yao na pia kutoa shukrani kwa wao kukubali kuhudumiwa na kampuni hiyo ya simu ya kizalendo nchini Tanzania. "...Mbali na kutoa huduma zetu katika matawi mbalimbali katika kipindi hiki maofisa waandamizi wa TTCL watawatembelea wateja moja kwa moja katika ofisi zao au majumbani kwa ajili ya kuwasikiliza na pia kupokea naoni yao," alisema Leonard akizungumza katika hafla hiyo. Katika uzinduzi wa hafla hiyo TTCL ilitoa zawadi kwa wateja watano wa mwanzo waliofika katika vituo vya huduma kwa wateja leo asubuhi kuhudumiwa na kampuni hiyo pamoja na kuwazawadia maofisa wa TTCL waliofanya vizuri zaidi katika idara ya huduma kwa wateja ya kampuni hiyo, ikiwa ni motisha ya kuchochea utendaji bora zaidi.
No comments:
Post a Comment