BREAKING

Saturday, 19 December 2020

JUMLA YA VIJANA 2000 KUTOKA MKOA WA IRINGA KUFIKIWA NA MRADI WA LYRA IN AFRCA

 

Msimamizi wa mradi imarika kijana wa LYRA IN AFRICA Gift Mafue akitoa elimu kwa baadhi ya vijana waliopo kwenye mradi huo
Msimamizi wa maradi imarika kijana wa LYRA IN AFRICA Gift Mafue akitoa elimu kwa baadhi ya vijana waliopo kwenye mradi huo
Baadhi ya vijana washiriki wa mafunzo yanayotolewa na
maradi imarika kijana wa LYRA IN AFRICA.

 

 Na Fredy Mgunda,Iringa

JUMLA ya vijana 2000 kutoka kwenye wilaya tatu za mkoa wa Iringa kufikiwa na mradi wa imarika kijana wa LYRA IN AFRCA  wenye lengo la kufungua fikra na mitazamo chanya kwa vijana katika Maisha yao.

 

Akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa baadhi ya vijana ambao wapo kwenye mradi huo, msimamizi wa mradi imarika kijana wa LYRA IN AFRICA Gift Mafue alisema kuwa lengo la mradi huo ni kuwawezesha vijana kutambua fursa zilizopo na kuzifanyika kazi kwa kupata matokeo chanya.

Alisema kuwa mradi huo unafadhiliwa na watu wa uingereza kwa kuwezesha kutoa mafunzo mbalimbali kwa vijana ambao watakuwa wanatoa elimu kwa vijana na watu wengine kutoka kwenye jamiii ambayo wanaishi huko vijijini kwao.

Mafue alisema kuwa wameshafanikiwa kufanya mafunzo kwa vijana wa vijiji kumi na moja kutoka katika wilaya ya Iringa na Kilolo ambopo hadi sasa takribani vijana 401 wameshafikiwa katika awamu ya kwanza wakitegemea kuanza awamu ya pili mwaka 2021 mwezi wa pili kwa lengo la kufikia vijana wote waliolengwa na mradi.

Alisema kuwa lengo kuu mradi huo ni kuwawezesha vijana kuzitambua fursa zilizopo katika maeneo wanaishi na kuzigeuza kuwa fursa kiuchumi na kukuza maendeleo na kusaidia vijana wasikimbilie mijini na kuzitelekeza fursa zilizopo vijijini.

Mafue alisema kuwa mradi huo unahusisha vijana wenye umri wa miaka kumi na tano hadi ishirini na nane ikiwajumisha vijana walemavu na mzazi mmoja ambao hawana fursa yoyote na kuwasaidia kisaikolojia kuanza kuzichangamkia furs ana kujikombo kimaisha.

“Tunawasaidia pia mzazi mmoja ambaye alipata mimba akiwa shuleni au akiwa na umri mdogo kuzitambua furs ana kuzitumia ili kujikomboa kiuchumi na matumaini kwa vijana wanaoishi vijijini yameongezeka kwa vijana hao kuanza kufanya biashara za kiuchumi” alisema Mafue

 

Alisema kuwa mafunzo ya imarika vijana yamesaidia uundwaji wa vikundi vya kiuchumi ambapo hadi sasa jumla ya vikundi 21 tayari vimeundwa na vinafanya vizuri katika kukopa na kukopesha kwa lengo la kuinua kiuchumi.

Shuhudia Chang’a anatokea Kijiji cha Imalutwa alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na faida ya kusaidia kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine ya kiuchumi tofauti na ilivyokuwa hapo awali kabla ya kupata mafunzo kutoka LYRA IN AFRICA.

Naye Yasinta Migodela alisema kuwa mafunzo hayo yamemsaidia kuboresha ufanisi wa kibiasha kwa kuwa hapo awali alikuwa anafanya biasha bila ya kuwa na mafunzo na kumpelekea kupata hasara lakini baada ya kupata mafunzo yamsaidia jinsi ya utunzaji wa fedha na mpangilio mzima wa biashara.

Kwa upande wao Stanslaus Mtweve,Nestory Simagunga,Cassian Kihongosi na Rebeka Mbwilo walisema kuwa mafunzo waliyopata kutoka katika shirika la LYRA IN AFRICA yamewasidia kuwakomboa kiuchumi na kifikra kutokana na elimu waliyopewa.

 

“Mara baada ya kupewa mafunzo hayo na shirika la LYRA IN AFRCA yalitusaidia kuridi katika vijiji vyetu na kuendelea kutoa elimu kwa jamii yetu ambao kwa asilimia furani tumesaidia vijana wengi kuacha tabia ya ulevi na matumizi ya madawa ya kulevya na wameanza kujikita katika shughuli za kiuchumi ambazo kwa sasa zinachochea uchumi kukua” walisema

 

 

 

MADIWANI HALMASHAURI MJI MAFINGA WAAHIDI NEEMA YA MAENDELEO KWA WANANCHI WAO

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mafinga Reginant Kivinge akiongea madiwani,watendaji na wananchi waliohudhuria ufunguzi wa baraza hilo.

Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini na mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve wakiwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo la madiwani



MADIWANI wa Halmashauri ya mji wa Mafinga mkoani Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kureta maendeleo kwa wananchi waliwachagua na kuwapa dhamana ya kuwepo madarakani mara baada ya uchaguzi mkuu

Akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza jipya la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mafinga,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Reginant Kivinge alisema kuwa wananchi wanamatumaini makubwa ya kimaendeleo kutoka kwa madiwani hao hivyo wanapaswa kwenda kuchapa kazi kwa nguvu zao zote.

Kivinge alimuomba mkurugenzi wa halmashauri hiyo Saada Mwaruka  pamoja na watendaji wote kuhakikisha wanashirikiana kwa ukaribu ili kuhakikisha wanatatua na kumaliza kero zote zinazowakabili wananchi.

 

Alisema kuwa halmashauri hiyo bado inakabiriwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikikwamisha juhudi za kureta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa umoja wao ili kuleta maendeleo kwa wananchi yanayotarajiwa.

  "Natambua uchaguzi huu ulioisha tulipitia mambo mengi sana,lakini sasa uchaguzi umekwisha  ni mwendo wa kuchapa kazi sasa twende kuchapa kazi ili turudishe ile heshima muliyopewa na wananchi wetu kwa kutuchagua " alisema

 

 

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa (CCM) wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa Daudi Yasini amewataka madiwani wa halimashauri ya Mji Mafinga kwenda kushungulika na kutatua kero za wananchi kwani chama hicho hakitasita kumchukulia hatua diwani yoyote asiyetimiza majukumu yake ipasavyo .

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kikao cha kwanza cha madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kula kiapo cha utii wa kuwatumikia wananchi kwa kufuata kanuni za maadili ya utumishi wa umma

Daudi alisema kuwa wananchi wamekuwa na imani kubwa na chama cha mapinduzi hivyo hivyo wanapaswa kuheshimu na kuthamini nafasi waliyopewa kwa kufanya kazi kwa weredi na ushirikiano kuhakikisha wanatatua kero za wananchi wa halamshauri hiyo.

"Tumekuwa na uchaguzi nyingi ila uchaguzi wa mwaka huu tumeweka historia kwa wilaya ya Mufindi kwa baraza letu lote ni CCM na hii ni kwa sababu ya kazi kubwa iliyofanywa na mh Rais Magufuli hivyo naamini hamtatuangusha mkatumikie nafasi muliyopewa kwa weredi uliotukuka" 

 

Daudi alitoa onyo kali kwa madiwani wote wanaodhani wamepewa nafasi hiyo kwa ajili ya kujinufaisha wao au kujipatia mali katika Halmashauri hiyo,chama cha mapinduzi kitapita kata kwa kata kuhakikisha kuwa viongozi waliochaguliwa wanatatua kero za wananchi la sivyo hatua kali zitachukuliwa kwa Diwani husika.

“Niwaonye wale wote ambao mnadhani mmepata nafasi ya kwenda kupiga dili halimashauri hapa ni kazi tu na endapo tutakuja kwenye kata yako na kukuta wananchi wanalalamika kero nyingi hazitatatuliwa basi hawatasita kuwachukulia hatua” alisema Daudi

Hata hivyo Daudi alimtaka mkurugenzi pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kushirikiana vyema na madiwani hao ili kutatua kero za wananchi zinazowakabili na sio kupishana kwenye maamuzi ya vikao ambavyo lengo ni kupunguza mzigo wa kero kwa wananchi

Naye katibu wa CCM wilaya ya Mufindi James Mgego aliwashukuru madiwani hao kwa uvumilivu na ushindi waliopata kwenye uchaguzi uliopita kwani walipita kwenye viunzi na vikwanzo Vingi mpaka kufika hapo walipo

Mgego alisema kuwa wananchi wamemaliza kazi yao na wajibu wao hivyo sasa ni wakati wa madiwani hao kurudisha dhamana na heshima waliyopewa kwa kwenda kuwatumikia na kutatua kero za wananchi

Alisema chama hicho kinatambua dhamana kubwa waliyopewa na wananchi hao kwa kuonyesha imani kwa chama hicho hivyo wanadeni kubwa la kurudisha maendeleo ya kweli kwa watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama kwani uchaguzi umekwisha na sasa ni muda wa kuchapa kazi

Lakini pia Mbunge wa jimbo la Mafinga Cosato Chumi alissema kuwa anataka kupeleka mapendekezo bungeni ili kuweza kupata kibali na kubadili sheria ili kufanya biashara kwa mji wa Mafinga masaa 24 kwani wilaya hiyo inapitiwa na barabara kuu hivyo itakuwa ni fursa ya kukuza uchumi kwa wakazi wa Mafinga na kuongeza pato la halimashauri hiyo endapo watu watafanya biashara masaa 24 

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Saada Mwaruka alisema kuwa watendaji wote wa halmashauri hiyo wapo tayari kujitolea na kuonyesha ushirikiano kwa madiwani wote ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi na kuleta maendeleo katika Jimbo la Mafinga Mjini.

 

 

Wednesday, 17 June 2020

BABA WA SAMATTA ANENA JAMBO....WAKATI SAMATTA AKIWA UWANJANI LEO EPL

MSHAMBULIAJI wa timu ya Aston Villa inayoshiriki Premier League, Mtanzania, Mbwana Samatta amemhakikishia baba yake mzazi, mzee Ally Samatta kuwa atapambana kuhakikisha anainusuru timu yake isishuke daraja msimu huu.

Samatta ambaye amejiunga na timu hiyo katika usajili wa dirisha dogo msimu huu kwa mkataba wa miaka minne na nusu, ana kazi kubwa ya kuibakisha timu hiyo kutokana na kuwa kwenye nafasi mbaya ya 19 ikiwa na pointi 25 ikifuatiwa na Norwich City ambayo inaburuza mkia ikiwa na pointi 21.

Mzee Samatta alisema kuwa, kutokana na ligi kutarajiwa kurejea tena leo Juni 17, 2020, mtoto wake amemwambia atapambana kuinusuru timu hiyo kushuka daraja.

“Suala la ligi kurejea lipo wazi na kila mmoja amekuwa akilijua vizuri isipokuwa kijana amenieleza nia yake ni kutaka kuinusuru timu isishuke hivyo amepanga kucheza kwa kujituma zaidi ili kufikia malengo.

“Unajua wapo ambao walitaka ligi ifutwe kama zilizofanya nchi nyingine lakini England wao wameona ni bora kumalizia hivyo kila mmoja anatakiwa apambane na yeye ndiye amenieleza kwamba hatamani kuona wakishuka hivyo lazima ajitoe ili kuinusuru timu na msimu ujao waanze pamoja,” alisema mzee Samatta.

WADAU WATAKIWA KUENDELEA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA KUINUA MICHEZO







WADAU WAMETAKIWA KUENDELEA KUJITOKEZA KWA WINGI KATIKA KUINUA MICHEZO  KUWEKA UDHAMINI KWENYE TIMU ZA MTAANI ILI KUIBUA VIPAJI AMBAVYO VITAKUA NA MANUFAA KWA TAIFA 
Kuali hiyo imetolewa katika Mchezo wa Kusisimua uliozikutanisha  timu mbili kati ya Soccer City ya Mabwepande ya Mtaa wa Mji Mpya  dhidi ya timu ya New Kibamba FC Mchezo ambao umedhaminiwa na kampuni ya Msukuma One inayodhalisha na kusambaza Nafaka huku lengo ikiwa kuunga Mkono Serikali ya awamu ya tank kuunga mkono juhudi za kuinua sekta ya Michezo.

Mkurugenzi Mkuu wa Msukuma One Aman Manengero amesema kuwa wataendelea kusaidia jitihada hizo ili kuleta meandeleo zaidi.
Ktika mchezo huo mkali ilishuhudiwa timu ya kibamba FC kukubali kipigo baada ya kuzidiwa kwa mikwaju ya penati dhidi ya timu ya soka city baada ya timu hizo kutoka sare ya 

goli mbili kwa mbili ndani ya dakika tisini huku timu ya soka city ikiibuka na zawadi ya jezi iliyotolewa na mdau huyo.






Tuesday, 2 June 2020

NDEGE YA MIZIGO KUIMARISHA USAFIRISHAJI SAMAKI NJE NCHI HIYOOO KUTUA


 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe amesema mipango ya Serikali kununua ndege ya mizigo utaimarisha usafirishaji wa minofu ya samaki moja kwa moja kwenda nje ya nchi kutokea uwanja wa ndege wa Mwanza.

Waziri Kamwelwe ameyasema hayo Jumatatu Juni Mosi 2020 jijini Mwanza wakati akifungua mkutano wa kupokea mikakati ya pamoja kuondoa vikwazo na kufanikisha biashara ya usafirishaji minofu ya samaki kwenda nje ya nchi hususani mataifa ya Ulaya ambako kumekuwa na soko la uhakika.

Kikao hicho kimewajumuisha pia Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Wizara za Mifugo na Uvuvi, Viwanda na Biashara pamoja na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katika) akizungumza kwenye kikao hicho. Kushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na kulia ni Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella.


Friday, 22 May 2020

LAMPARD HANA NENO NA KANTE,KUJITENGA KUTAZAMA AFYA YAKE






Kocha Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard amesema kuwa uamuzi wa kiungo wake N'Golo Kante kujitenga na wenzake ni mzuri kwa manufaa yake na afya za wengine pia.

Kante aliripoti mazoezini siku ya Jumanne katika kituo cha Cobham HQ ila alishindwa kurejea siku ya Jumatano kutokana na kutojihisi vizuri.

Kwa sasa timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu England zimeanza maandalizi ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kumalizia mechi zilizobaki baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona .

Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa ya Kante kushindwa kuendelea kuripoti mazoezini ni hofu ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo bado vinasambaa kwa kasi.

RAIS MAGUFULI ARUHUSU MICHEZO NA VYUO JUNI MOSI....


Rais wa Tanzania, John Magufuli ametangaza kuwa vyuo vikuu nchini humo vitafungufuliwa Juni Mosi, na kuruhusu pia shughuli zote za michezo nazo ziendelee kama kawaida.
Rais Magufuli amesema vyuo vikuu vyote sasa vitarejea katika hali yake ya kawaida kuendelea na masomo kuanzia Juni Mosi baada ya kijiridhisha kutokana na maendeleo ya hali ya maambukizi ya virusi vya corona.
Amesema maambukizi nchini humu yameshuka kwa kiwango cha kuridhisha hatua ambayo imemfanya aanze kufungua baadhi ya shughuli zilizokuwa zimesimama kutokana na janga hilo la virusi vya corona lilipopiga hodi kwa mara ya kwanza nchini Machi 16.
"Ikiwa mwelekeo nnaouona utandelea katika wiki zijazo, napanga kufungua vyuo vikuu ili wanfunzi waendelee na masomo yao, alisema Magufuli wakati akizungumza kwenye ibada ya misa kaskazini-magharibi mwa nchi wiki iliyopita.
Hatua nyingine ambazo Rais Magufuli amezitangata wakati alipokuwa akiwaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni ni kuwaruhusu wanafunzi wa kidato cha sita wanaojiandaa na mitihani ya kuhitimu masomo yao kurejea shuleni.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube