Kocha Mkuu wa Chelsea, Frank Lampard amesema kuwa uamuzi wa kiungo wake N'Golo Kante kujitenga na wenzake ni mzuri kwa manufaa yake na afya za wengine pia.
Kante aliripoti mazoezini siku ya Jumanne katika kituo cha Cobham HQ ila alishindwa kurejea siku ya Jumatano kutokana na kutojihisi vizuri.
Kwa sasa timu nyingi zinazoshiriki Ligi Kuu England zimeanza maandalizi ya kufanya mazoezi ya pamoja kwa ajili ya kumalizia mechi zilizobaki baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona .
Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa ya Kante kushindwa kuendelea kuripoti mazoezini ni hofu ya kupata maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo bado vinasambaa kwa kasi.
No comments:
Post a Comment