BREAKING

Saturday, 19 December 2020

MADIWANI HALMASHAURI MJI MAFINGA WAAHIDI NEEMA YA MAENDELEO KWA WANANCHI WAO

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Mafinga Reginant Kivinge akiongea madiwani,watendaji na wananchi waliohudhuria ufunguzi wa baraza hilo.

Mbunge wa jimbo la Mafinga Mjini na mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve wakiwa kwenye uzinduzi wa baraza hilo la madiwani



MADIWANI wa Halmashauri ya mji wa Mafinga mkoani Iringa wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa ili kureta maendeleo kwa wananchi waliwachagua na kuwapa dhamana ya kuwepo madarakani mara baada ya uchaguzi mkuu

Akizungumza mara baada ya kuzinduliwa kwa baraza jipya la madiwani wa Halmashauri ya mji wa Mafinga,mwenyekiti wa halmashauri hiyo Reginant Kivinge alisema kuwa wananchi wanamatumaini makubwa ya kimaendeleo kutoka kwa madiwani hao hivyo wanapaswa kwenda kuchapa kazi kwa nguvu zao zote.

Kivinge alimuomba mkurugenzi wa halmashauri hiyo Saada Mwaruka  pamoja na watendaji wote kuhakikisha wanashirikiana kwa ukaribu ili kuhakikisha wanatatua na kumaliza kero zote zinazowakabili wananchi.

 

Alisema kuwa halmashauri hiyo bado inakabiriwa na changamoto nyingi ambazo zimekuwa zikikwamisha juhudi za kureta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini hivyo wanapaswa kufanya kazi kwa umoja wao ili kuleta maendeleo kwa wananchi yanayotarajiwa.

  "Natambua uchaguzi huu ulioisha tulipitia mambo mengi sana,lakini sasa uchaguzi umekwisha  ni mwendo wa kuchapa kazi sasa twende kuchapa kazi ili turudishe ile heshima muliyopewa na wananchi wetu kwa kutuchagua " alisema

 

 

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wa (CCM) wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa Daudi Yasini amewataka madiwani wa halimashauri ya Mji Mafinga kwenda kushungulika na kutatua kero za wananchi kwani chama hicho hakitasita kumchukulia hatua diwani yoyote asiyetimiza majukumu yake ipasavyo .

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kikao cha kwanza cha madiwani wa halmashauri hiyo baada ya kula kiapo cha utii wa kuwatumikia wananchi kwa kufuata kanuni za maadili ya utumishi wa umma

Daudi alisema kuwa wananchi wamekuwa na imani kubwa na chama cha mapinduzi hivyo hivyo wanapaswa kuheshimu na kuthamini nafasi waliyopewa kwa kufanya kazi kwa weredi na ushirikiano kuhakikisha wanatatua kero za wananchi wa halamshauri hiyo.

"Tumekuwa na uchaguzi nyingi ila uchaguzi wa mwaka huu tumeweka historia kwa wilaya ya Mufindi kwa baraza letu lote ni CCM na hii ni kwa sababu ya kazi kubwa iliyofanywa na mh Rais Magufuli hivyo naamini hamtatuangusha mkatumikie nafasi muliyopewa kwa weredi uliotukuka" 

 

Daudi alitoa onyo kali kwa madiwani wote wanaodhani wamepewa nafasi hiyo kwa ajili ya kujinufaisha wao au kujipatia mali katika Halmashauri hiyo,chama cha mapinduzi kitapita kata kwa kata kuhakikisha kuwa viongozi waliochaguliwa wanatatua kero za wananchi la sivyo hatua kali zitachukuliwa kwa Diwani husika.

“Niwaonye wale wote ambao mnadhani mmepata nafasi ya kwenda kupiga dili halimashauri hapa ni kazi tu na endapo tutakuja kwenye kata yako na kukuta wananchi wanalalamika kero nyingi hazitatatuliwa basi hawatasita kuwachukulia hatua” alisema Daudi

Hata hivyo Daudi alimtaka mkurugenzi pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kushirikiana vyema na madiwani hao ili kutatua kero za wananchi zinazowakabili na sio kupishana kwenye maamuzi ya vikao ambavyo lengo ni kupunguza mzigo wa kero kwa wananchi

Naye katibu wa CCM wilaya ya Mufindi James Mgego aliwashukuru madiwani hao kwa uvumilivu na ushindi waliopata kwenye uchaguzi uliopita kwani walipita kwenye viunzi na vikwanzo Vingi mpaka kufika hapo walipo

Mgego alisema kuwa wananchi wamemaliza kazi yao na wajibu wao hivyo sasa ni wakati wa madiwani hao kurudisha dhamana na heshima waliyopewa kwa kwenda kuwatumikia na kutatua kero za wananchi

Alisema chama hicho kinatambua dhamana kubwa waliyopewa na wananchi hao kwa kuonyesha imani kwa chama hicho hivyo wanadeni kubwa la kurudisha maendeleo ya kweli kwa watanzania wote bila kujali itikadi ya vyama kwani uchaguzi umekwisha na sasa ni muda wa kuchapa kazi

Lakini pia Mbunge wa jimbo la Mafinga Cosato Chumi alissema kuwa anataka kupeleka mapendekezo bungeni ili kuweza kupata kibali na kubadili sheria ili kufanya biashara kwa mji wa Mafinga masaa 24 kwani wilaya hiyo inapitiwa na barabara kuu hivyo itakuwa ni fursa ya kukuza uchumi kwa wakazi wa Mafinga na kuongeza pato la halimashauri hiyo endapo watu watafanya biashara masaa 24 

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Saada Mwaruka alisema kuwa watendaji wote wa halmashauri hiyo wapo tayari kujitolea na kuonyesha ushirikiano kwa madiwani wote ili kuhakikisha wanatatua kero za wananchi na kuleta maendeleo katika Jimbo la Mafinga Mjini.

 

 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube