Tuesday, 20 August 2019
WANANCHI WA KIJIJI CHA WAMI NA MBUNGE MGIMWA WAIKATAA BARABARA INAYOTENGENEZWA NA KAMPUNI YA FABEC CIVIL AND TELECOM ENGINEERS

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiungana na wananchi kuikataa barabara ambayo inatengenezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe)

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini wakimsikiliza mbunge wao juu ya utengenezaji wa barabara unaotekelezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe)
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wananchi wa kijiji cha Wami(mbalwe)
kilichopo katika kata ya Ihalimba wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wameikataa
barabara inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe) kutokana na
kutengenezwa chini ya kiwango na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom
Engineers na kusababisha madhara ya kiafya kwa wananchi wa kijiji hicho.
Wakizungumza kwenye mkutano wa
hadhara ulihudhuriwa na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa,walimwambia
mbunge huyu kuwa mkarasi aliyepewa kazi ya kutengeneza barabara hiyo ameahibu
ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali.
“Mheshimiwa Mbunge wetu Mahmoud
Mgimwa tunakuomba kweli hii barabara imetengenezwa chini ya kiwango kweli kweli
kiasi cha kusababisha magonjwa ya kifua na mafua na kusababisha kuanza kuingia
gharama ambazo zipo nje ya bajeti zetu sisi wananchi hivyo unapaswa kuliangalia
swali hili kwa njia ya kutuokoa wananchi wako” walisema wananchi
Wananchi hao waliongeza kwa
kusema kuwa mkandarasi huyo amekuwa anamajibu mabaya yasiyolizisha kwa wananchi
na viongozi wa kijiji hicho kwa kuwa kazi hiyo walipewa na serikali ya mkoa wa
Iringa hivyo mtu pekee wa kuwawajibisha ni serikali ya mkuu wa Mkoa na sio mtu
mwingine yeyeto yule.
“Mbunge huyu mkandarasi
anakiburi na anamajibu mabaya mno maana ametengeneza barabara chini ya kiwango
na kusababisha madhara kwa wananchi ila kila akiulizwa hatoe majibu ya
kurizisha kwa wananchi hata kwa viongozi wetu” alisema mmoja ya mwananchi aliyekuwepo kwenye mkutano huo wa hadhara
Aidha wananchi hao walisema
kuwa utengenezwaji wa barabara hiyo unaotengenezwa na kampuni ya Fabec civil,Building
and Telecom Engineers umesababisha kukatika kwa masaliano ya kijiji hicho kwa
kuwa hakuna usafiri wa magari ya abiria yanayofanya safari kuelekea katika
kijiji hicho.
“Huku saizi hakuna usafiri wa
gari yeyeto ya abiria ambao unafika huku
kutokana na mkandarasi huyu kukata mawasialiano ya barabara yetu hii ambayo
hapo awali ilikuwa inapitika vizuri na mabasi yalikuwa yanakuja na tulikuwa tunasafiri saizi hakuna kitu
mheshimiwa mbunge Mgimwa” walisema wananchi
Akijibu hoja hizo za wananchi
wa kijiji cha wami(mbalwe) mbunge wa jimbo hilo Mahmoud Mgimwa alikiri kuwa
kuwa hata yeye hakubariani na utengenezaji wa barabara hiyo kutokana na
mkandarasi huyo kutengeneza barabara hiyo chini ya kiwango na kusababisha
madhara kwa wananchi wa kijiji cha wami(mbalwe)
“Saizi naona mnaguna hapa
kutokana na kupata ugonjwa wa mafua kutokana kutengenezabarabara chini ya
kiwango na kusababisha vumbi jingi ambalo linasababisha magonjwa hayo na
imekata mawasialiano ya usafiri kwa wananchi hao” alisema Mgimwa
Mgimwa alirazimika kumpigia
simu meneja wa TARURA wilaya ya Mufindi enjinia Sanga kusitisha malipo kwa
mkandarasi huyo kwa kuwa amekuwa akifanya kazi chini ya kiwango na amekuwa na
majibu ambayo siyo ya kulidhisha kwa wananchi pale wanapohoji kiwa njo na
kutengeneza barabara hiyo.
“Nakuomba meneja kuanzia sasa sitisha
malipo kwa mkandarasi huyo hadi pale atakapo kamilisha kutengeneza barabara
hiyo ili kurahisisha maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho” alisema Mgimwa
Kwa upande wake msimamizi wa
miradi ya kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers Heri Rubeni
alisema kuwa magari na vitendea kazi vyao vingi vimeharibika toka wiki
iliyopita hivyo wapo kwenye matengenezo na vifaa hivyo vikikamilika ndio
watarudi kazini na kuanza kufanya kazi upya.
08:53
Friday, 26 July 2019
LUKAKU AICHUNGULIA KWA MBAALI MAN U!....
Romelu Lukaku Muda mchache mara baada ya Manchester United kurejea England ikitokea ziarani barani Asia amekwea pipa kuelekea nchini Ubelgiji.
Habari zinaeleza kuwa Lukaku ameamua kwenda kwao Ubelgiji kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo na Inter Milan ya Italia.
Mipango ikamilika huenda msimu ujao akaitumikia timu ya Inter Milan ambao wamekuwa wakihaha kuipata saini yake.
United imewaambia Inter Milan wafanye haraka kusaka mkwanja kabla ya gosti 8 wakichelewa hawatampata tena na dau ambalo wanataka ni pauni milioni 75.
17:54
LIONEL MESSI KIBOKO YA RONALDO KWA MKWANJA...
Lionel Messi mshambuliaji wa Barcelona inayoshiriki La Liga yeye anaongoza kwa kukunja mkwanja mrefu kuliko wengine wanaopiga soka kwa sasa.
Kwa mwezi anakunja euro milioni 8.3 sawa na shilingi bilioni 21.3 kwa mwezi, hapo ni kabla ya kodi.
Cristiano Ronaldo kwenye Ligi ya Serie A yeye ni namba moja anakipiga Juventus, kwa mwezi anakunja euro 4,7
shilingi bilioni 12.1 kwa mwezi ni kinara ndani ya Seria A.
Neymar Jr yupo Ligue 1 anakunja euro milioni 3.6 kwa mwezi sawa na shilingi bilioni 7.8.
17:44
KATIKA MAKOCHA 100 WANAOOMBA KUINOA TAIFA STARS HAKUNA KOCHA HATA MMOJA MZAWA, JE NI UOGA AMA MASILAHI KIDUCHU?
Wilfredy Kidao, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kuwa mpaka sasa tayari wamepokea maombi ya makocha 100 wanaotaka nafasi ya kuinoa timu ya Taifa.
Katika orodha hiyo hakuna hata jina moja la mzawa ambaye ameomba kuinoa timu ya Taifa ya Tanzania baada ya Kocha Mkuu Emmanuel Ammunike kusitishiwa mkataba wake baada ya kuboronga kwenye michuano ya Afcon 2019 nchini Misri.
"Tumepokea maombi ya makocha zaidi ya 100 wakitaka kazi ya kuifundisha timu ya Taifa, maombi ni mengi na tunayafanyia kazi.
"Kwa sasa nguvu zeru tunazielekeza kwenye michuano ya Chan na kwenye maombi hayo 100 hakuna mzawa hata mmoja," amesema.
17:40
TAHA WATAKIWA KUFANYA TAFITI ZA KUWAKOMBOA WAKULIMA NCHINI TANZANIA
Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) iliyofanyika katika mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.
Meneja miradi Taasisi ya Tanzania Horticultural Association SASI (TAHA) Bi. Elianchea Shanga akiongea na wakulima na wageni waalikwa wakati wa sharehe za wakulima wa mazao ya mboga mboga yaliyoandaliwa taasisi ya TAHA iliyofanyika katika mjini humo.
Wakulima wa Mboga Mboga akinyoosha mikono kujitambulisha.
Meneja mradi Naimana akizungumza wakati akitambulisha mradi huo huku wakulima na wageni waalikwa wakifuatilia.
Mmiliki wa shamba la nyanya la kisasa akiongea machache.
Kilima cha kisasa cha nyanya.
Mgeni rasmi Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akipewa maelezo juu ya kilimo cha kisasa cha nyanya kutoka kwa Meneja mradi huo Naimana.
Vingozi wa kijiji wakiwa na Mgeni rasmi.
Wakulima wakiwa na mgeni rasmi.
Meneja mradi Naimana akizungumza wakati akitambulisha mradi huo huku wakulima na wageni waalikwa wakifuatilia.
Mmiliki wa shamba la nyanya la kisasa akiongea machache.
Meneja miradi TAHA Bi. Elianchea Shanga akiwatambulisha mabwana shamba wanaosaidia kufundisha wakulima.
Wafanyakazi wa TAHA wakitoa elimu kwa wakulima.
Kilima cha kisasa cha nyanya.
Mgeni rasmi Afisa Kilimo wa mkoa wa Morogoro Isabela Chilumba akipewa maelezo juu ya kilimo cha kisasa cha nyanya kutoka kwa Meneja mradi huo Naimana.
Vingozi wa kijiji wakiwa na Mgeni rasmi.
Wakulima wakiwa na mgeni rasmi.
17:35
CHATO WAITAMANI DHAHABU YA KIJANI ILIYOPO WILAYA YA MUFINDI
Mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akipata maelezo kutoka kwa mkurugenzi wa Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo jinsi gani wanavyoweza kuzalisha miche ya miti ambayo inakuwa kwa muda mfupi sana
Mkuu wa msafara huo Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri akiwa na baadhi ya viongozi wa kutoka mkoa wa Geita walipokuwa kwenye ziara ya kutembelea shamba la miti ya kupandwa la Sao Hill lililopo mkoani Iringa

Moja kati ya maeneo ambayo yanatumika kuzalia miche ya miti
Uchumi wa wilaya ya Mufindi mkoani Iringa umetajwa kutegemea zao
la miti katika kukuza uchumi na kuongeza pato la taifa tofauti ya wilaya
nyingine kama Chato ambao wamekuwa wakitegemea ufugaji,uchimbaji wa dhahabu,uvuvi
na kilimo
Hiyo imebainika wakati wa ziara ya baadhi ya viongozi wa wilaya
ya Chato,Mkoa wa Geita na viongozi wa vijiji vinavyolizunguka Shamba la Miti la
Biharamulo lililopo mkoani Geita baada ya kutembelea Shamba la Miti Sao Hill
linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa lengo la
kujifunza shughuli mbalimbali za uendeshaji katika shamba hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa msafara huo Mkuu wa
Wilaya ya Chato Mhe. Eng. Mtemi Msafiri alisema kuwa kwa mara ya kwanza
amejifunza faida kubwa inayotokana na zao la miti katika kukuza uchumi wa nchi
na kujionea jinsi gani wananchi wa wilaya ya Mufindi wanavyonufaika na dhahabu
ya kijani
“Leo ndio nimegundua kuwa zao la miti ni dhahabu ya kijani kwa
namna inavyosaidia kukuza uchumi tofauti na walivyodhani hapo awali kwa namna
ambavyo wao wamekuwa wakitegemea kuchimba dhahabu ambazo hazionekani tofauti na
zao la miti ambavyo limekuwa linaonekana” alisema Eng Msafiri
Eng Msafiri alisema kuwa shamba la Miti Sao Hill ndilo shamba
kubwa zaidi kati ya mashamba yote ya Serikali na ni nguzo ya maendeleo, na
mkombozi wa mazingira wa Wilaya ya Mufindi na mikoa ya Nyanda za Juu Kusini
nasi tumeona ni vema tujifunze kutoka kwa wenzetu.
“Tumejionea jinsi shamba hili lilivyo kuwa dhahabu ya ukuaji wa
sekta ya viwanda vidogo na vikubwa vya uchakataji wa mbao, linavyosaidia
kuongezeka kwa ari ya upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira kwa wananchi
wanaozunguka shamba na wananchi wa Wilaya za Mufindi, Kilombero na jamii jirani
wamekuwa wakipatiwa gawio la asilimia 5 ya mrahaba kila mwaka”alisema Eng.
Msafiri.
Eng. Msafiri anasema ziara hiyo imeweza kuwafumbua macho na
kuona jinsi gani shamba hilo lilivyo toa fursa ya ajira zinazotokana na
kazi za msimu za mashambani na viwanda tegemezi vya mazao ya misitu, fursa za
uwekezaji, na ufugaji wa nyuki unaotokana na na uwepo wa misitu ya asili
na ile ya kupandwa pamoja na vyanzo mbalimbali vya maji.
Awali akitoa ufafanuzi wa shamba la Sao Hill mkurugenzi wa
Rasilimali Misitu na Nyuki TFS, Zawadi Mbwambo alisema shamba hilo ni
miongoni mwa mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya serikali ambayo yanasimamiwa na
wizara ya maliasili na utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
“Shamba la Sao Hill lililopo hapa Mufindi lilianzishwa kwa
majaribio mnamo mwaka 1939 hadi mwaka 1951 na upandaji kwa kiasi kikubwa
ulianza rasmi mwaka 1960 hadi 1980 na
shamba hilo linaukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya
upandaji wa miti na uhifadhi wa
mazingira” alisema Mbwambo
Mbwambo alisema shamba hilo limehamasisha kwa kiwango kikubwa
upandaji wa miti kwa jamii inayolizunguka ambapo pia hutoa msaada wa mafunzo na
miche ya miti kwa ajili ya kupandwa ili kupambana na uharibifu mkubwa wa misitu
unaoendelea nchini.
“Takribani hekta 372,000 ya misitu inapotea kila mwaka na
ili misitu hii isiweze kupotea tunatakiwa tuendelee kupanda angalau hekta
185,000 kwa mwaka kwa hapa Mufundi na Ukanda wote wa Nyanda za Juuu Kusini
hamasa ya kupanda miti imekuwa kubwa kutokana na thamani inayoonekana Sao Hill
kiasi kwamba imefikia hatua sasa Serikali inawaelimisha watu waache baadhi ya
maeneo kwa ajili ya kilimo cha mazao mengine ya chakula na biashara” Alisema
Mbwambo.
Kwa upande wake meneja wa Shamba la Miti la Biharamulo Thadeus
Shirima alisema kupitia ziara hiyo ya siku mbili anaamini sasa kutakuwa na
uelewa wa pamoja wa umuhimu wa shamba hilo katika kuleta maendeleo katika Kanda
ya Ziwa na Tanzania kwa ujumla.
Thadeus alitoa shukurani kwa Mkuu wa Wilaya ya Chato, kamati ya
Ulinzi na Usalama ya Wilaya Chato na Mkoa wa Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Wilaya ya Chato na Bukombe kwa msaada na maelekezo yao muhimu
yaliyosaidia kuhakikisha uanzishwaji wa Shamba la Miti la Biharamulo
unafanikiwa kwa kufanikisha kuwaondoa wananchi waliovamia msitu wa hifadhi
Biharamulo ili kuanzishwa shamba hilo la miti.
Ziara hiyo ina wajumbe 45 ambao vingozi wa Wilaya na Mkoa wa
Geita, Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita, Mkurugenzi wa halmashauri,Wenyeviti wa
Vijiji, Madiwani, Maafisa tarafa, Jeshi la Zima moto na uokoaji, Mwenyekiti na
katibu wa Chama cha Mapinduzi, baadhi ya Wakuu wa Vitengo na Idara za
Halmashauri ya Wilaya, baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya , Katibu Tawala wa Wilaya na Wataalamu kutoka Shamba la miti
Biharamulo.
17:32
Subscribe to:
Posts (Atom)
















