BREAKING

Tuesday, 20 August 2019

WANANCHI WA KIJIJI CHA WAMI NA MBUNGE MGIMWA WAIKATAA BARABARA INAYOTENGENEZWA NA KAMPUNI YA FABEC CIVIL AND TELECOM ENGINEERS

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiungana na wananchi kuikataa barabara ambayo inatengenezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe) akiwa na sambamba na diwani wa kata ya Ihalimba

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiungana na wananchi kuikataa barabara ambayo inatengenezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe)

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa mbunge wa  jimbo la Mufindi Kaskazini wakimsikiliza mbunge wao juu ya utengenezaji wa barabara unaotekelezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe)

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.



Wananchi wa kijiji cha Wami(mbalwe) kilichopo katika kata ya Ihalimba wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wameikataa barabara inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe) kutokana na kutengenezwa chini ya kiwango na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers na kusababisha madhara ya kiafya kwa wananchi wa kijiji hicho.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulihudhuriwa na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa,walimwambia mbunge huyu kuwa mkarasi aliyepewa kazi ya kutengeneza barabara hiyo ameahibu ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali.

“Mheshimiwa Mbunge wetu Mahmoud Mgimwa tunakuomba kweli hii barabara imetengenezwa chini ya kiwango kweli kweli kiasi cha kusababisha magonjwa ya kifua na mafua na kusababisha kuanza kuingia gharama ambazo zipo nje ya bajeti zetu sisi wananchi hivyo unapaswa kuliangalia swali hili kwa njia ya kutuokoa wananchi wako” walisema wananchi

Wananchi hao waliongeza kwa kusema kuwa mkandarasi huyo amekuwa anamajibu mabaya yasiyolizisha kwa wananchi na viongozi wa kijiji hicho kwa kuwa kazi hiyo walipewa na serikali ya mkoa wa Iringa hivyo mtu pekee wa kuwawajibisha ni serikali ya mkuu wa Mkoa na sio mtu mwingine yeyeto yule.

“Mbunge huyu mkandarasi anakiburi na anamajibu mabaya mno maana ametengeneza barabara chini ya kiwango na kusababisha madhara kwa wananchi ila kila akiulizwa hatoe majibu ya kurizisha kwa wananchi hata kwa viongozi wetu” alisema mmoja ya mwananchi  aliyekuwepo kwenye mkutano huo wa hadhara

Aidha wananchi hao walisema kuwa utengenezwaji wa barabara hiyo unaotengenezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers umesababisha kukatika kwa masaliano ya kijiji hicho kwa kuwa hakuna usafiri wa magari ya abiria yanayofanya safari kuelekea katika kijiji hicho.

“Huku saizi hakuna usafiri wa gari yeyeto  ya abiria ambao unafika huku kutokana na mkandarasi huyu kukata mawasialiano ya barabara yetu hii ambayo hapo awali ilikuwa inapitika vizuri na mabasi yalikuwa yanakuja  na tulikuwa tunasafiri saizi hakuna kitu mheshimiwa mbunge Mgimwa” walisema wananchi

Akijibu hoja hizo za wananchi wa kijiji cha wami(mbalwe) mbunge wa jimbo hilo Mahmoud Mgimwa alikiri kuwa kuwa hata yeye hakubariani na utengenezaji wa barabara hiyo kutokana na mkandarasi huyo kutengeneza barabara hiyo chini ya kiwango na kusababisha madhara kwa wananchi wa kijiji cha wami(mbalwe)

“Saizi naona mnaguna hapa kutokana na kupata ugonjwa wa mafua kutokana kutengenezabarabara chini ya kiwango na kusababisha vumbi jingi ambalo linasababisha magonjwa hayo na imekata mawasialiano ya usafiri kwa wananchi hao” alisema Mgimwa

Mgimwa alirazimika kumpigia simu meneja wa TARURA wilaya ya Mufindi enjinia Sanga kusitisha malipo kwa mkandarasi huyo kwa kuwa amekuwa akifanya kazi chini ya kiwango na amekuwa na majibu ambayo siyo ya kulidhisha kwa wananchi pale wanapohoji kiwa njo na kutengeneza barabara hiyo.

“Nakuomba meneja kuanzia sasa sitisha malipo kwa mkandarasi huyo hadi pale atakapo kamilisha kutengeneza barabara hiyo ili kurahisisha maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho” alisema Mgimwa

Kwa upande wake msimamizi wa miradi ya kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers Heri Rubeni alisema kuwa magari na vitendea kazi vyao vingi vimeharibika toka wiki iliyopita hivyo wapo kwenye matengenezo na vifaa hivyo vikikamilika ndio watarudi kazini na kuanza kufanya kazi upya.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube