BREAKING

Friday, 12 October 2018

DSTV WAENDELEA KUWAPA RAHA WATANMZANIA ,MECHI YA STARS NA CAPE VERDE ITAKUWA LIVE SUPERSPORT10

Habari  njema kwa kuwa  Watanzania wataishuhudia timu ya taifa, Taifa Stars Mubasharaa ikiivaa Cape Verde ugenini, kesho.

Mechi hiyo ya kuwania kufuzu Afcon, itaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya SuperSport10 kupitia king'amuzi cha Dstv.

Katika taarifa iliyotolewa na Multichoice Tanzania, mechi hiyo itarushwa moja kwa moja kutoka mjini Praia kuanzia saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Watanzania wengi wapenda michezo na hasa soka walikuwa wakiuliza kama mechi hiyo itarushwa moja kwa moja lakini sasa wana uhakika wa mambo kwamba wataishuhudia mechi hiyo muhimu ya kuwania kufuzu kucheza Afcon, mwakani.

Wednesday, 10 October 2018

MAWAZIRI WA SEKTA YA KILIMO WATUAMA JIJINI DODOMA KUJADILI UTEKELEZAJI WA ASDP AWAMU YA PILI



Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb)  akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Kutoka kushoto ni waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Willium Lukuvu (Mb), Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) na Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji wakifatilia kwa umakini kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akieleza umuhimu wa kuanza haraka utekelezaji wa ASDP II wakati wa kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.
Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mhe Willium Lukuvu (Mb), akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelezaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018. Mwingine ni Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba.
Naibu waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji akieleza utayari wa ushiriki wa wizara yake wakati wa kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.
Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb)  akizungumza jambo wakati akifungua kikao cha Mawaziri wa sekta za kilimo juu ya utekelzaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) leo tarehe 10 Octoba 2018.

Na Mathias Canal, WK-Dodoma

Mawaziri wa wizara za sekta ya kilimo leo tarehe 10 Octoba 2018 wametuama  kwa masaa kadhaa Mjini Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kujadili kwa kina kuhusu maandalizi ya utekelezaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

Wizara washirika katika kutekeleza ASDP II ni pamoja na Wizara ya kilimo, Wizara ya mifugo na Uvuvi, Wizara ya Viwanda, Biashara, na Uwekezaji Wizara ya Maji, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi, na Ofisi ya Rais-TAMISEMI.

Utekelezaji wake utachagizwa pia na Wabia wa maendeleo, Sekta binafsi, Taasisi zisizo za kiserikali, Wakulima, Wafugaji na Wavuvi.

Mawaziri hao wakiongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) wameridhia kwa pamoja kuanza haraka utekelezaji wa mradi huo wa ASDP II ambao utakuwa chachu ya ukuzaji wa uchumi kupitia kilimo.

Majadiliano hayo yalijikita zaidi kujadili mapendekezo ya kikao cha makatibu wakuu wa wizara za sekta ya kilimo kilichofanyika tarehe 30 Agosti 2018 pia kujadili namna bora ya Uratibu wa ASDP II, na Mikakati ya kutafuta fedha za kugharamia utekelezaji wa ASDP II.

Katika Mkutano huo Mwenyekiti ambaye ni Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na walemavu Mhe Jenista Mhagama (Mb) aliitaka timu ya ASDP II Taifa kueleza kwa kina mikakati ya kuboresha masoko ya mazao ya kipaumbele yaliyoainishwa katika utekelezaji wa ASDP awamu ya pili.

Alisema kuwa kumekuwa na uhamasishaji mkubwa kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kulima pindi unapofika msimu wa kilimo lakini bado hamasa ya kutafuta masoko ni ndogo jambo ambalo linageuka karaha kwa wakulima nchi hivyo muarobaini wa kutafuta masoko ndio njia pekee ya kumkomboa mkulima.

Kwa upande wake Waziri wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba akizungumza katika kikao hicho alisema kuwa “ Majira ya Nchi yetu tunaendeshwa na msimu wa kilimo hivyo tunapaswa kutekeleza mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo kwa haraka ili kuendana na msimu” Alisema

Aidha, alisema kuwa punde utekelezaji utakapoanza wafadhili wa mradi huo wanapaswa kupewa uhuru wa kuchagua eneo watakalosaidia ili kuongeza chachu na ufanisi wa haraka katika uwajibikaji.

Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Ashatu Kijaji amewahakikishia mawaziri hao wa sekta za kilimo kuwa, wizara yake imejipanga vyema katika utekelezaji wa Mpango wa kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II).

“ Wengi wamezoea kuiita wizara yetu kama wizara ya madeni sasa tumejipanga vyema katika utekelezaji wa ASDP II kwani tunaamini kabisa kuwa ili kuwa na uchumi mzuri ulioimarika kwa wananchi na Taifa kwa ujumla tunahitaji kuwa na kilimo madhubuti “ Alikaririwa Dkt Kijaji

ASDP II inalenga katika mnyororo wa thamani wa mazao ya kipaumbele na ikolojia ya kanda ya kilimo tofauti na utekelezaji wa ASDP awamu ya kwanza ambao ulifanyika nchi nzima na kuwa na miradi karibu sekta ndogo zote za serikali na vipaumbele na maamuzi ya uwekezaji wa Mamlaka za serikali za mitaa.

Katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ASDP II Mazao ya kipaumbele yaliyochaguliwa kwa kilimo ni Mchele, Mahindi, Mtama/Uwele, Muhogo, Mboga/Matunda, Mazao ya Mbegu za mafuta (Alizeti, Ufuta, Nazi, Michikichi n.k) Pamba, Kahawa, Sukari, Korosho, Chai, Viazi mviringo na vitamu, Mikunde, Ndizi, na kwa Mifugo na Uvuvi ni Maziwa, Nyama (Ng’ombe), Mbuzi na Kondoo, Kuku, samaki na Mwani.

Malengo ya ASDP II ni kuleta mageuzi ya sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ili kuongeza uzalishaji na tija, kufanya kilimo kiwe cha kibiashara zaidi na kuongeza pato la wakulima wadogo kwa ajili ya kuboresha maisha yao, usalama wa chakula na lishe.

Tuesday, 9 October 2018

STARS KUPAA KUELEKEA CAPE VERDE USIKU LEO..


Serikali imewaomba  watazania kuendelea kujitokeza Kwenda nchini Cape Verde kuishangilia  timu ya taifa ya Tanzania,Taifa stars 

Akizungumza na wandishi wa habari jinin Dar es salaam Mkurugenzi wa maendeleo ya michezo nchini Yusuph Singo amesema bado nafasi ipo wazi kwa watanzania kusafiri na timu kesho kuelekea Cape Verde.

Kwa upande wake makamu wa raisi wa TFF amewatoa hofu watanzania kuhusiana na maandalizi ya mchezo huo.

Stars itaondoka kesho saa tano usiku na ndege ya serikali kuelekea nchini Cape Verde na itashuka dimbani kuwakabili wenyeji hao oktoba 12.

KONGAMANO LA AJIRA BINAFSI LAFANYIKA MKOANI MOROGORO

DSC_0006
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi  mjini Morogoro juzi, lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu na  watoto  mkoani humo .DSC_0015
Washiriki wa kongamano hilo.
DSC_0018

DSC_0019
Kongamano likiendelea.
DSC_0020

DSC_0022

DSC_0024

DSC_0033
Mtoa mada Mogani Isdori akitoa mada kuhusu ulipaji kodi.
DSC_0055
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo akitoa mada kuhusu matumizi ya mitandao.
DSC_0062
Mwanachuo cha Jordan cha mjini Morogoro, Aviva Chrispin akiuliza swali.
DSC_0068
Mjasiriamali, Neema Heri akitoa ushuhuda wa mafanikio yake.
DSC_0070
Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo SUA, Dk.Suleiman Rashid akitoa mada kuhusu umuhimu wa vifungashi kwenye Tangaza na kuongeza thamani ya bidhaa.
DSC_0080
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo akizungumzia umuhimu wa vifungashio na kuongeza thamani ya bidhaa.
DSC_0083
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka  akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi wa kongamano hilo, DC Mchembe pamoja na watoa mada.
DSC_0092

Mjasiriamali, Sara Ngonyani akitoa mada.
DSC_0114

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu, akihutubia.
DSC_0129
Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe, akimkabidhi zawadi ya saa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo.
DSC_0139
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF, Mwajabu Dhahabu akimkabidhi zawadi ya picha baba yake Mzee Dhahabu.
DSC_0144
Picha ya pamoja.
DSC_0149
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa katika picha ya pamoja na vijana walioshiriki katika kongamano hilo.
DSC_0156
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Gairo.
DSC_0160
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo, akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya WICOF.

WANAWAKE nchini wametakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu na wabunifu ili waweze kuinuka kiuchumi.

Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Gairo, Siriel Mchembe mjini Morogoro juzi wakati akifungua kongamano la siku moja la ajira binafsi lililoandaliwa na Taasisi ya WICOF inayojishughulisha na masuala ya kijamii hususani, walemavu, watoto na wazee   mkoani Morogoro.

"Ili mjikomboe kiuchumi mnatakiwa kuthubutu, kuwa wavumilivu nawabunifuna uiunga katika vikundi vya ujasiriamali muweze kupata mikopo nakufanyashughuli mbalimbali za biashara" alisema Mchembe.

Alisema dhana ya  50 kwa 50 kati ya wanaume na wanawake si kuosha vyombo bali ni mwanamke kuweza kufanya kazi za uzalishaji mali kama wanavyofanya wanaume na kumiliki ardhi.

Akizungumza wakati akitoa mada katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Trumark, Agnes Mgongo aliwataka wanawake hao kutumia mitandao ya kijamii kwa maufaa badala ya kuitumia kwa masuala yasiyo na tija.

"Jamani wanawake wenzangu tutumie simu zetu kwa ajili ya maendeleo, kama kupeana taarifa, kutafuta masoko ya bidhaa zetu na si vinginevyo" alisema Mgongo.

Akitoa zawadi ya pekee katika kongamano hilo alisema kwa kutambua umuhimu wa mtoto wa kike Shule ya John The Baptist Girls High School imetangaza fursa ya kusomesha bure wanafunzi  watatu wa kidato cha kwanza na watatu wengine hadi cha nne kwa mwaka 2019.

Alisema anachotakiwa kufanya mwanafunzi ni kufika shuleni hapo siku yoyote ndani ya mwezi wa oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mtihani wa kuchuana na kuwa fursa hiyo imetolewa na Mfuko wa Ndibalema John Mayanja Memorial Scholarship.

Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Mwajabu Dhahabu alisema kuwa kongamano hilo lenye lengo la kuwajengea uwezo ajira binafsi watoto wa kike ni la kwanza tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo mwaka jana.

Alisema kufanyika kwa kongamano hilo ni maandalizi ya kuelekea katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani yatakayofanyika hivi karibuni.s

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka akizungumza katika kongamano hilo alisema serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk.John Magufuli imeweka mazingira mazuri ya kuwasaidia wajasiriamali na kuwa imetenga fedha  kwa ajili ya kuwakopesha hivyo akato mwito kwa wajasiriamali hao kuongeza thamani ya bidhaa zao kwa kuziweka katika vifungashio vilivyobora. 

Katika hatua nyingine Mtaka aliipongeza kampuni ya Trumark kwa kazi kubwa inayoifanya ya kuwasaidia vijana  kuzitambua fursa za maendeleo na akatoa mualiko kwa wajasiriamali hao kwenda Simiyu kwenye maonyesho ya viwanda vidogo vidogo (SIDO) yatakayofanyika kuanzia Oktoba 23 hadi 28.

Kongamano hilo lilihitimishwa kwa makundi mbalimbali pamoja na watoa mada kupata zawadi na vyeti vya ushiriki. 

Thursday, 4 October 2018

NEYMAR APIGA HAT TRICK PSG YAWAFUMUA RED STAR 6-0 PARIS


Mshambuliaji Mbrazil, Neymar da Silva Santos Junior, maarufu tu kama Neymar akishangilia baada ya kuifungia mabao matatu Paris Saint-Germain dakika za 20, 22 na 81 katika ushindi wa 6-1 dhidi ya Red Star Belgrade kwenye mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa Jumatano Uwanja wa Parc des Princes mjini Paris, Ufaransa. Mabao mengine ya PSG yamefungwa na Edinson Cavani dakika ya 37, Ángel Di María dakika ya 41 na Kylian Mbappe dakika ya 70 

DREAMLINER YA AIR TANZANIA KUIPELEKA TANZANIA CAPE VERDE, MASHABIKI WAITWA WAJITOKE





Timu ya Taifa Stars, itasafiri na ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner kwenda nchini Cape Verde kuwavaa wenyeji wao katika mechi ya kuwania kufuzu Afcon 2019 nchini Afcon. 

Ndege hiyo itaruka kwa saa 9 bila kutua hadi nchini humo. Mashabiki wametakiwa kujitokeza kukata tiketi kwa ajili ya kwenda kuishangilia Stars. Kikosi hicho na mashabiki wake watarejea siku hiyohiyo baada tu ya mechi.

Tayari Taifa Stars imeanza maandalizi ya mchezo huo chini ya kocha Emmanuel Amunike raia wa Nigeria.

Baada ya mechi hiyo, Stars itarejea nchini mara moja kuja kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Cape Verde jijini Dar es Salaam.

DKT TIZEBA AIPONGEZA MVIWATA KWA KUWAUNGANISHA WAKULIMA NCHINI

Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akitoa salamu za Wizara ya kilimo mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Baadhi ya wakulima wakifatilia Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro
Naibu Waziri wa kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) aakisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.
Waziri wa kilimo Mhe Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiru Ally mara baada ya kuwasili kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) Leo tarehe 3 Octoba 2018 katika uwanja wa Jamhuri Mjini Morogoro.

Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba (Mb) ameupongeza mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA) tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 kwa kuwa dira na Muungano wenye sauti moja yenye mshikamano na mafanikio makubwa kwa wakulima nchini.

Waziri Tizeba ametoa pongezi hizo Leo tarehe 3 Octoba 2018 wakati akitoa salamu za Wizara ya kilimo mbele ya Mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kwenye Maadhimisho ya miaka 25 ya mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania (MVIWATA).

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dkt Bashiri Ally, Waziri Tizeba alisema kuwa kipindi cha miaka 25 MVIWATA imekuwa mtandao wenye dhamira chanya kwa kuwaunganisha wakulima wadogo kwa kutetea maslahi yao na kujenga mikakati ya pamoja ya kujikwamua kijamii, kiuchumi na kiutamaduni.

Aliitaka MVIWATA kuwa inapaswa kusimamia zaidi maslahi ya wakulima nchini kwa kuwa wahusika wakuu na wamiliki wa mfumo wa uzalishaji na kuwa sehemu ya mfumo wa maamuzi ya masuala yahusuyo maisha ya wakulima wadogo hususani mfumo wa uzalishaji na rasilimali ardhi.

Dkt Tizeba aliwahakikishia wananchama hao zaidi ya 2000 walioshiriki katika kongamano hilo la siku tatu kuwa wakulima wanapaswa kueleza changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka iwezekanavyo.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Mtandao wa wakulima Tanzania (MVIWATA) Ndg Stephen Ruvuga akisoma risala ya maadhimisho hayo ameipongeza serikali katika kujenga uchumi wa Taifa katika kuimarisha sekta ya kilimo nchini.

Alisema kuwa kwa kutambua hilo na hususani katika matumizi ya fedha za umma aliongeza kuwa kunapaswa kuongeza msisitizo katika usimamizi wa matumizi ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Alisema kuwa pamoja na jitihada kubwa za serikali za kuimarisha sekta ya kilimo wakulima kwa ujumla bado wanachangamoto mbalimbali ikiwemo swala la ardhi, bei ya Mazao na soko la uhakika na mitaji ya uwezeshaji wakulima.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube