BREAKING

Monday, 13 August 2018

ARSENAL YA MZEE WENGER NA YA UNAI BADO NI HOI YACHAPWA BAO 2-0 NYUMBANI NA MAN CITY

















Saturday, 11 August 2018

PUMZIKA KWA AMANI MZEE KING MAJUTO

Image may contain: 1 person, smiling
Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za Msiba wa Msanii nguli na Bingwa wa tasnia ya Sanaa za uigizaji na vichekesho, Amir Athuman almaarufu "King Majuto" kilichotokea usiku wa Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimsumbua.
...
Kifo hiki kimenikumbuka miaka ile ya zamani alipoanza kuwika na msemo wa hamsini, hamsini mia akiwa na muigizaji mwenzake mkongwe Marehemu Mzee Small.
Kwa wasiomjua vyema King Majuto alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini mkoani Tanga. Alianza kuigiza mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa.
Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji, mwandishi wa mswada. Pia Mzee Majuto ni muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC).
Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki.
King Majuto ni kipaji halisia cha kuzaliwa cha uchekeshaji kuwahi kutokea hapa nchini. Wenzake walikuwa kina Mzee Jongo, Hamis Kitambi, Fundi Said (Mzee Kipara) na Mama Haambiliki.
Msiba huu ni majonzi makubwa sana kwa familia, Wasanii, Tasnia ya Filamu nchini, Wapenzi wa kazi zake za sanaa na Taifa kwa ujumla.
Daima tutakukumbuka kwa ufundi, ustadi wa uigizaji wako, vituko vyako, tabasamu lako, upendo wako kwa kila Mtu.
Pumzika kwa amani Mfalme na Bingwa wa vichekesho wa kipindi chote hapa nchini Mzee "King Majuto".
Inna lillaahi wainna ilaihi raajiuun.

KIWANGO DUNI CHA MAN U SI HOJA CHAITWANGA LEICESTER CITY 2-1


Kikosi cha Manchester United kimeanza harakati za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England msimu wa 2018/19 kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Leicester City.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Old Trafford, United imejipatia mabao yake kupitia kwa Paul Pogba aliyefunga kwa njia ya penati pamoja na Luke Shaw.

Bao pekee la Leicester limewekwa kimiani na Jammie Vardy aliyefunga kwa njia penati mnano dakika za mwisho.

Matokeo hayo yanifanya United kuwa kileleni kwa muda huku mitanange mingine ikisubiriwa kuendelea wikiendi hii.

MSIMU MPYA EPL, DSTV NI WALE WALE NA WANASEMA KAMA SIO DSTV POTEZEAAAAAAAA


Baada ya Msimu wa Kombe la Dunia kuisha tunarudi kwenye ratiba yetu rasmi ya Soka la Kibabe la Ligi ya EPL. 

Wanaotufungulia dimba Ijumaa hii ni mechi kati ya Manchester United dhidi ya Leicester City. Wazee wa kazi wanasema biashara asubuhi, je wabingwa hawa wataanzaje msimu huu? 


MAJIBU tutayapata Ijumaa hii ndani ya Supersport 3 Saa 3:50 usiku LIVE kwenye DStv pekee ikiwa kwenye Lugha yetu tamu adhimu ya Kiswahili.


Bila kusahau, wateja wa DStv wanaweza pakua “Download Application”  ya DstvNow  itakayowawezesha watanzania wengi kufurahia msimu huu wa soka kwani unachotakiwa tu ni kuwa na akaunti yako ya DStv na unaweza kutazama katika vifaa zaidi ya vinne kama vile simu, kompyuta, na televisheni ya kawaida ukiwa mahali popote wakati wowote!
Huu Moto hauzimi na kama sio DStv, Basi Potezea!


10Aug2018

Tuesday, 7 August 2018

UGENI WA RASI MAGUFULI IKULU....




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Gervas John Nyaisonga na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Dkt. Flavian Kasalla wakiwa na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Charles Kitima baada ya viongozi hao wapya wa kanisa kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018

DSTV WAIREJESHA LIGI YA ITALIA -SERIE A SASA WATEJA WAKE KUSHUHUDIA LIGI KUBWA ULIMWENGUNI KWA BEI 'KIDUCHU'

Baada ya kiu ya muda mrefu, sasa wateja wa DStv wataanza tena kushuhudia moja ya ligi maarufu kabisa duniani – Ligi ya Italia – Serie A sasa MultiChoice imetangaza habari njema kuwa kuanzia msimu huu, ligi hiyo itaonyeshwa mubashara kupitia DStv.
 
Mbali na Serie A ambapo atakuwepo nguli wa soka Cristiano Ronaldo, wateja wa DStv wataendelea kufurahia ligi na michuano mikubwa mingi duniani ikiwemo Ligi ya Uingereza (Premier League) na La Liga.
 

Mbali na habari za kurudi kwa Serie A, DStv pia itaongeza maudhui zaidi katika soka msimu huu. Watumiaji wa DStv Bomba, wataweza kuona zaidi ya mechi 100 katika michuano ya  Serie A na Ligi Kuu ya Uingereza, huku wateja wa DStv Family wao watakuwa wakipata mechi zote 380 za michuano ya Serie A na mechi zaidi ya 120 kutoka Ligi Kuu ya Uingereza. Watumiaji wa kifurushi cha DStv Compact, Compact Plus na wateja wa Premium watakuwa na upatikanaji wa mechi zote za Premium League, Serie A na mechi zote 380 za La Liga.

Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo (Kushoto) na Meneja Masoko Alpha Mria (Kulia) wakiwa na wachezaji wakongwe wa soka hapa nchini muda mfupi baada ya uzinduzi wa msimu wa soka ambapo DStv imetangaza kurejea kwa ligi ya Italia Serie A.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa msimu mpya wa soka,, Meneja uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo alisema wateja wa DStv watapata fursa ya kufurahia  msimu huu mpya wa soka na katika kunogesha zaidi amesema michuano ya ligi ya uingereza itatangazwa kwa lugha ya kiswahili.

Amesema pia huduma ya DStv Now ambayo inamuwezesha mteja kutazama DStv popote alipo itawafanya watanzania wengi kufurahia msimu huu wa soka kwani unachotakiwa tu ni kuwa na akaunti yako ya DStv na unaweza kutazama katika vifaa zaidi ya vinne kama vile simu, kompyuta, na televisheni ya kawaida.

3

Watangazaji maarufu wa Soka hapa nchini (kutoka kushoto) Maulid Kitenge, Aboubakar Liongo, Edo Kumwembe na Ephraem Kibonde wakiwa katika uzinduzi wa msimu mpya wa soka watangazaji hao watakuwa wakiwaletea matangazo ya ligi kuu ya uingereza msimu huu kwa kiswahili.
 

Thursday, 2 August 2018

ARSENAL YATOKA NYUMA NA KUIZIMA CHELSEA KWA MATUTA






Mshambuliaji Alexandre Lacazette akishangilia baada ya kuifugia Arsenal bao la kusawazisha dakika ya 90 na ushei ikitoa sare ya 1-1 na Chelsea katika mchezo wa kirafiki wa Kombe la Mabingwa wa Kimataifa Uwanja wa Aviva mjini Dublin kufuatia Antonio Rudiger kuanza kuifungia The Blues dakika ya tano. Arsenal ikaenda kushinda kwa penalti 6-5 kufuatia Ruben Loftus-Cheek kukosa penalti ya mwisho ya Chelsea na Alex Iwobi kufunga kwa upande wa Washika Bunduki wa London, ambao wapo chini ya kocha mpya, Mspaniola, Unai Emery aliyechukua nafaisi ya Mfaransa, Arsene Wenger mwezi uliopita. Waliofunga penalti za Arsenal ni Alexandre Lacazette, Reiss Nelson, Matteo Guendouzi, Ainsley Maitland-Niles, Mesut Ozil na Alex Iwobi wakati za Chelsea zimefungwa na Danny Drinkwater, Tammy Abraham, Victory Moses, Emerson na Lucas Piazon













 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube