Jacline Woiso-Mwanachama wa Rotary Club
Ili kuendana na kasi ya kidigital ya ukuajia wa teknolojia duniani Taasisi ya Rotary Klabu imetoa mafunzu ya Teknohama kwa walimu wa Shule tano za msingi katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam,.
Hamza kasongo Mwanachama Rotary Club akizungumza na walimu washiriki wa Mafunzo ya Kidigital
Ili kuendana na kasi ya kidigital ya ukuajia wa teknolojia duniani Taasisi ya Rotary Klabu imetoa mafunzu ya Teknohama kwa walimu wa Shule tano za msingi katika Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam,.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mwananchama wa Rotary Klabu Jackline Woiso amesema mafunzo hayo ni faida kubwa kwa walimu hao husuani kipindi hiki ambacho matumizi ya digital yanazidi kukua ambapo kuptia mafunzo hayo yatakapomalizika watakuwa wamepata faida.
Ameongeza mafunzo hayo kwa walimu zaidi ya 80 itawajengea uwezo wa kutumia teknolojia hiyo kwa upande wa uongozi na kuwajengea wanafunzi uwezo pindi wakiwa wakubwa kuendana na kasi ya Dunia
Kwa upande wake Dkt. Gaudensia Tesha Mhadhiri idara ya Kompyuta Chuo cha DIT amesema kuwa mafunzo hayo ya walimu kutumia vishikwambi itawasaidia kwa urahisi kuandaa matokeo ya mitihani yaweze kuchakatwa kwa urahisi, huku baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo Moses Fransis ambaye ni Mkuu wa Shule ya msingi Kunduchi akisema kuna changamoto kubwa baadhi ya walimu wengi hawana uelewa na mambo ya tehama hivyo itawasaidia kupunguza changamoto hiyo
No comments:
Post a Comment