Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wateule kuwa nguzo kubwa katika kutatua migogoro iliyopo kwenye jamii na sio kuisababisha migogoro.
Mhe. Rais Dkt. Samia amesema hayo kwenye uapisho wa viongozi wateule, Ikulu jijini Dar es Salaam, ambapo amesema mabadiliko ya viongozi ni mambo ya kawaida, ili kuimarisha ufanisi katika utendaji kazi kwa jamii na niwajibu wa viongozi kwenda kuwatumikia wananchi pindi wanapoteuliwa .
Aidha Rais Samia Suluhu Hassan amemtaka aliyekuwa Naibu Waziri wa Tamisemi, Deogratusi Ndejembi ambaye sasa ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu akimsihi kwenda kufanya kazi kwa ukaribu na ushirikianio na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Patrobas Katambi, huku akitoa maagizo ya kuhakikisha vijana wanapata ajira na kuajiriwa.
Katika hatua nyingine amekemea migongano ya kimadaraka katika taasisi walizopo kwani watakapofanya hivyo hatosita kuwaondoa wote wawili…
No comments:
Post a Comment