BREAKING

Wednesday, 3 April 2024

HAPI AULA U-KATIBU MKUU JUMUIYA YA WAZAZI CCM


Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) chini ya uenyekiti wa Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano, Aprili 3, 2024 imemteua aliyewahi kuwa mkuu wa mikoa ya Iringa na Mara, Ally Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa chama hicho.

Hapi anachukua nafasi ya Gilbert Kalima ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube