Afisa maendeleo bodi ya Filam nchini Simon Peter, amewaka watunzi wa Filam nchini kuwa wabunifu ili kuendelea kutengeneza soko kubwa la ajira kwa wasanii huku akiwakumbusha wasanii kuendelea kusajili kazi zao za sanaa katika Bodi ya filam
Hayo ameyasema wakati wa uzinduzi wa Tamthiliya ya Jiya mfalme wa Boma , ambayo imeshirikisha wasanii mbalimbali ikibeba maudhui ya kitanzania
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Masoko MultiChoice Tanzania Ronald Shelukindo akizungumza katika uzinduzi huo amesema kwamba kwa mara ya kwanza DSTV imepokea kazi yenye viwango vikubwa ikiwemo mchanganyiko wa wasanii maarufu na wasio maarufu.
Katika hatua nyingine kuelekea marudiano ya michuano ya vilabu bingwa Afrika ambapo Simba na Yanga zinatarajia kucheza michezo yao ambapo Simba watawavaa Al Ahly Ijumaa wiki hii na Yanga wakiwakabilia Mamelod Sundowns siku hiyo hiyo amazitakia kheria huku akisema timu hizo zinauwezo mkubwa wa kutinga hatua ya nusu fainali.
No comments:
Post a Comment