Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Daniel Chongolo akifuatilia baadhi ya mada katika mafunzo ya Viongozi vyama vya ukombozi |
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewaasa vijana kutoka bara la Afrika,ujitambua na kuwa tayari kuzitumikia nchi zao kwa weledi, uwezo na uzalendo mkubwa , hasa katika kuendeleza mambo mazuri yanyoambatana na kuongoza mapambano ya ukombozi wa kiuchumi kwa ajili ya wananchi
Chongolo amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Viongozi Makada wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika ya Mwaka 2023 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) iliyopo Kibaha kwa Mfipa, mkoani Pwani.
Aidha Chongolo amewataka vijana kutambua wajibu wa kuiandaa kwa wakati mwema wa uongozi kwa nyakati na mazingira ya sasa, ambapo wanatakiwa kujitambua na kubeba dhima ya uongozi unaolenga kuwatumikia watu kwa weledi na uzalendo mkubwa wa hali juu, kwa ajili ya kubadilisha na kuboresha hali za maisha ya watu.
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa takriban wiki mbili, ambapo yanawakutanisha vijana viongozi na makada wa Vyama mbalimbali vikiwemo vya MPLA, SWAPO, FRELIMO, ANC na ZANU PF, CCM pamoja na CPC.
No comments:
Post a Comment