BREAKING

Wednesday, 21 June 2023

DC MOYO AONDOA SINTOFAHAMU KATIKA MLIMA CHILALO



Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mbute juu ya sintofahamu ya uchimbaji wa madini katika mlima Chilalo

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwasikiliza wananchi wa Kijiji cha Mbute wakati wa kuondoa hofu kuwa Mlima Chilalo upo wilaya ya Ruangwa



Na Fredy Mgunda, Nachingwea

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amefanikiwa kuondoka sintofahamu kwa wananchi wa Kijiji cha Mbute iliyokuwa imetanda juu ya uchimbaji wa madini ya Graphite  katika mlima Chilalo

Akizungumza wakati alipofanya ziara katika Kijiji hicho baada kusambaa Kwa video ikionyesha malalamiko ya wananchi juu mlima na msitu wa akiba wa Chilalo kuonekana upo katika wilaya ya Ruangwa na sio Nachingwea.

Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo aliwaeleza wananchi kuwa Mlima Chilalo upo wilaya ya Nachingwea na kila shughuli inayofanywa kwenye Mlima huo mapato yote yatakuwa ya wananchi wa wilaya ya Nachingwea.

Moyo aliwatoa hofu hiyo kwa kuwaambia suala la mipaka linashughulikiwa na serikali ya mkoa wa Lindi kwa ofisi ya wilaya ya Nachingwea ilifanya kazi mgogoro huo ila bado upande wa mkoa na kuhaidi hivi karibuni wataalam kutoka TAMISEMI na ofisi mkoa watafika eneo hilo kutatua mgogoro huo.

Kwa upande wake Afisa madini mkazi mkoa wa Lindi Eng Dickson Joram alisema kuwa leseni iliyotelewa katika eneo la Mlima Chilalo ni leseni ya utafiti na sio ya kuchimbwa kwa madini ya Graphite katika eneo hilo.

Eng Joram alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuondoa hofu kuwa eneo hilo limeanza kuchimbwa madini wakati sio kweli.

Nao baadhi ya wananchi walisema kuwa wanampongeza mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo Kwa kuwapeleka wataalam na kutoa ufafanuzi juu ya uchimbaji wa madini ya Graphite katika mlima Chilalo

"Tumepata ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo mradi wa uchimbaji wa madini ya Graphite  Mlima Chilalo ambao umetulea hofu iliyokuwa imetanda Kwa wananchi"walisema

Tuesday, 20 June 2023

FOODPOINT WAPO MLANGONI KWAKO


 

Wednesday, 14 June 2023

ZIARA YA RAIS SAMIA -MWANZA YASHUSHA NEEMA AHAIDI KUKAMILISHA MIRADI YOTE YA KIMKAKATI




 

Monday, 12 June 2023

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE .SAMIA SULUHU HASSAN AFANYA MAZUNGUMZA NA MAKATIBU WA KIMATAIFA WA MPANGO WA DHARURA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mratibu wa Kimataifa wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani katika mwitikio wa kupambana na Ukimwi (PEPFAR) na Mwakilishi Maalum wa Serikali ya Marekani katika masuala ya Diplomasia ya Afya Balozi Dkt. John Nkengasong,  pamoja na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) Bw. Peter Sands,  Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma
tarehe 12 Juni 2023.





 

WAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA WAKUU WA MIKOA TANZANIA BARA





WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaelekeza Wakuu wa Mikoa yote ya Tanzania Bara, wakae na Mabaraza ya Biashara na Wamiliki wa kumbi za Starehe katika mikoa yao kwa madhumuni ya kutafuta muafaka wa pamoja katika utekelezaji wa sheria, kanuni, mwongozo kuhusu udhibiti wa athari zitokanazo na sauti zilizozidi viwango.

 Waziri Mkuu amezielekeza Idara za Mipangomiji katika halmashauri za wilaya zote nchini zitenge maeneo ya ujenzi wa nyumba za ibada kama wanavyotenga maeneo ya taasisi nyingine.  

Ametoa maelekezo hayo leo (Jumatatu, Juni 12, 2023) wakati akizindua Kongamano la Kujengewa Uelewa kuhusu madhara yatokanayo na sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada. Kongamano hilo liloandaliwa na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) limefanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Amesema ipo miongozo inayosimamiwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inayohusu masuala ya usimamizi wa mipango miji. “Nasisitiza toeni miongozo mahsusi ya mipango ya matumizi ya ardhi .” 

“Kwa upande wa udhibiti wa sauti zilizozidi, kila mamlaka iliyotoa vibali au leseni ya shughuli au biashara, zifuatilie mwenendo wa matumizi ya leseni hizo. Nasisitiza kuwa kila mamlaka itimize wajibu wake kulingana na maelekezo yaliyimo katika Mwongozo wa Uthibiti wa Uchafuzi wa Mazingira Utokanao na Kelele na Mitetemo uliotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais.”

Saturday, 10 June 2023

MELLECK :CIDAT TUTANUFAIKA NA BADARI


"Sisi kama Bandari kavu tutataneemeka na uwekezaji huu kwa kuwa tutapata kazi kubwa zaidi kwani mizigo mingi inahitajika kuondoka bandari na sisi watu wa bandari kavu tutapata kazi" Meleck  Shange Mwenyekiti Chama cha waendesha Bandari Kavu CIDAT

LIVE!! MJADALA KUHUSU MAENDELEO YA BANDARI NCHINI


 

https://www.youtube.com/live/_9s_ilgWrNM?feature=share

Friday, 9 June 2023

KATIBU MKUU CHONGOLO AKUTANA NA BALOZI WA CHINA NCHINI TANZANIA .


Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe  Daniel Chongolo lakutana na na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini Balozi Chen Mingjian, Ofisini kwake katika , Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

 

BENKI YA CRDB KUWAZAWADIA SH.MILION 15. 4 YA ADA YA SHULE WATEJA WAKE

 

Meneja Mwandamizi wa Mauzo Benki ya CRDB, Muhumuliza Buberwa akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni ya “Timiza Ndoto yake na Junior Jumbo” yenye lengo la kutoa elimu ya fedha kwa watoto na kuwahamasisha wazazi/ walezi juu ya umuhimu wa kuwawekea watoto wao akiba ambapo benki ya CRDB imetenga Shilingi milioni 15.4 kama zawadi ya ada kwa washindi wa kampeni hiyo inayotarajiwa kufanyika kwa kipindi cha mwezi mmoja, katika hafla fupi iliyofanyika kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini Dar es salaam leo. Wengine pichani ni Meneja Mauzo wa Benki ya CRDB, Amina Mawona (kushoto), na Meneja wa Benki ya CRDB Tawi la Buza, Mary Joshua. Hafla hiyo imefanyika leo katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB.

==========    ==========     ===========

Kuelekea Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka huu, Benki ya CRDB imezindua promosheni ya “Timiza Ndoto yake na Junior Jumbo” ikiwa na lengo la kuwahamasisha wazazi/ walezi juu ya umuhimu wa kuwawekea watoto wao akiba. 
 
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Meneja Mwandamizi wa Mauzo, Muhumuliza Buberwa amesema kupitia kampeni hiyo Benki ya CRDB pia imejipanga kutoa elimu ya fedha kwa watoto ili kuanza kuwaandaa mapema kukabiliana na changamoto za kifedha. “Tumekuwa tukiwafundisha watoto juu ya mambo mbalimbali katika maisha, lakini watoto walio wengi wanakosa elimu juu ya fedha na kujiwekea akiba, elimu ambayo ni muhimu sana kwa watoto na vijana wetu. 
 
Kampeni hii inakwenda kuhimiza juu ya ya umuhimu wa elimu, pamoja na kuwafundisha watoto kujenga utamaduni wa kuanza kujiwekea akiba,” amesema Buberwa. 

Akielezea kuhusu muda wa kampeni hiyo Meneja Mauzo wa Benki ya CRDB, Amina Mawona amesema katika promosheni hiyo ya “Timiza Ndoto yake na Junior Jumbo” ambayo inatarajiwa kufikia kikomo Julai 5, 2023, Benki ya CRDB imetenga kiasi cha shilingi milioni 15.4 kama zawadi ya ada kwa ajili ya watoto 21 ambapo kila kanda ya benki hiyo kunatarajiwa kuwa na washindi watatu. 
 
“Mshindi wa kwanza katika kila kanda atajishindia Shilingi Milioni 1, mshindi wa pili Shilingi laki 7, na mshindi wa tatu Shilingi laki 5, hivyo kufanya jumla ya zawadi za Shilingi milioni 15.4. Lengo la promosheni hii ni kuhamasisha wazazi kujenga utamaduni wa kuwawekea akiba watoto,” aliongezea Amina. Kushiriki katika promosheni hiyo, mzazi/ mlezi anatakiwa awe amefungulia akaunti ya “Junior Jumbo” mtoto wake na kumuwekea akiba mara kwa mara au kumfundisha kuweka akiba mwenyewe. 
 
Mzazi anaweza kuweka fedha katika akaunti ya Junior Jumbo ya mtoto kwa kutembelea tawi, kwa CRDB Wakala, kwa kuhamisha fedha kutoka akaunti yake kupitia SimBanking au Internet banking au kutoka mitandao ya simu. 
 

Kwa upande wake Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Buza, Mary Joshua alisema wazazi wengi wamekuwa wakipata changamoto katika kulipa ada za Watoto kutokana na wengi kutokuwa na utamaduni wa kuweka akiba kwa ajili ya watoto. Hali hiyo imepelekea watoto wengi kuchelewa kurudi shule kuendelea na masomo au kujiunga na shule kwa wanafunzi wapya kutokana na kukosa mahitaji ya msingi ikiwamo ada. 
 
“Tuna wahimiza wazazi/ walezi kuwafungulia watoto akaunti ya Junior Jumbo na kuanza kuweka akiba kwa ajili ya watoto kidogo kidogo. Akaunti hii inafunguliwa kwa vigezo nafuu sana, haina makato yoyote na hutoa faida ya riba kwa mteja,” amesema Bi. Mary Joshua huku akisisitiza kuwa Benki ya CRDB imejipanga kutoa elimu kwa wazazi ili kuwasaidia kuishi ndoto za watoto wao kwa kuwawezesha kupata elimu bora. 
 
Meneja huyo alitoa rai pia kwa wazazi kutumia elimu inayotolewa na Benki ya CRDB kuwawekea akiba watoto wao kwani itasaidia sana kuweka msingi bora katika elimu. “Huu ni msimu wa sikukuu wengi wetu huwa tunafanya matumizi bila ya kujali January tunatakiwa kulipa ada pamoja na gharama nyengine za shule za watoto. Tunawahimiza kuweka akiba kwa ajili ya watoto kupitia akaunti ya Junior Jumbo,” aliongezea.

Thursday, 8 June 2023

CHONGOLO :TUMIKIENI MATAIFA YENU AWAASA VIJANA WA AFRIKA


Katibu Mkuu wa Chama cha mapinduzi Daniel Chongolo akiwahutubia Viongozi Makada wa vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika  katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) iliyopo Kibaha kwa Mfipa, mkoani Pwani.



Katibu
 wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Sophia Mjema, akisikiliza kwa makini Mada katika ufunguzi a Mafunzo ya Viongozi Makada wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika ya Mwaka 2023







Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Daniel Chongolo akifuatilia baadhi ya mada katika mafunzo ya Viongozi vyama vya ukombozi 

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  amewaasa  vijana kutoka bara la Afrika,ujitambua na kuwa tayari kuzitumikia nchi zao kwa weledi, uwezo na uzalendo mkubwa , hasa katika kuendeleza mambo mazuri yanyoambatana na kuongoza mapambano ya ukombozi wa kiuchumi kwa ajili ya wananchi 

Chongolo amesema hayo wakati akifungua Mafunzo ya Viongozi Makada wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika ya Mwaka 2023 katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) iliyopo Kibaha kwa Mfipa, mkoani Pwani.

Aidha  Chongolo amewataka vijana kutambua wajibu wa kuiandaa kwa wakati mwema wa uongozi kwa nyakati na mazingira ya sasa, ambapo wanatakiwa kujitambua na kubeba dhima ya uongozi unaolenga kuwatumikia watu kwa weledi na uzalendo mkubwa wa hali juu, kwa ajili ya kubadilisha na kuboresha hali za maisha ya watu.

Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa takriban wiki mbili, ambapo yanawakutanisha vijana  viongozi na makada wa Vyama mbalimbali vikiwemo vya MPLA, SWAPO, FRELIMO, ANC na ZANU PF, CCM pamoja na CPC.

Wednesday, 7 June 2023

RAIS MWINYI AKUTANA NA JUMUIYA YA WAZEE ZANZIBAR

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Uongozi wa Jumuiya ya Wastaafu na Wazee Zanzibar (JUWAZA) ukiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw.Aboud Talib Aboud (kulia kwa Rais) mazungumzo hayo yaliyofanyika katika  ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Katibu wa Jumuiya wa Wastaafu na Wazee Zanzibar (JUWAZA) Bi. Salama Kombo akizungumza na kuelezea kazi za jumuiya hiyo na kutoa shukrani kwa kuongeza kwa Pencheni Jamii kwa Wazee, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 7-6-2023 na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bw.Aboud Talib Aboud

WAZIRI GWAJIMA AWAPA NENO WAKUU WA MIKOA KUHUSU WAZEE NCH


 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza  na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, jijini Dodoma leo Juni 7,2023 kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.

Mwenyekiti wa  Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma Mzee Peter Mpolo,akizungumza  na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, jijini Dodoma leo Juni 7,2023 kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.


Sehemu ya wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze wakimsikiliza Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati ,akizungumza nao   jijini Dodoma leo Juni 7,2023 kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akiwa katika picha ya pamoja na wazee mara baada ya kuzungumza a na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, jijini Dodoma leo Juni 7,2023 kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.

Na.Alex Sonna-DODOMA

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,amewataka Wakuu wa Mikoa  kuhakikisha elimu ya kina inatolewa kwa wananchi juu ya haki, ulinzi, usalama na ustawi wa wazee.

Waziri Gwajima ameyasema hayo leo Juni 7,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wazee kata ya Mkonze, Mkoani Dodoma kuelekea Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayofanyika kila mwaka Juni 15.

Dkt. Gwajima amesema kuwa kutokana na kuboreshwa kwa huduma mbalimbali za kijamii nchini idadi ya wazee imeongezeka kutoka 2,507,568 hadi kufikia 5,008,339 ambayo ni sawa na asilimia 8.1 ya Watanzania 61,741,120.

Amesema Serikali imeendelea kuadhimisha Siku ya kupinga Ukatili Dhidi ya Wazee kila tarehe 15, Juni ambapo Maadhimisho haya muhimu kwa ajili ya kuuhabarisha umma juu ya haki, ulinzi, maendeleo na ustawi wa wazee wetu. Aidha, katika kulinda haki ya wazee kuishi, pia Serikali imeendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji kwa Wazee

“Ninachukua fursa hii pia kuwaomba Wakuu wa Mikoa yote nchini kuratibu maadhimisho haya kimikoa kwa kushirikiana na viongozi wa Mabaraza ya Wazee katika mikoa husika. Katika maadhimisho haya” amesema Waziri Dkt. Gwajima.

Waziri Gwajima ameendelea kusisitiza jamii yote kuacha kufanya ukatili kwa Wazee na makundi yote kwa ujumla na amewaomba Wanahabari kutumia vyombo vyao kuelimisha na kuendelea kukemea masuala ya ukatili nchini kote.

“Serikali itaendelea kuchukua hatua stahiki kuwashughulikia ipasavyo wale wote watakaobainika kufanya vitendo vya ukatili kwa makundi mbalimbali katika jamii hususani kwa wazee”. ameongeza Waziri Dkt. Gwajima.

Maadhimisho ya Kupinga ukatili Dhidi ya Wazee mwaka huu yatafanyika katika ngazi ya Mikoa kote nchini na Kaulimbiu ni “Wazee Wanastahili Heshima na Usikivu Wetu”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Mkoa wa Dodoma Peter Mpolo ameipongeza serikali kwa kuendelea kuwajali wazee kwa kuwapatia huduma mbalimbali ambazo zinawafanya waendelee na shughuli mbalimbali.

” Kila mzee anapaswa kurudi kwenye jukumu la kutunza watoto kwa kuwafundisha mila na desturi za kitanzania.”amesema Mzee Mpolo

MATUKIO YA MHE. WAZIRI MKUU BUNGENI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),  Alphayo Kidata (kushoto) na Mkurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) Sabasaba Muyanja kwenye viwanja wa vya Bunge jijini Dodoma,  Juni 7, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata (kushoto)  na mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga  kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 7, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti Maalum, Janet Masaburi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 7, 2023. Kushoto ni Mbunge wa Nsimbo, Anna Lupembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Viti Maalum, Janet Masaburi kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 7, 2023. Kushoto ni Mbunge wa Nsimbo, Anna Lupembe. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na walimu kutoka jimbo la Kilombero kwemye viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Juni 7, 2023. Kulia kwake ni Mbunge wa Kilombero, Abubakar Asenga. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube