Mshambuliaji Emmanuel Okwi ana nafasi ya kuwa katika kikosi cha Simba kitakachoivaa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara, kesho.
Simba itakuwa mwenyeji wa Azam FC katika mechi hiyo huku ikiwa na matumaini ya kumtumia Okwi ambaye ni kinara wa mabao Ligi Kuu Bara kwa sasa akiwa na mabao 12.
Okwi aliumia baada ya kupigwa kwa makusudi na beki wa Ruvu Shooting katika mechi iliyopita na kulazimika kutolewa nje kwa ajili ya matibabu na hakurejea kwa kuwa alikuwa akipata shida.
Lakini Okwi ameonekana kupata nafuu haraka na aliungana na wenzake kambini tokea juzi na kuungana nao katika mazoezi.
Raia huyo wa Uganda aliikosa mechi ya kwanza kati ya Simba dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Azam Complex na kumalizika kwa sare ya bila bao.
No comments:
Post a Comment