BOHARI ya Dawa (MSD) imeendelea kukidhi viwango vya ubora vya kimataifa katika mfumo wa ununuzi, utunzaji na usambazaji dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara (Supply Chain Management) na kupata Ithibati ya Kimataifa ya ubora ya daraja la juu inayojulikana kama ISO 9001:2015 ambayo itadumu kwa miaka mitatu (2018 - 2020).
Hatua hiyo imekuja baada ya ukaguzi wa ubora wa huduma zinazotolewa na MSD uliofanywa na kampuni ya Kimataifa ya ACM LIMITED mweziAgosti 2017, na kudhihirisha kuwa huduma zake zinafuata miongozoya ya juu ya kimataifa katika utoaji wa huduma za mnyororo wa ugavi.
Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Bwana Laurean Rugambwa Bwanakunu amesema kuwa hatua hiyo ya kupata ithibati ya juu ya Ubora ya Kimataifa imethibitisha umahiri wa MSD na imeongeza chachu ya utendaji, ubunifu na kuboresha masuala yote yanayo husiana na mnyororo wa ugavi ilikuwapa wananchi huduma bora, zenye viwango, bei nafuu na kuwafikishia kwa wakati.
Bwanakunu ameongeza kuwa Ithibati hiyo inaonesha dhahiri ubora wa mfumo wa ugaviwa MSD kwa wateja na wananchi kwa ujumla, na kueleza kuwa huduma za MSD zinaendelea kuboreshwa zaidi kwani taasisi hiyo iko katika kipindi cha maboresho ya kiutendaji kupitia mpango mkakati wake wamwaka 2017 - 2020.
Mara ya kwanza MSD ilipataIthibatiya kimataifa mwaka 2013 (ISO 9001:2008) baada ya kukidhi matakwa ya ubora kwa huduma zake za Ununuzi, tunzaji na Usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na iliweza kuishikilia ithibati hiyo kwa miaka yote bila kunyanganywa, kutokana na kuonekana kuendelea kukidhi viwango vya ubora kila walipokaguliwa.
MSD imekuwa miongoni mwa taasisi za kwanza nchinikupataithibatiyauborayakiwango cha ISO 9001:2015 kutokakiwango cha ISO 9001:2008 na imethibitisha umahiri wa utendaji wake.
No comments:
Post a Comment