Marehemu Joyce Mmasi enzi za uhai wake.
Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mwanahabari Joyce wakati ukiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam leo kwa ibada ya kuuaga kabla ya kuelekea mkoani Kilimanjaro kwa mazishi.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wanahabari wakiwa kwenye ibada hiyo.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye ibada hiyo.
Mchungaji Kulwa wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, akiongoza ibada hiyo.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando akizungumza kwenye ibada hiyo.
Mbunge wa Viti Maalumu, Suzan Lyimo akizungumza. Lyimo na marehemu Mmasi wanatoka kijiji kimoja.
Familia ya marehemu ikiwa katika ibada hiyo. Kulia ni mtoto wa kwanza wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella.
Mume wa marehemu Joyce Mmasi, Andrew Kamugisha akizungumza kwenye ibada hiyo.
Rafiki wa marehemu Mashaka Mgeta, akizungumzia maisha ya Joyce na jinsi alivyomfahamu.
Waandishi wa habari wanawake wanaounda kikundi cha Wawata wakitoa neno katika ibada hiyo.
Mwanahabari Hellen Mwango akisaidiwa baada ya kupoteza fahamu.
Mtoto mkubwa wa marehemu, Lawrence Nicky Mayella, akisoma Historia ya mama yake.
Mwenyekiti wa kamati ya mazishi, Thomson, akizungumza katika ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa katika foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu.
Foleni ya kwenda kutoa heshima za mwisho.
VILIO Majonzi na simanzi vilitawala wakati wa ibada ya kuuaga mwili wa mwanahabari nguri Joyce Mmasi iliyofanyika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Katika ibada hiyo mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam, wanahabari na wadau wengine walijitokeza katika viwanja hivyo kwa ajili ya kumuaga mpendwa wao Joyce Mmasi ambaye alikuwa akifanyia kazi katika gazeti la Mwananchi.
Mchungaji Kulwa kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), ambaye aliongoza ibada hiyo aliwaambia watu waliokuwepo kwenye ibada hiyo kuwa wanapaswa kujitayarisha wakati wote kwani hawajui ni lini wataondoka hapa duniani.
"Mwenzetu Joyce ametutangulia tulikuwa naye pamoja lakini wewe uliye hai leo hii umejiandaeje katika maisha ya kiroho?" alisema Mchungajia Kulwa.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Kigamboni, Rachel Mhando alisema kifo cha Mmasi kimemshitua kila mtu na wanahabari wamepata pigo la kumpoteza mwenzao.
Mhando alihimiza kudumisha upendo kwa watu wote pamoja na wanahabari.
Katika ibada hiyo makundi mbalimbali yalijitokeza kutoa salamu za rambirambi na kuhudhuriwa na viongozi wa dini, siasa, serikali na wadau wengine.
Mwili wa marehemu Joyce umesafirishwa kwenda mkoani Kilimanjaro nyumbani kwao kwa mazishi.
Marehemu ameacha mume na watoto watatu, Mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu.
No comments:
Post a Comment