Vijana kutoka Zanzibar na Tanzania Bara wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuzifanyia kazi kwa ajili ya kulitetea taifa maendeleo. Mkutano huo ulifanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark jijini Dar es Salaam.
Majadiliano yakiendelea.
Msisitizo katika majadiliano hayo.
Fursa mbalimbali zikiandikwa katika makundi.
Picha ya pamoja ya vijana hao.
VIJANA wa Zanzibar na Tanzania Bara wamekutana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia fursa zilizopo nchini ili kuliletea taifa maendeleo.
Katika mkutano huo uliofanyika mwishoni mwa wiki Makao Makuu ya Kampuni ya Trumark vijana hao wapatao 14 kwa niaba ya wenzao walijadiliana mambo mbalimbali na kuangalia fursa za maendeleo zilizopo nchini.
Kwa ujumla fursa zilizokuwa zimeangaliwa katika maeneo mbalimbali na wazo hilo limekuja baada ya baadhi yao kutembea nchi nzima Tanzania Visiwani na Tanzania Bara na kuziona hivyo wakaona ni vema kuunganisha nguvu ya pamoja kwa kuwashirikisha wenzao na kuona waanzie wapi.
"Tumetembea nchi nzima na kuona fursa mbalimbali tukaona ni vizuri vijana wa Zanzibar na Tanzania Bara tukutane tujadiliane na tuone ni fursa zipi tuzifanyie kazi kwa manufaa yetu kama vijana na taifa kwa ujumla" alisema mmoja wa vijana hao ambaye hakupenda kuingia kiundani zaidi kwa kuwa mchakato wa jambo hilo ndio kwanza upo jikoni.
Alisema hivi sasa vijana wasitegemee kuajiriwa badala yake waziangalie fursa zilizopo nchini na hizo ndizo zitakazo waondoa katika mawazo ya kutegemea kuajiriwa.
Alisema kuna fursa za kuanzisha viwanda vidogo vidogo, ufugaji, ufundi mbalimbali, kilimo na mambo mengine hivyo ni vema vijana wakaangalia huko zaidi.
Alisema wamekutana katika mkutano huo kuangalia fursa hizo na wapi pa kuanzia na mchakato huo ukikamilika wataweka mambo hadharani na kukamilisha mambo yote lengo likiwa ni kuwaunganisha vijana wa nchi nzima.
=
No comments:
Post a Comment