Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika tukio hilo
Baadhi ya watoto kutoka katika vituo vya kulea watoto Yatima ambao waliandaliwa futari hiyo maalum wakiwa katika tukio hilo
Mmoja wa wasomaji wa dini ya kiislamu akiendelea na dua
Wageni waalikwa wakiwa katika shughulo hiyo
Wadau
Dua zikiendelea
Mkuu wa Mkoa wa Kinondoni, Mh. Ali Hapi akipata futari hiyo
Mwanadada Mboni Masimba akizungumza machache kuhusiana na tukio hilo
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Mh. Makonda
Mkuu wa Mkoa akiagana na wadau katika tukio hilo
Wadau waliojitokeza kumuunga mkono Mwanadada Mboni Masimba
Kipindi
cha The Mboni Show, chini ya Mtangazaji wake, Mboni Masimba ambacho
kinachorushwa kupitia televisheni ya Taifa ya TBC, Jioni ya jana ya
Juni 29.2016 wameweza kufuturisha wageni Watoto Yatima 268 kutoka katika
baadhi ya vituo vya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwafariji na
kuwasaidia kama ilivyo kwa desturi ya waandaaji wa kipindi hicho huku
Mama mgeni rasmi akiwa Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu.
Akizungumza
katika tukio hilo mara baada ya kufuturisha Watoto hao pamoja na wageni
mbalimbali Mwanadada Mboni ameeleza kuwa, wamekuwa wakifanya hivyo mara
kwa mara hii ni kutokana na kurudisha fadhila kwa jamii kwa kidogo
kinachopatikana hivyo amewaomba wadau wengine kujitokeza kufanya jambo
kama hilo kila inapohitajika kwa jamii.
Kwa
upande wake, Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amepongeza tukio hilo la
Mwanadad Mboni Masimba kwani ni la kuigwa hivyo ni lazima jamii imuunge
mkono kwa kujilea kwake.
"Nakupongeza
Mboni na timu yako kwa kuwakumbuka watoto hawa. Tukio kama hili
kuliandaa linahitaji gharama na kujitolea haswa. Tupo pamoja nawe na
juhudi zako tunaziona nakupongeza sana." alibainisha Makamu wa Rais Mama
Samia.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda,
alimpongeza Mboni Masimba kwa shughuli hiyo kwani inasadia katika
kukumbuka jamii hasa watoto hao ambao wengi wao wanalelewa katika vituo
vya Yatima.
Katika
tukio hilo lililofanyika katika ukumbi wa Karimjee uliopo Posta jijni
Dar es Salaam mbali na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh. Paul Makonda,
Pia viongozi wengine kadhaa walijumuika akiwemo Mkuu wa Mkoa wa
Kinondoni, Mh Ali Hapi na viongozi wa dini Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhadi Mussa Salum pamoja na Kaimu Mufti wa Tanzania
aliyemwakilisha Mufti Mkuu pamoja na Mabalozi akiwemo Balozi wa INDIA.
Pia
wadau wa kipindi hicho cha The Mboni Show, watu maarufu, Wasanii,
Wanahabari na wadau wengine wakiwemo wadhamini waliofanikisha shughuli
hiyo.
No comments:
Post a Comment