Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye leo Juni 26.2016
amezindua msimu wa sita (6) wa mashindano ya soka ya vijana chini ya
umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars, tukio lililofanyika Makao makuu
ya kampuni hiyo ya mtandao wa simu jijini Dar es Salaam.
Katika
tukio hilo, mbali na Nape, pia Rais wa TFF, Jamali Malinzi naye
aliungana pamoja na viongozi wengine na wadau wa soka. Awali Waziri Nape
alipatiwa taarifa mbalimbali namna kampuni hiyo ilivyojikita katika
kuinua vipaji vya vijana na michezo kwa ujumla ambapo kwa vijana waliopo
sasa ambao ni chimbuko la program hiyo wameanza kua lulu kwa taifa hasa
uwezo wao wa kisoka.
Akizungumza katrika tukio hilo Nape alieleza: “Program
za soka za vijana ndiyo muhimili wa maendeleo ya soka popote pale
duniani. Ndio maana nasisitiza umuhimu wa mashindano ya Airtel Rising
Stars ambayo matunda yakek yameonnekana Dhahiri katika kipindi cha miaka
mitano iliyopita” alisema Nape.
Nape
pia aliipongeza Airtel kwa progamu hiyo kwani miongoni mwa wachezaji wa
timu ya Taifa ya Vijana wa umri wa chini ya miaka 17, wanatoka katika
program hiyo ya Airtel Rising Stars hivyo amewataka viongozi
wanaosimamia soka hapa nchini kuisimamia vizuri program hiyo ya Airtel.
Alisema
kushirikisha vijana hasa Wasichana na Wavulana ni jambo bora sana
katika kukuza michezo hapa nchini hivyo ameiunga mkono na kuwapongeza
kwani inasaidia Taifa katika kufikia malengo yake.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bi.
Beatrice Singano amemuakikishia Waziri Nape kuwa Airtel Tanzania ina
nia thabiti ya kuendeleza kudhamini michuano hiyo ambayo imesaidia
kuzalisha wachezaji wengi chipukizi hivyo kuendeleza mchezo huo maarufu
hapa nchini.
Aidha,
amebainisha kuwa,program hiyo hapa nchini inafanyika chini ya mwamvuli
wa kampeni ya Airtel FURSA iliyozinduliwa mwaka jana kwa lengo la
kuwahamasisha vijana kutumia fursa kupitia uwezo wa vipaji vyao hasa
mpira wa miguu kuwa chanzo cha kipato chao.
“Kwa
kuwa na wateja wengi nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar. Tunatakiwa
kuendelea kutoa sehemu ya faida yetu kwa jamii kupitia mchezo wa mpira
wa miguu ambayo ni maarufu hapa kwetu kuliko mchezo mwingine Hii ni njia
ya kuwashukuru wateja wetu kwa kutuunga mkono” alieleza Bi Beatrice
Singano.
Kwa
upande wake, Rais wa TFF, Jamali Malinzi alipongeza program hiyo ya
Airtel Rising Stars kwani imeleta mapinduzi na kubadilisha kabisa sura
ya mchezo wa soka hapa nchini.
Airtel
Rising Stars mwaka huu itashirikisha mikoa ya Mwanza, Morogoro, Mbeya,
Temeke, Ilala (Wavulana) huku kwa mikoa itakayoshirikisha Wasichana ni
pamoja na Ilala, Kinondoni, Temeke, Arusha, Lindi na Zanzibar.
Naye
Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando ilieleza kuwa,
Airtel itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ikiwemo
kupitia programu zake mbalimbali ikiwemo hiyo ya soka.
“Tunajivunia
mafanikio ya Airtel Rising Stars ambayo yametoa mchango mkubwa katika
maendeleo ya mchezo wa soka nchini. Wachazeji kutoka programu hii ya
Airtel Rising Stars hivi sasa wako katika timu za daraja la kwanza, ligi
kuu Tanzania Bara na timu za taifa hasa ile ya U-20 na timu ya wanawake
Twiga Stars,” alibainisha Mmbando mara baada ya uzinduzi huo.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipatiwa maelekezo
ya moja ya vijana walioiburiwa na programu hyo ya Airtel Rising Stars
ambaye pia wapo katika timu ya Taifa ya Vijana walio chini ya umri wa
miaka 17.
Rais wa TFF, Jamali Malinzi akizungumza katika tukio hilo
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano akizungumza katika uzinduzi huo..
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza katika uzinduzi huo
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akijiandaa kupiga
mpira kuelekea golini kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano hiyo..
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipiga mpira
kuelekea golini kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano hiyo
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akifunga bao safi
katika ufunguzi huo kuashiria uzinduzi rasmi wa michuano hiyo
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye katikati akipiga picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo. Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipata picha ya
pamoja na maafisa wa Airtel Tanzania pamoja na viongozi wengine wa soka
hapa nchini.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akipata picha ya
pamoja na maafisa wa Airtel Tanzania pamoja na viongozi wengine wa soka
hapa nchini. wakati wa tukio hilo la Airtel Rising Stars 2016. ( Picha
zote na Andrew Chale,modewjiblog).
No comments:
Post a Comment