BREAKING

Monday 27 June 2016

TP MAZEMBE WASEMA YANGA WATASIMULIA KESHO....


Kamisaa wa mchezo kati ya Yanga na TP Mazembe wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika, Celestine Ntangungira kutoka Rwanda amesema kuwa ni mashabiki elfu  40,000 wanapaswa kuingia UWANJA wa Taifa, Dar es Salaam, baada ya Yanga kutangaza mashbiki hao kuingia bure katika mchezo wa kesho.

Uwanja wa Taifa una uwezo wa kuchukua mashabiki waliokaa elfu 60,000, lakini kesho utafungwa wakati wa mchezo wa Yanga na TP Mazembe ya DRC baada ya mashabiki hao 40 elfu kuingia Uwanjani.

Agizo hilo la kamisaa limesomwa na msemaji wa Yanga Jerry Muro alipozungumza na Waandishi wa Habari akisema kwamba mashabiki watakaobahatika kuingia uwanjani ni wale ambao watafika mapema na kwamba Yanga itatekeleza agizo la Kamisaa la kufunga mageti yote wakitimia watu elfu 40,000.

Amesema kwamba kutakuwa na ulinzi  wa askari Polisi kesho kuhakikisha kwamba hazitokei vurugu za aina yoyote na watu kwani watakuwa wakiepuka rungu kutoka CAF iwapo fujo zitatokea.

Tayari wapinzani wa Yanga Mazembe waliwasili usiku wa jana ikiwa na kikosi cha wachezaji 18 huku wakiwa na mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu wachezaji wengine wakiwa ni Robert Kidiaba, Sylvain Gbohou, Issama Mpeko, Joel Kimwaki,  Christian Koume,Jean Kasusula, Salif Coullbaly, Merveille Bope,Jose Badibake, Kissi Boateng, Roger Assale, Rainford Kalaba, Deo Kanda, Adama Traore, Chriastian Luyindama, Nathan Sinkala na Joas Sakuwaha.

Timu hizo zinakutana huku Yanga ikiwa na kumbu kumbu mbaya ya kufungwa bao 1-0 na  MO Bejaia ya Algeria wakati Mazembe ilishinda 3-1 nyumbani dhidi ya Medeama ya Ghana  Jumapili iliyopita.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube