Afisa Mipango wa UNFPA, hapa nchini, Bi.Felista Bwana akitoa maelezo mafupi juu ya wakunga hapa nchini
Chama
cha Wakunga Tanzania (Tanzania Midwives Association-TAMA) imefanya
mkutano maalum wa kuhamasisha waandishi wa Habari kuhusu kazi za wakunga
katika kuelekea siku ya Wakunga Dunia ifikapo hapo Mei 5 mwaka huu.
Katika
mkutano huo uliofanyika jana Aprili 28, TAMA ilibainisha kuwa,
wanahabari wengi wamekuwa wakichanganya habari za wakunga wataalam
ambao wapo chini ya Chama hicho na wale wakunga wa jadi ambao hawana
taalum pamoja na kiapo cha kufanya kazi hiyo kitu ambacho kinaleta
usumbufu mkubwa kwa jamii.
Mratibu
wa TAMA, Bi. Martha Rimoy katika mkutano huo, ameeleza kuwa, shughuli
za Wakunga wataalam ni wale tu ambao wamesomea taaluma hiyo pamoja na
kula kiapo katika kumsaidia Mama na Mtoto na na huyo ndiyo anaitwa
Mkunga na si wale ambao hawajapata mafunzo wala kula kiapo.
Aidha,
aliomba wanahabari na vyombo vya habari kuzipatia nafasi/Kipaumbele
habari za Wakunga kwani zitaondoa woga kwa jamii iliyojenga Imani potofu
kwa wakunga.
“Jamii
imekuwa ikijenga Imani potofu namna ya Wakunga buka kujua mkunga huyo
ni yupi. Tunaomba ifahamike Mkunga ni yule aliyepata mafunzo yake
kitaalam na pia kula kiapo pamoja na kusajiliwa na taasisi husika kama
ilivyo taratibu za Nchi.
Tuondoe
Imani zingine kwa Wakunga pia tunawaomba wanahabari kuweza kutoa elumu
ya kutosha kuhusiana na mambo ya Wakunga hasa wakunga wataalam ambao
wamepatiwa mafunzo yote ya kuhakikisha wanamuokoa Mama na mtoto wakati
wa uzazi” alieleza Bi. Martha Rimoy.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TAMA, Dkt Sebalda Reshabari ambaye alikuwa
mgeni rasmi katika mkutano huo, ameeleza kuwa, Wakunga wataalam wanao
wajibu
wa
kumsaidia Mwanamke na mtoto katika kukabiliana na vifo vitokanavyo na
Masuala ya Uzazi vinavyozidi kuwatesa akina mama wengi, hasa inapokuja
wakati wa tendo la kujifungua.
Aidha,
Dkt. Sebalda amebainisha kuwa, pamoja na Changamoto mbalimbali, vifo
vya watoto walio chini ya umri wa miaka 5, imepungua kwa asilimia 81,
huku akitaka muendelezo wa elimu utolewe kwa Jamii.
Kwa
upande wake, Afisa Mipango wa Afya ya Mama na Uzazi wa Shirika la Idadi
ya Watu Duniani (UNFPA)nchini, Bi. Felista Bwana ameelezea kuwa, upo
umuhimu wa Mkunga mtalaam katika kuokoa Uhai wa Mama na mtoto kwani bila
wao Dunia ingekuwa kwenye matatizo makubwa.
Siku
ya Ukunga Duniani Inatarajiwa kuadhimishwa katika Viwanja vya Mnazi
mmoja Jijini Dar es Salaam, Mei 5 mwaka huu huku ikibeba ujumbe wa kauli
mbinu ya “Wanawake na Watoto wachanga ni muhimili wa Ukunga”.
Aidha,
mkutano huo ulieza changamoto wanazokabiliana nazo wakunga ni nyingi
hivyo wameimba Serikali kuangalia namna ya kukabiliana nayo ili kila
Mkunga kufanya kazi yake kwa uhuru na haki kwa dhama za sasa huku
wakiomba jamii kuondoa dhana potofu dhidi yao pindi wawaonapo katika
vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali zote.
Mkutano
huo maalum wa TAMA, ulihusisha wanahabari mbalimbali kutoka katika
vyombo vya Habari nchini ikiemo, Magazeti, Radio, Televisheni na
magazeti ya mtandaoni.
No comments:
Post a Comment