BREAKING

Monday, 4 April 2016

WAZIRI MWAKYEMBE AISHUKURU KAMPUNI YA KAMAL STEEL KWA KUTOA VIUNGO BANDIA KWA WALEMAVU

1
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta wakati wa hafla ilyofanywa na kampuni hiyo ya Kamal Steel Ltd kiwandani hapo wakati wa utoaji wa msaada wa viungo bandia, kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 80, hafla hiyo ya kukabidhi msaada huo imefanyika hivi karibuni jijini Dar es salaam.(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-DAR ES SALAAM)
2
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akishukuru kampuni hiyo kwa msaada ilioutoa kwa watanzania hao wenye ulemavu wa miguu ambapo yeye ndiye aliyewakabidhi kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta.
3
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimvisha mguu wa bandia Bw. Siaga Raphael Kiboko mara baada ya kukabidhiwa kutoka kampuni ya Kamal Steel ya jijini Dar es salaam kushoto ni Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw. Gagan Gupta.
4
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na Bw. Siaga Raphael Kiboko kabla ya kumkabidhi msaada wake wa viungo bandia vya mguu.
5
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Gagan Gupta ambaye ni mwenyekiti wa kampuni ya Kalam Steel tayari kwa ajili ya kukabidhi msaada huo.
6
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akifurahia jambo na Bw. Siaga Raphael Kiboko mara baada ya kumvisha mguu wake huku Mwenyekiti wa kampuni ya Kamal Steel Bw. Gagan Gupta pamoja na viongozi wengine wa kampuni hiyo wakishuhudia.
7
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiongozana na Bw. Joshua Mwamunyange mara baada ya kumvisha mguu wakena kuanza kujaribu kutembea.
8
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimbidhi Bi Fatuma mguu wake wa bandia ikiwa ni msaada kutoka kampuni ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel ya jijini Dar es salaam.
9
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wa kampuni ya Kamal Steel na baadhi ya walemavu waliokabidhiwa msaada huo.
10
Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe akimsikiliza Mwenyekiti wa kampuni ya Kamal Steel Bw. Gagan Gupta.mara baada ya kukabidhi misaada hiyo katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta na wakuu wengine wa vitengo kutoka kampuni hiyo.
.............................................................................................................
KAMPUNI ya kutengeneza chuma ya Kamal Steel Ltd, imetoa msaada wa viungo bandia, kwa watu wenye ulemavu 16, vyenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 80.
Akifunga kambi ya kutoa viungo bandia hivyo jijini Dar es Salaam sambamba na kukabidhi vifaa hivyo, Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema, serikali itaendelea kuwawezesha watu wenye ulemavu nchini ili waweze kukabiliana na changamoto zinazowazunguka ikiwa ni pamoja na kuwapatia vifaa bandia.
Alisema, suala la ulemevu linagusa maisha ya kila mwanadamu na kwamba mtu yoyote anaweza kufikwa na tatizo hilo.
Alibainisha, viungo bandia vinauzwa kwa ghalama kubwa ambayo watu wengi wenye ulemavu hawawezi kumudu kununua hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wake itaendelea kutoa msaada wa vifaa hivyo.
“Jamii iamini kuwa wote ni walemavu watarajiwa. Kupoteza kiungo kimoja cha mwili ni changamoto kubwa. Tunaishukuru kampuni ya Kamal Steel kwa kutoa misaada hii muhimu ambayo tunaamini kuwa inasaidia kupunguza madhira ya ulemavu,”alisema Dk. Mwakyembe ambaye kupitia msaada huo ameweza kuwasaidia watu wenye ulemavu wanne kutoka jimbo lake la Kyela mkoani Mbeya.
Mwenyekiti wa makampuni ya Kama Group , Gagan Gupta, alisema,kampuni yake haijatoa viungo bandia hivyo kama msaada, bali kama wajibu wake kwajamii.
“Tunaamini kwamba, viungo hivi bandia vitawawezesha kumudu kutembea, kufanya kazi mbalimbali zitakazo waletea kipato,”alisema Gupta.
Katika hatua nyingine, Gupta aliahidi kumuajiri mmoja wawatu hao wenye ulemavu mwenye taaluma ya ufundi mitambo, Siaga Raphael ambapo alisema ajira yake itaanza leo.
“Huyu atafundishwa ufundi wa kutengeneza vifaa mbalimbali hasa vya watu wenye ulemavu hapa, ili aweze kusaidia kuwafundisha watu wenye ulemavu wengine.Mradi anataaluma hiyo ataanza kazi kesho asubuhi (leo asubuhi),”alisema Gupta.
Mkurugenzi Mkuu wa Kamal Steel, Sameer Gupta, alisema, kampuni hiyo imekuwa mstari wa mbele katika kusaidia viungo hivyo bandia kwa watu wenye ulemavu ambapo mpaka sasa imesaidia watu 200.
“Tutaendelea kuwasaidia kila mara ili tuweze kuisaidiana na serikali yetu kuwaondolea changamoto wenzetu hawa. Tunaamini wakipewa viungo hivi bandia wanaweza kushiriki shughuli mbalimbali muhimu zitakazowaingizia kipato,”alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake walio pokea msaada huo, Siaga Raphael, aliipongeza kampuni hiyo kwa masaada wa vifaa hivyo na kuitaka serikali kuwa kumbuka watu wenye ulemavu kwa kuwasaidia pia kuwapa taaluma ya ufundi itakazowawezesha kujimudu kimaisha.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube