Kapteni mpya wa timu ya Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mjini, Mh. Sixtus Mapunda akitoa maelezo kwa kikosi hicho cha Bunge muda mfupi kabla ya kuanza kwa mchezo wao huo dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi mchezo uliochezwa katika uwanja wa Amaan,
Waziri wa Kilimo, Mfugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba akipata picha ya pamoja na mmoja wa wachezaji wa Baraza la Wawakilishi
Mchezaji wa timu ya Baraza la Wawakilishi ambaye pia analiwakilisha Jimbo la Tunguu, Mh. Simai Mohamed Said akijadiliana jambo na ,Mwakilishi wa Rahaleo (CCM), Mh. Nasasor Salum Al Jazeera wakati wa mchezo huo maalum dhidi ya timu ya Bunge.
Timu zikiingia uwanjani
Wachezaji wakisalimiana kabla ya mechi
Kikosi cha timu ya Bunge kabla ya mchezo huo kuanza..
Kikosi cha timu ya Bunge kabla ya mchezo huo kuanza..
Kikosi cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar kabla ya mchezo huo kuanza...
Mchezo ukiendelea katika uwanja huo wa Amaan
Mashabiki wakifuatilia mchezo huo
Viongozi wakiwa katikajukwaa maalum la wageni waalikwa.
Kikosi cha Bunge kikitoka katika vyumba vya kupumzikia kuendelea na kipindi cha pili
Viongozi wa timu wakihamasisha timu yao hiyo ya Bunge...
Viongozi wa timu wakiwa hawaamini baada ya Baraza la Wawakilishi kusawazisha bao hilo na kuwa 1-1...
Kikosi cha Baraza la Wawakilishi waliokuwa wapo mapumziko wakifurahia baada ya kusawazisha bao hilo
Kikosi cha Bunge mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo
Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid akizungumza baada ya mchezo huo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Mazingira na Muungano Mh. January Makamba akizungumza mara baada ya mchezo huo
Kikosi cha Bunge kikiomba dua mara baaa ya mchezo huo...
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge (wa pili aliyesimama nyuma) akipata picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliojitokeza katika mchezo huo wa kuimalisha Muungano.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Mwenyekiti wa timu ya Bunge na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh. Mwigulu Nchemba wakipata picha pamoja na Vijana wa Visiwani Zanzibar mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa Bunge na Baraza la Wawakilishi ambao uliisha kwa sare ya bao 1-1.
Timu
ya Mpira wa miguu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania, Bunge
Sports Club usiku wa leo Aprili 26.2016 imeweza kutoka sare ya bao 1-1,
dhidi ya timu ya Baraza la Wawakilishi la Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, mchezo uliochezwa uwanja wa Amaan, Unguja na kushuhudiwa na
watu mbalimbali.
Mchezo
huo wa aina yake na wa kipekee kwa kikosi hicho cha Bunge Sports Club
kiliweza kucheza kandanda safi na la kuvutia wakati wote ambapo
waliweza kupata bao lao la kuongoza ndani ya dakika 22 ya mchezo katika
kipindi cha kwanza bao safi lililofungwa kwa kushuti la nje ya 18 na
kuwaacha Wachezaji wa Baraza la Wawakilishi wasijue la kufanya.
Bao
hilo la Bunge Sports Club ambalo lilikuwa la ushindi lilidumu hadi
kipindi cha pili ambapo katika dakika ya 67, Timu ya Baraza la
Wawakilishi ilifanikiwa kusawazisha bao hilo na kufanya mchezo kuwa 1-1.
Bao hilo lilipachikwa kutokana na hali ya hewa kuwa mbaya hasa mvua
kiasi cha kuwapoteza vibaya wachezaji wa timu ya Bunge ambao walicheza
katika mazingira magumu sana.
Mara
baada ya mchezo huo kumalizika, Kocha wa timu hiyo ambaye pia Mbunge
Jimbo la Kilolo mkoani Iringa, Mh. Venance Mwamoto alibainisha kuwa
kikosi chake kilicheza soka safi na wataendelea kukiimalisha kwani
wanaamini mpira ni ajira ambapo pia alieleza kuwa bila washindani wao
‘kuwachomekea’ wanahakika wangefanya vizuri zaidi n ahata kuibuka na
mabao mengi.
Kwa
upande wake, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zubeir Ali Maulid
alizipongeza timu zote mbili na kuzitaka kuendelea kudumisha michezo na
suala la Muungano kwa ujumla kwani wanahakika kupitia michezo suala hilo
litaenziwa kwa miaka yote.
Naye
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu Wa Rais Mazingira na Muungano Mh.
January Makamba alibainisha kuwa wataendelea kuulinda Muungano huku
akiwataka Watanzania kuishi kwa misingi ya Amani na utulivu kwa kipindi
chote ambapo pia alieleza kuwa suala la Michezo litaendelea kuwapo
ilikuongeza mshikamano kwa watu wote.
No comments:
Post a Comment