Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akizungumza kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) juu ya droo hiyo pamoja na ofa mbalimbali zinazoendelea kutolewa kwa wateja wa DSTV
Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo akichanganya droo hiyo kwa njia ya kielektoniki kupitia kompyuta. wengine wanaoshuhudia ni maafisa wa MultiChoice Tanzania. Kulia ni mwakilishi kutoka Bahati Nasibu ya Kubahatisha, Bw. Mrisho Millao.
Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akihakiki moja ya majina ambayo yameingia kwenye droo ya ushindi kwa wateja wa DSTV
Droo hiyo ikiendelea
Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo akionyesha majina ya washindi kwenye 'sreen' kubwa (Haipo pichani) wakati wa tukio hilo
Droo hiyo ya JISHINDIE NA DSTV ikienndelea huku maafisa wa MultiChoice Tanzania na Mwakilishi wa Mchezo wa kubahatisha Tanzania pamoja na wanahabari wakishuhudia tukio hilo mapema leo Aprili 19.2016, Makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es Salaam.
Kampuni
ya MultiChoice Tanzania inayosambaza vifaa vya ving’amuzi vya DSTV hapa
nchini mapema leo Aprili 19.2016 imechezesha droo maalum na kuwapata
washindi wa “JISHINDIE NA DSTV” katika tukio lililofanyika Makao makuu
ya kampuni hiyo Oysterbay, barabara ya Ali Hasan Mwinyi, Jijini Dar es
Salaam huku ikishuhudiwa na mwakilishi kutoka bodi ya michezo ya
kubahatisha nchini.
Awali
katika droo hiyo, Meneja wa Huduma kwa wateja, Bi Hilda Nakajumo
alieleza kuwa, droo hiyo ilianza tokea mwezi wa kwanza ambapo wateja
walitakiwa kuwa na malipo kwenye ving’amuzi vyao vya DSTV bila kukatika
kuanzia hiyo Januari hadi mwezi Machi.
Wateja
ambao hawajakatiwa ving’amuzi vyao katika promosheni hiyo ya JISHINDIE
NA DSTV, waliotangazwa leo ambaoo ni wateja waliojiunga mwezi wa kwanza
na kuweza kulipia DSTV zao bila kukatiwa matangazo kwa muda wa miezi
mitatu wameweza kujishindia zawadi ya safari ya kwenda Zanzibar wakiwa
wao na familia zao.
“Washindi
wawili ambao kila mmoja atapata nafasi ya kupelekwa Zanzibar na kukaa
huko kwa siku mbili katika hoteli huku akilipiwa kila kitu kuanzia
usafiri, malazi, chakula yeye na familia yake ikiwemo baba, mama na
watoto wawili. Washini hao ni Mwelly Nyakusaima ambaye ni mkazi wa
Igoma-Mwanza na mshindi mwingine ni Evarist Ndambo mkazi wa Tabataa
Jijini Dar es Salaam.” Alisema Bi. Hilda Nakajumo.
Aidha,
alibainisha kuwa, washindi wengine waliojishindia droo hiyo ambao ni wa
kipengele cha pili ni wale wateja ambao tayari walishajiunga na DSTV
huku wakitakiwa wasikatiwe malipo yao kuanzia mwezi wa kwanza hadi wa
tatu.
Ambapo
wateja 50 wamejishindia DSTV EXPLORA Decoders huku wateja 90 wao
wakibahatika kupata kuunganishwa malipo ya bure ya mwezi ikiwemo ya
mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita na miezi 12 bure.
Aidha,
washindi hao wote walioshinda MultiChoice ilibainisha kuwa, watapigiwa
simu na kuelekezwa namna ya kuchukua zawadi zao hizo kuanzia sasa kwa
muda hadi June mwaka huu.
Kwa
upande wake, Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu
aliwakumbusha wateja wa DSTV kuendelea kulipia malipo ya ving’amuzi vyao
huku wakitoa ofa mbalimbali sambamba na vipindi vizuri ikiwemo vya
uhondo wa soka la kimataifa, filamu na muziki..
No comments:
Post a Comment