BREAKING

Tuesday, 1 October 2019

TANZANIA YAMIMINIWA SIFA KEDE KEDE TAMASHA LA JAMAFEST....

Wachezaji ngoma wa Kinyarwanda wamesimamisha kwa muda shughuli nyingine zilizokuwa zikiendelea kwenye maonyesho ya Tamasha la Utamaduni la Afrika Mashariki (JAMAFEST) jijini Dar es Salaam nchini Tanzania baada ya kupanda jukwaani. Watazamaji mbalimbali kwenye maonyesho wameacha shughuli zao kwa muda na kusogea kushuhudia ngoma hiyo iliyoshirikisha wanaume na wanawake. Wadada wa Kinyarwanda walikuwa kivutio zaidi huku baadhi ya watazamaji wakiwashangilia na wengine wakionyesha kuwakubali kwa kuchukua video kwa simu na wengine wakijadiliana kuhusu urembo wa wanawake wa Kinyarwanda. “Huwa nashangaa hawa kina dada kutoka nchini Rwanda ni warembo jamani “Halafu hawatumii mavitu vitu lakini kama wananyumbulika.” “Nikiwaona kwenye picha huwa nahisi wamejiumba wenyewe jinsi wanavyovutia kama wamezaliwa na mama mmoja..” walisikia vijana wawili waliokuwa wakizungumza uwanja hapo wakati ngoma hiyo ikiendelea kutumbuiza Walisikika baadhi ya watu uwanjani hapo kila mmoja akisema lake kuhusu urembo wa wanawake hao ambao umekuwa gumzo.

VIFAA VYA UJENZI WA MELI MWANZA VYAWASILI MWANZA...







 Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Atashasta Nditye wa tatu kutoka kushoto akisubiri vifaa vya ujenzi wa meli mpya ziwa victoria wa pili kushoto mkuu wa mkoa wa mwanza John Mongella wa nne kushoto Katiibu wa CCM Mkoa Salum Kalli.


Baadhi ya wananchi wakishuhudia vifaa vya Ujenzi wa meli vikiingia -Mwanza


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella





PUMA ENERGY INALALA 'JALALANI' NA WATOTO WENYE MAHITAJI' YATOA MILIONI 40 KUMUUNGA MKONO MKUU WA MKOA WA DAR..PAUL MAKONDA KUOKOA MAISHA YA WATOTO 20 WANAOUGUA UGONJWA WA MOYO.





NA SAID MWISHEHE

KAMPUNI ya mafuta ya Puma Energy, imeunga mkono kampeni ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya  kuokoa maisha maisha watoto wanaogua ugonjwa wa moyo kwa kuchangia Sh milioni 40 ili kufanikisha upasuaji kwa watoto 20.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana mashindano ya michoro ya Usalama Barabarani kwa wanafunzi wa mkoa humo kwa mwaka 2019, Mkurugenzi wa Puma Energy,  Dominic Dhanah, alisema hatua ya kuunga mkono kampeni hiyo ni kuhakikisha wanaokoa maisha ya watoto ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia matibabu.

Akizungumzia mafunzo ya usalama barabarani kwa watoto wa shule za msingi, alisema yamesaidia kupunguza ajali katika maeneo ambayo wametoa mafunzo hivyo wanaamini kwa kufanya hivyo wanaokoa kizazi cha sasa na kijacho kwa kuwa elimu ya matumizi bora ya barabara inaendelea kusambaa.

“Lengo kubwa la mpango huu ni kuwafanya watoto hawa kuwa na uelewa wa matumizi ya barabara wakiwa bado wadogo. Tunaamini kwa kufanya hivyo tunawaongezea uelewa kuhusu dhima nzima ya usalama barabarani kwa wa Tanzania wengi zaidi,” alisema Dhanah.

Alisema kazi hiyo kwa mwaka huu imefanyika katika mikoa ya Dodoma na visiwani Zanzibar ambapo jumla ya shule 34 zitafikiwa kwa mpango huu kwa mwaka 2019.

“Lengo letu kama kampuni ni kuongeza wigo ili kufikia shule nyingi Zaidi nchi nzima. Pia tutaendelea kuwekeza katika kampeni ya usalama barabarani ikishirikiana na serikali kupitia Jeshi la Polisi ili kuokoa maisha ya Watanzania,” alisema

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, alisema kuwa Kampuni ya Puma, imetoa kiasi cha Sh milioni 40 ambapo wamegharamia matibabu ya watoto 20 ambao wanahitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo lakini wazazi mwao hawana uwezo wa kulipia matibabu.

“Puma wameonesha njia ya kujali na kutusaidia kwenye moyo. Niliomba msaada huo katika mkutano wa SADC. Nina watoto 500 pale Muhimbili wanaumwa moyo.

“Mimi nikialikwa mahali ninaomba msaada kwa wananchi wangu. Dominick wa Puma nilimuomba na gharama za matibabu kwa kila mtoto ni Shilingi milioni mbili kwa kiasi hiki cha fedha Shilingi milioni 40 sasa tunakwenda kurudisha tabasabu kwa watoto 20.

“Watapata operesheni kwakuwa sehemu ya faraja na mafanikio kwa mtoto atakayefanyiwa opesheni. Hata nilipokutana na Balozi wa Dubai baada ya kumueleza hili, yeye alikwenda kuleta madaktari ambao walifanya upasuaji wa matibabu kwa watoto 50. Mwezi ujao nitaunda kamati ya watu saba kwa ajili ya kusaka Shilingi bilioni moja, ili mpaka tukifika Desemba mwaka huu watoto wote wawe wamefanyiwa upasuaji,” alisema Makonda

Akizungumzia idadi ya watu wanaopata ajali za barabarani, alisema kuwa kwa sasa imepungua kutokana na elimu ya usalama barabarani.

“Tuna imani watoto 1m atakuwa na uelewa iwapo wataelimishwa na wenzao. Watumia vyombo vya moto watambue kila mmoja ana jukumu la kufuata usalama barabarani. Kabla ya Desemba kutakuwa na check up ya bure kwa wanaotaka kwenda likizo.

“Mafundi wa bure watakuwapo, nataka waende vizuri kula likizo na warejee tena Dar wakiwa salama. Trafiki kwenye mwendokasi inafanya vibaya,” alisema

Hata hivyo Makonda aliagiza kukamatwa kwa madereva wanaotumia barabara za mwendokasi.

“Wanatumia barabara ya mwendokasi wakamatwe hakuna gari, pikipiki wala mtu anayepaswa kuitumia, Mwakyoma (RTO),  apeleke trafiki hapo,” alisema

Mpaka sasa wanafunzi zaidi ya 20,000 wa shule za msingi katika shule tisa  za Jiji la Dar essalaam  wamepata mafunzo ya usalama barabarani ambapo katika mashindano hayo Shule ya Msingi Kibamba iliibuka mshindi wa kwanza na kuzawadiwa Sh milioni nne.






Thursday, 12 September 2019

MSHINDI WA JACKPOT YA SPORTPESA AMEPOKELEWA NA WAZAZI WAKE, YEYE AELEZA FURAHA YAKE






Yule mshindi wa Jackpot ya Sh Mil. 825 Magabe Marwa amesema kuwa anajisikia furaha kurudi nyumbani kwao na kukutana na familia, wazee huku akiamini hicho alichoshinda kitamfanya aishi maisha ya kati tofauti na awali.


Marwa hivi karibuni alishinda mamilioni hayo pamoja na mwenzake Kingsley Simon mamilioni hayo kabla ya kugawana Sh Mil. 412 kila mmoja baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 13.


Marwa alisema kuwa mamilioni atayatumia kwa ajili ya matumizi ya familia yake pekee aliyoyaanzisha kwa maana ya mke na watoto, na familia aliyotoka kwa maana ya wazazi na wadogo zake,  hivyo ndio vitu vya msingi.


"Mimi ndio mtoto wa pili kwenye familia yetu, na tangu wazazi wangu wana nguvu mpaka wanafikia hatua hii, mimi ndio nimeyafaidi sana maisha. " "Sisi ni familia ambayo huwa tunafuraha hata kama kuna shida na inapendwa na watu wengi," alisema Marwa.


Neno la shukrani kwa SportPesa

"Naishukuru SportPesa kwakuwa wameweza kubadilisha maisha yangu, hivyo ningependa kuwashauri vijana wenzangu kuwa kama mtu anaweza basi aweze kucheza kama ambavyo mimi nimethubutu, maana cha msingi ni uthubutu.


Kuiamini SportPesa

"Mimi mara nyingi huwa nacheza Multibet kwa hiyo kama nikipata kidogo huwa napokea na mimi tayari ni mtu mwenye upeo kwamba hii michezo ipo kisheria.


"Najua nikishatengeneza mkeka wangu nikabet naletewa namba kwa hiyo kama wasiponilipa nina uwezo wa kwenda mahakamani kufungua kesi kwa hiyo nilikuwa najua kwamba nikishinda nitapata changu.


"Kwa watu ambao wanacheza na wale ambao bado hawajaingia kucheza, hii ni fursa ambayo haihitaji nguvu kubwa sana na haikuzuii kufanya shughuli nyingine.


"Ninaamini kama ukiitumi kama fursa, Mungu akikujalia na uwezo wako wa kutengeneza timu na kuzichambua basi mwisho wa siku utaibuka mshindi kama mimi


Marwa aliongeza kuwa yeye ni mtumishi na alikuwa na mipango yake  aliyoipanga lakini hamufikiri kwamba atakuja kupata fedha kama hiyo na kupanga mipango itakayomtoa hapo alipo hivi sasa ya kushinda mamilioni ilikuwa nafikiria kwamba nipange mipango itakayomtoa katika maisha yake ya hivi sasa.

WAHITIMU WA AKADEMI YA MULTCHOICE WATING BUNGEN


Wanafunzi wanne waliohitimu hivi karibuni mafunzo maalum ya uzalishaji filamu chini ya programu ya MultiChoice Talent Factory wamehudhuria kikao cha bunge la Tanzania kama wageni maalum wa Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Katika ziara hiyo pia wanafunzi hao walikutana na wadau mbalimbali akiwemo naibu spika Dr. Tulia Akson waziri Dr. Harrison Mwakyembe, naibu waziri Juliana Shonza, naibu waziri Anthony Mavunde na katibu mkuu wa wizara Suzan Mlawi.

1Mwakyembe
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe akisalimiana na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi pampja na mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na wahitimu hao katika viwanja vya bunge jijini Dodoma, viongozi hao waliwataka wahitimu hao kutumia mafunzo maalum waliyoyapata katika kuleta mapinduzi ya tasnia ya filamu hapa Tanzania. 
3 Juliana
Naibu waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Juliana Shonza (kushoto) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) katika viwanja vya bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kulia ni Wilson Nkya, Grace Mgaya, Jane Moshi, Sarah Kimario na Jamal Mohamed.

Kwa pamoja wamekiri kuwa tasnia ya filamu ni moja ya tasnia zinazokuwa kwa haraka hapa nchini hivyo ni muhimu wanatasnia wawe na mafunzo ya kutosha na yanayoendana na wakati ili iweze kupambana na nchi nyingine katika soko la filamu ulimwenguni huku tukihakikisha kuwa kazi zetu zinaakisi mila, desturi, utamaduni na uzalendo wetu.

4Tulia
Naibu Spika Dr. Tulia Ackson (katikati) akizungumza na wahitimu wa Akademi ya Filamu ya MultiChoice (MultiChoice Talent Factory Academy) nje ya ukumbi wa bunge jijini Dodoma jana. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika. Kutoka kushoto ni Jane Moshi, Sarah Kimario, Jamal Mohamed na Wilson Nkya

Akizungumza na wanafunzi hao baada ya kumtembelea ofisini kwake, Katibu Mkuu Suzan Mlawi amesisitiza ahadi ya serikali kushirikiana na wadau wa tasnia mbalimbali ili kuharakisha ukuaji wa tasnia hizo. Amesema ushirikiano kati ya serikali na wadau ni muhimu na kwamba serikali itaendelea kuhakikisha kuwa sera na kanuni zinaboreshwa ili kuakisi hali halisi ya ukuaji wa tasnia ya filamu.
Wanafunzi hao wanne – Wilson Nkya, Jane Moshi, Jamal Mohamed na Sarah Kimario wamehitimu mafunzo maalum ya mwaka mmoja yanayofadhiliwa na MultiChoice ambapo vijana 60 kutoka kote barani Afrika huchaguliwa kwa mafunzo hayo kutoka nchi mbalimbali. Programu hiyo ina vituo vitatu vya mafunzo ambapo kwa upande wa kusini mwa Afrika kipo Lusaka Zambia, kwa Afrika Mashariki na kati kipo Nairobi Kenya na kwa Afrika Magharibi Lagos Nigeria.

2Mwakyembe
Mkuu wa Mahusiano wa MultiChoice Tanzania Johnson Mshana (wa pili kushoto) akiwatambulisha wahitimu wa mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu kwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe (Kushoto) mara baada ya wahitimu hao kuhudhuria kikao cha bunge kama wageni maalum wa waziri. Wanafunzi hao 4 kutoka Tanzania ni miongoni mwa wanafunzi 60 kutoka bara la Afrika walioshiriki mafunzo maalum ya uzalishaji wa filamu yanayofadhiliwa na MultiChoice Afrika kupitia program yake ya MultiChoice Talent Factory. Kutoka kulia ni Sarah Kimario, Jamal Mohamed, Wilson Nkya, Jane Moshi pampja na Afisa Uhusiano wa MultiChoice Tanzania Grace Mgaya

Awamu ya pili ya program hii itaanza mwezi Octoba 2019 ambapo wanafunzi wengine 60 watapata mafunzo hayo. Tanzania kwa mara nyingine tena itapeleka wanafunzi wanne.

Tuesday, 20 August 2019

MAN U..........NA POGBA...NI JUA NA ARDHI.......




WANANCHI WA KIJIJI CHA WAMI NA MBUNGE MGIMWA WAIKATAA BARABARA INAYOTENGENEZWA NA KAMPUNI YA FABEC CIVIL AND TELECOM ENGINEERS

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiungana na wananchi kuikataa barabara ambayo inatengenezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe) akiwa na sambamba na diwani wa kata ya Ihalimba

Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiungana na wananchi kuikataa barabara ambayo inatengenezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe)

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa mbunge wa  jimbo la Mufindi Kaskazini wakimsikiliza mbunge wao juu ya utengenezaji wa barabara unaotekelezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe)

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.



Wananchi wa kijiji cha Wami(mbalwe) kilichopo katika kata ya Ihalimba wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wameikataa barabara inayotoka katika kijiji cha Vikula kwenda wami(mbalwe) kutokana na kutengenezwa chini ya kiwango na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers na kusababisha madhara ya kiafya kwa wananchi wa kijiji hicho.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara ulihudhuriwa na mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa,walimwambia mbunge huyu kuwa mkarasi aliyepewa kazi ya kutengeneza barabara hiyo ameahibu ukilinganisha na ilivyokuwa hapo awali.

“Mheshimiwa Mbunge wetu Mahmoud Mgimwa tunakuomba kweli hii barabara imetengenezwa chini ya kiwango kweli kweli kiasi cha kusababisha magonjwa ya kifua na mafua na kusababisha kuanza kuingia gharama ambazo zipo nje ya bajeti zetu sisi wananchi hivyo unapaswa kuliangalia swali hili kwa njia ya kutuokoa wananchi wako” walisema wananchi

Wananchi hao waliongeza kwa kusema kuwa mkandarasi huyo amekuwa anamajibu mabaya yasiyolizisha kwa wananchi na viongozi wa kijiji hicho kwa kuwa kazi hiyo walipewa na serikali ya mkoa wa Iringa hivyo mtu pekee wa kuwawajibisha ni serikali ya mkuu wa Mkoa na sio mtu mwingine yeyeto yule.

“Mbunge huyu mkandarasi anakiburi na anamajibu mabaya mno maana ametengeneza barabara chini ya kiwango na kusababisha madhara kwa wananchi ila kila akiulizwa hatoe majibu ya kurizisha kwa wananchi hata kwa viongozi wetu” alisema mmoja ya mwananchi  aliyekuwepo kwenye mkutano huo wa hadhara

Aidha wananchi hao walisema kuwa utengenezwaji wa barabara hiyo unaotengenezwa na kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers umesababisha kukatika kwa masaliano ya kijiji hicho kwa kuwa hakuna usafiri wa magari ya abiria yanayofanya safari kuelekea katika kijiji hicho.

“Huku saizi hakuna usafiri wa gari yeyeto  ya abiria ambao unafika huku kutokana na mkandarasi huyu kukata mawasialiano ya barabara yetu hii ambayo hapo awali ilikuwa inapitika vizuri na mabasi yalikuwa yanakuja  na tulikuwa tunasafiri saizi hakuna kitu mheshimiwa mbunge Mgimwa” walisema wananchi

Akijibu hoja hizo za wananchi wa kijiji cha wami(mbalwe) mbunge wa jimbo hilo Mahmoud Mgimwa alikiri kuwa kuwa hata yeye hakubariani na utengenezaji wa barabara hiyo kutokana na mkandarasi huyo kutengeneza barabara hiyo chini ya kiwango na kusababisha madhara kwa wananchi wa kijiji cha wami(mbalwe)

“Saizi naona mnaguna hapa kutokana na kupata ugonjwa wa mafua kutokana kutengenezabarabara chini ya kiwango na kusababisha vumbi jingi ambalo linasababisha magonjwa hayo na imekata mawasialiano ya usafiri kwa wananchi hao” alisema Mgimwa

Mgimwa alirazimika kumpigia simu meneja wa TARURA wilaya ya Mufindi enjinia Sanga kusitisha malipo kwa mkandarasi huyo kwa kuwa amekuwa akifanya kazi chini ya kiwango na amekuwa na majibu ambayo siyo ya kulidhisha kwa wananchi pale wanapohoji kiwa njo na kutengeneza barabara hiyo.

“Nakuomba meneja kuanzia sasa sitisha malipo kwa mkandarasi huyo hadi pale atakapo kamilisha kutengeneza barabara hiyo ili kurahisisha maendeleo kwa wananchi wa kijiji hicho” alisema Mgimwa

Kwa upande wake msimamizi wa miradi ya kampuni ya Fabec civil,Building and Telecom Engineers Heri Rubeni alisema kuwa magari na vitendea kazi vyao vingi vimeharibika toka wiki iliyopita hivyo wapo kwenye matengenezo na vifaa hivyo vikikamilika ndio watarudi kazini na kuanza kufanya kazi upya.

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube