Yule mshindi wa Jackpot ya Sh Mil. 825 Magabe Marwa amesema kuwa anajisikia furaha kurudi nyumbani kwao na kukutana na familia, wazee huku akiamini hicho alichoshinda kitamfanya aishi maisha ya kati tofauti na awali.
Marwa hivi karibuni alishinda mamilioni hayo pamoja na mwenzake Kingsley Simon mamilioni hayo kabla ya kugawana Sh Mil. 412 kila mmoja baada ya kubashiri kwa usahihi mechi 13.
Marwa alisema kuwa mamilioni atayatumia kwa ajili ya matumizi ya familia yake pekee aliyoyaanzisha kwa maana ya mke na watoto, na familia aliyotoka kwa maana ya wazazi na wadogo zake, hivyo ndio vitu vya msingi.
"Mimi ndio mtoto wa pili kwenye familia yetu, na tangu wazazi wangu wana nguvu mpaka wanafikia hatua hii, mimi ndio nimeyafaidi sana maisha. " "Sisi ni familia ambayo huwa tunafuraha hata kama kuna shida na inapendwa na watu wengi," alisema Marwa.
Neno la shukrani kwa SportPesa
"Naishukuru SportPesa kwakuwa wameweza kubadilisha maisha yangu, hivyo ningependa kuwashauri vijana wenzangu kuwa kama mtu anaweza basi aweze kucheza kama ambavyo mimi nimethubutu, maana cha msingi ni uthubutu.
Kuiamini SportPesa
"Mimi mara nyingi huwa nacheza Multibet kwa hiyo kama nikipata kidogo huwa napokea na mimi tayari ni mtu mwenye upeo kwamba hii michezo ipo kisheria.
"Najua nikishatengeneza mkeka wangu nikabet naletewa namba kwa hiyo kama wasiponilipa nina uwezo wa kwenda mahakamani kufungua kesi kwa hiyo nilikuwa najua kwamba nikishinda nitapata changu.
"Kwa watu ambao wanacheza na wale ambao bado hawajaingia kucheza, hii ni fursa ambayo haihitaji nguvu kubwa sana na haikuzuii kufanya shughuli nyingine.
"Ninaamini kama ukiitumi kama fursa, Mungu akikujalia na uwezo wako wa kutengeneza timu na kuzichambua basi mwisho wa siku utaibuka mshindi kama mimi
Marwa aliongeza kuwa yeye ni mtumishi na alikuwa na mipango yake aliyoipanga lakini hamufikiri kwamba atakuja kupata fedha kama hiyo na kupanga mipango itakayomtoa hapo alipo hivi sasa ya kushinda mamilioni ilikuwa nafikiria kwamba nipange mipango itakayomtoa katika maisha yake ya hivi sasa.
No comments:
Post a Comment