Monday, 20 February 2017
DC SAME AAGIZA WANAFUNZI KUWA NA MITI YA KUITUNZA
![]() |
| Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule. |
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki Senyamule amewaagiza walimu wakuu Wilayani Same Mkoani Kilimanjaro kusimamia zoezi la upandaji miti kwa kumkabidhi kila mwanafunzi mti mmoja ambao atautunza katika kipindi chake cha masomo.
Dc Senyamule
ametasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa elimu Wilayani humo
kilichohudhuriwa na walimu wote wa shule za msingi na sekondari,
Waratibu elimu, Maafisa Tarafa, Wazazi, Wanafunzi wawakilishi pamoja na
baadhi ya Viongozi wa dini.
“Sote hapa kwa umoja wetu ni lazima tutambue kuwa
matokeo bora ya wanafunzi waliopo darasa la saba, wanafunzi wa kidato cha nne
na cha sita yapo mikononi mwa walimu hivyo njia bora ni kutatua matatizo yanayowakabili
walimu ili tuweze kufikia lengo” Alisisitiza Mhe Senyamule
Ameeleza kuwa endapo Changamoto za makundi yote zitatekelezwa kwa kufuata utaratibu ikiwemo kila mmoja kutumia nafasi yake ipasavyo katika kufuatilia mwenendo wa wanafunzi kwa kuanzia Walimu, Serikali, Wazazi, na Wanafunzi Wilaya hiyo itakuwa na matokeo makubwa katika matokeo yajayo.
Staki alisema kuwa Wilaya ya Same imeanza imeanza kukua kielimu kupitia matokeo ya kidato cha pili na cha nne kwani Wilaya hiyo imeshika nafasi ya 62 kati ya Halmashauri 184 ambapo kwa Mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 103.
Aidha katika matokeo ya kidato cha pili Wilaya ya Same imeshika nafasi ya 37 kati ya 184 kwani mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 47.
Pia amewataka viongozi wote katika kada mbalimbali kutumia vyema uongozi wao kwa kuwatumikia wananchi huku akiwasihi kutumia lugha nzuri pindi wanapozungumza nao kwani kiongozi yeyote atakayetumia lugha mbaya anapaswa kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Same amepinga vikali matumizi ya Dawa za kulevya ambapo amesema kuwa kwa Wilaya hiyo baadhi ya wananchi wake ni wazalishaji wakubwa wa zao aina ya Mirungi ambalo pia limepelekea vijana wengi kutumia huku wakijiweka kando na elimu kwa kuamini kulima zao hilo sehemu ya mafanikio yao ya haraka.
Dc Staki amesema uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea na oparesheni ya kuteketeza matumizi ya mirungi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na matumizi ama uuzaji wa zao hilo.
Kikao hicho kilichokuwa na lengo la kukubaliana na
kupata namna bora ya kuboresha elimu na kiwango cha ufaulu Wilayani Same, Mkuu
huyo wa Wilaya amesisitiza kuwepo kwa namna maalumu kwa ajili ya wanafunzi
kufundishwa kwani mafanikio ya jitihada zao pekee katika kujisomea na
kufundishwa darasani haitoshi bali wanahitaji kuongezewa msukumo na utaalamu
zaidi kwa masomo ya ziada.
Ameeleza kuwa endapo Changamoto za makundi yote zitatekelezwa kwa kufuata utaratibu ikiwemo kila mmoja kutumia nafasi yake ipasavyo katika kufuatilia mwenendo wa wanafunzi kwa kuanzia Walimu, Serikali, Wazazi, na Wanafunzi Wilaya hiyo itakuwa na matokeo makubwa katika matokeo yajayo.
Staki alisema kuwa Wilaya ya Same imeanza imeanza kukua kielimu kupitia matokeo ya kidato cha pili na cha nne kwani Wilaya hiyo imeshika nafasi ya 62 kati ya Halmashauri 184 ambapo kwa Mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 103.
Aidha katika matokeo ya kidato cha pili Wilaya ya Same imeshika nafasi ya 37 kati ya 184 kwani mwaka uliopita ilikuwa nafasi ya 47.
Pia amewataka viongozi wote katika kada mbalimbali kutumia vyema uongozi wao kwa kuwatumikia wananchi huku akiwasihi kutumia lugha nzuri pindi wanapozungumza nao kwani kiongozi yeyote atakayetumia lugha mbaya anapaswa kuchukuliwa hatua haraka iwezekanavyo.
Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Same amepinga vikali matumizi ya Dawa za kulevya ambapo amesema kuwa kwa Wilaya hiyo baadhi ya wananchi wake ni wazalishaji wakubwa wa zao aina ya Mirungi ambalo pia limepelekea vijana wengi kutumia huku wakijiweka kando na elimu kwa kuamini kulima zao hilo sehemu ya mafanikio yao ya haraka.
Dc Staki amesema uongozi wa Wilaya hiyo unaendelea na oparesheni ya kuteketeza matumizi ya mirungi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote wanaohusika na matumizi ama uuzaji wa zao hilo.
17:52
NI UBABE UBABE TU U/ TAIFA KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA YANGA MWISHONI MWA JUMA,CCTV KUAMUA VURUGU MASHABIKI KUKIONA CHA MOTO.
Serikali ya imelitaka Shirikisho la Soka tanzania TFF kuwatumia waamuzi sahihi na wenye vigezo vya kuchezesha mechi kati yua Yanga na Simba Jumamosi wiki hii Mechi itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Singo wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kuwa iwapo waamuzi hawatatenda haki upande mmoja basi huenda ilateta matukio mabao ya kimichezo kutoka na upenzi wa timu hizo na mashabiki wake.
Singo ametoa tahadhari akieleza pia kuwa Serikali imejipanga kuahakikisha mchezo huo unafanyika bila matatizo na mashabiki kutoleta matatizo kama yaliyotokea nyuma.
Kwa upande wake msimamizi wa Usalama wa Uwanja kutoka Jeshi la Polisi amesema wamejipanga vyakutosha kuhakikisha mchezo unamalizika salama.
Aidha viongozi hao waliwatembeza waandishi wa Habari kujionea mwenekano wa Uboreshaji wa Camera za Uwanja huo za CCTV zitakazooonyesha matukio yote sehemu za Uwanja huo, ambapo iwapo mashabiki wataleta fujo wataonekana moja kwa moja na kuchukuliwa hatua.
Simba na Yanga zinakutana kwenye Mchezo huo kila mmoja akitaka kupata pointi tatu mhimu na kujiwekea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inayoelekea ukingoni.
17:22
WACHAMBUZI WA SOKA WAENDELEA KUMSAKAMA WENGER
Wachambuzi wa soka Uingereza wameendelea kumkosoa kocha wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger kuwa kikosi chake kimekosa kiongozi wa Uwanjani na kupelekea kuendelea kufanya vibaya kwa kila mchezo ikiwepo Ligi Kuu ya Uingereza.
Gary Neville na Rio Ferdinand ambapo sasa wanafanya uchambuzi wa soka katika vituo vya televisheni Super Sport,wamesema kuwa mwalimu huyo anaheshima kubwa katika soka lakini anaangushwa na wachezaji wake ambao wameshindwa kupata kiongozi ndani ya uwanja tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma wakati wakiwepo wachezaji kama Thierry Henry, Vieira ,hodha Tony Adamsna Martin Keown ambao walikuwa wachezaji wenye kushimka kutokana na kuwaongoza wachezaji wengine kwa maslahi ya klabu na mashabiki wake.
Rio amenukuliwa akisema 'Moja ya sababu zinazoonekana kuisumbua Arsenal ni uongozi wa ndani ya uwanja. Si timu tena yenye watu ambao wakati mwingine kwa misemo ya wapenda soka huitwa Baba Mwenye Nyumba.
Rio amesema kuwa wakati Arsenal ilipokuwa chini ya nahodha Patrick Vieira,na Manchester United ilikuwa kwa Roy Keane timu hizo zilipokuwa zikikutana kila mchezaji walionyesha umhimu wa kuongoza Uwanjani.
Viera kwa upande wake anasema kuwa kwa sasa Manchester United ina kiongozi ndani ya uwanja japo sio nahodha lakini ni mchezaji mwenye kiwango kikubwa cha soka duniani, akimaanisha Zlatan Ibrahimovic kuwa hakuna mchezaji wa Man U anayeweza kubishana naye.
Viera anasema wachezaji wa Arsenal kwa sasa, kila mmoja ni mkubwa na hata wale nyota mahiri kama Mesut Ozil au Alexis Sanchez
17:04
MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA MINJINGU
Mifuko ya mbolea ya kiwanda cha Minjingu mkoani Kagera ikiwa na maandishi yanayoonyesha kuwa mbolea hiyo inazalishwa nchini Kenya. Mifuko hiyo ambayo ilishuhudiwa na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa Februari 19, 2017 wakati alipotembelea kiwanda hicho, ilimkera sana na aliuagiza uongozi wa kiwanda hicho kumuandikia barua Rais John Pombe Magufuli ya kumuomba radhi kwa kitendo hicho. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
09:24
UNDP YAJENGA VYOO VYA SHILINGI MILIONI 510 KUSAIDIA USAFI KILIMANJARO.
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakizindua rasmi vyoo vilivyojengwa katika shule za msingi 10 wilayani Moshi za kufadhiliwa na UNDP.
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alavaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa wilaya ya Moshi Kippi Warioba wakitizama vyoo vilivyojengwa na UNDP katika shule ya Msingi Mandela.
Mkuu wa Idara ya Ushirikino wa Afria Mashariki ,Balozi Celestine Mushy (katikati) akizungumza jambo na Mkuu wa Wilaya ya Moshi Kippi Warioba (Kulia) kushoto ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi,Raymond Mboya mara baada ya kuzinduliwa kwa vyoo katika shule za msingi za Mandela na Azimio.
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez na ujumbe wake wakiangalia vyoo vya kisasa vilivyojengwa katika shule 10 katika manispaa ya Moshi na Manispaa ya Moshi.
Jengo la Choo kipya na cha kisasa kilichojengwa katika shule za Msingi za Azimio na Mandela vilivyojengwa na UNDP.
Choo maalumu kwa ajili ya walemavu kilichojengwa katika vyoo vipya vilivyojengwa na UNDP katika shule ya msingi 10 za Msingi wilayani Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi rasmi wa Vyoo 10 zilizojengwa katika shule za msingi 10 za wilaya ya Moshi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi ,Raymond Mboya akiteta jambo na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez wakati wa uzinduzi wa vyoo katika shule za msingi.
Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeelo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Alvaro Rodriguez akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Majengo ya vyoo katika shule 10 za Msingi,Moshi.
Mkuu wa Idara ya Ushirikino wa Afria Mashariki ,Balozi Celestine Mushy akizungumza katika uzinduzi huo.
Wanafunzi katika shule za Msingi za Azimio na Mandela wakitoa burudani za nyimbo na Ngoma wakati wa uzinduzi rasmi wa Vyoo katika shule za msingi za Azimio na Mandela.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba pamoja na Mwakilishi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez wakiwa katika picha za pamoja na viongozi wengine pamoja na kamati ya shule hizo.
Mkuu wa wilaya ya Moshi,Kippi Warioba pamoja na Mwakilishi wa Shirika la
Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini ,Alvaro Rodriguez
wakiwa katika picha za pamoja na wanafunzi wa shule za Azimio na Mandela.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Mwakiishi wa Shirika la Mipango wa Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini Tanzania ,Alvaro Rodriguez,akishirikiana na Mkuu wa Idara
ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki ,Balozi Celestine Mushy wamezindua vyoo 10 vilivyojengwa katika
shule za msingi 10 wilayani Moshi.
Ujenzi huo ulifanyika ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya
miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.
Wakati wa maadhimisho hayo pia wafanyakazi wa Umoja wa
Mataifa walifanya shughuli mbalimbali mkoani Kilimanjaro za kusaidia maendeleo
ikiwamo hifadhi ya mazingira na usafi.
Katika kuhakikisha kwamba shule zinakuwa na UNDP Tanzania
ilisaidia mkoa wa Kilimanjaro Sh Mil 510
kujenga vyoo vya kisasa katika shule za msingi 10 ili kusaidia kuezesha usafi
kwa wanafunzi na walimu wao.
Hadi kufikia sasa jumla ya matundu 178 yamejengwa katika
shule 10 ambapo matundu 104 ni kwa ajili ya wasichana na 74 kwa ajili ya
wavulana.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mwakilishi makzi wa
UNDP.Alvaro Rodriguez alipongeza mradi huo na ushirikiano uliokuwepo kati ya
serikali ,wao na shule ikiwa ni hatua moja ya maendeleo endelevu kwa kuboresha
mazingira ya usafi kwa wanafunzi wa kike na wa kiume katika masomo yao na hivyo
kuimarisha safari ya kuelekea malengo ya dunia ya 2030.
Alisema kutokuwepo kwa mazingirabora ya usafi ni chanagamoto
kubwa kwa wanafunzi na hali hiyo inawaathiri sana wanafunzi wa kike.
Rodriguez alisema kutokana na kujengwa kwa vyoo hivyo
wanafunzi ,walimu na walezi sasa watakuwa na kazi pekee ya kuhakikisha kwamba
wanatoa elimu bora .
“Watoto wa kike watakuwa na changamoto chache zaidi za
mahudhurio shuleni na wakati huo huo masUala ya usafi yatakuwa yameboreka na
hivyo kuwa na wanafunzi na familia zenye siha njema.”alisema Rodriguez.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa
katika wizara ya Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Balozi
Celestine Mushy amepongeza kwa msaada huo na kuutaka Umja wa MAtaifa kuendelea
kutoa msaada kwa shule zenye mahitaji makubwa kuhakikisha kwamba malengo ya
dunia yanayohusiaa na usafi ,mazingira na maji safi yanafanikiwa ifikapo mwak
2030.
Naye mkuu wa wilaya ya Moshi ,Kippi Warioba pamoja n
kuishukuru UNDP kwa kazi nzuri waliyofanya pia alizitaka jumuiya za maeneo
yaliyojengewa vyoo kuiliki msaada huo kwa kuhakikisha wanaitumia na hivyo
kuisadia kufikia malengo ya dunia 2010.
Mwisho.
09:19
Friday, 17 February 2017
SOPHIA MJEMA AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA KUKAGUA VIPIMO NA MIZANI FEKI, ILALA LEO
![]() |
| Mjema akionyeshwamizani malimbali feki na iliyo bora, katika karakana ya WMA mkoa wa Ilala |
![]() |
| Mjema akiwafafanulia zaidi kuhusu hasara ya Lumbesa |
![]() |
| Mfanyakzi katika Bucha moja eneo la Kariakoo, Omar Khalfan akitoa maelezo kuhusu mzani anaotumia kupimia nyama wateja,katika bucha hiyo. |
![]() |
| Mfanyakzi katika Bucha moja eneo la Kariakoo, Omar Khalfan akitoa maelezo kuhusu mzani anaotumia kupimia nyama wateja,katika bucha hiyo. |
![]() |
| Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo (kushoto) na Mkuu wa Wilaya hiyo Sophia Mjema wakimsikiliza kwa makini mfanyakazi wa bucha hiyo |
![]() |
| Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema akimhoji mfanyakazi huyo ikiwa kweli ana uhakika mzani wake ni halali |
![]() |
| Ofisa wa MWA (kulia) akijaribu kutumia vipimo vyake, kubaini kama mzani uliokuwa ukitumia katika Bucha ya Ndevu Complete, Kariakoo, siyo feki. Baadaye ulibainika kuwa mzani huo unafaa |
![]() |
| Mfanyakazi wa Bucha hiyo ya Ndevu Complete akiweka nyama kuonyesha mzani unavyopima |
![]() |
| Mjema akizungumza na wananchi na waandishi wa habari baada ya kumaliza sehemu ya ukaguzi wake wa vipimo na mizani, leo. Wapili kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo. |
08:57
Subscribe to:
Posts (Atom)














































