BREAKING

Monday, 23 January 2017

RAIS WA UTURUKI WASILI NCHINI


Rais wa  Uturuki,  Mheshimiwa  , Recep Tayyip Erdogan akiongozana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam kwa ziara rasmi Januari 22, 2017.Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan  aliyefuatana na  mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo  kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 22, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan akiagana na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa baada ya kumfikisha kwenye hoteli ya Serena  jijini Dar es salaam  baada ya kumpokea kwenye uwanja wa ndege wa Dar es salaam na kumsindikiza hadi kwenye hoteli hiyo alikofikia Januari 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Saturday, 21 January 2017

KINANA AWASHANGAA WAPINZAI KUDAI KUIBIWA KURA KILA UCHAGUZI


Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na makada ambao ni mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, alipokuwa akifunga  semina ya mawakala hao, leo Janauari 20, 2017. Uchaguzi mdogo wa Unatarajiwa kufanyika Jumapili hii nchini kote.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisaini kitabu cha wageni alipopita kwenye ofisi ya CCM Kata ya Kijichi akiwa njiani kenda kufunga semina ya makada ambao ni mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, leo Janauari 20, 2017. Kulia ni Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi huo, Tausi Milanzi.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwsili ukumbini kwa ajili ya kufunga semina hiyo. Kulia ni Mgombea Udiwani katika kata ya Kijichi  Tausi Milanzi, Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida.
Mawakala wa CCM katika Uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala Dar es Salaam, wakimshangilia, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipowasili ukumbini kufunga semina yao, leo
Meneja wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, akitoa maelezo, kabla ya Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kufunga semina ya mawakala wa CCM katika uchaguzi huo leo
Mgombea wa Udiwani kwa tiketi ya CCM, katika Uchaguzi Mdogo wa Madiwani, Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, Tausi Milanzi, akisalimia mawakala wa CCM waliokuwa kwenye semina maalum, kwa ajili ya uchaguzi huo
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, akisalimia viongozi na mawakala wa CCM, katika Ucaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi
Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, akisalimia viongozi na mawakala wa CCM, katika Ucaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi
Katibu Mkuu wa CCM, akipokea kadi kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa Chadema Adam Hamis ambaye aliamua kuhamia CCM, wakati wa Semina ya Mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kijiji, iliyofanyika leo
Kisha Katibu Mkuu akampa Kapelo rasmi ya CCM
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, ili amkaribishe Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kufunga semina hiyo
Mwenyekiti wa CCM mkkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida akifafanua jambo kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kufunga semina hiyo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na makada ambao ni mawakala wa CCM katika uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kijichi, Mbagala, Dar es Salaam, alipokuwa akifunga  semina ya mawakala hao, leo Janauari 20, 2017. Uchaguzi mdogo wa Unatarajiwa kufanyika Jumapili hii nchini kote

MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA KWENYE UWANJA WA MABEWANI MJINI MAKETE

 Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Mabewani mjini Makete, januari 20, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


SERIKALI YAMPONGEZA MWANARIADHA ALPHONCE FELIX SIMBU KWA KUILETEA SIFA TANZANIA KWENYE RIADHA

 Mwanariadha Alphonce Felix Simbu akizungumza katika hafla hiyo iliyoandaliwa na wadhamini wake DSTV
 Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Wilhelm Gidabuday 
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye akizungumza katika hafla ya kumpongeza mwanariadha Alphonce Felix Simbu baada ya kutwaa ubingwa katika mashindano ya Riadha Mumbai-India

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanazania  Baraka Shelukindo akitoa nemno katika hafla hiyo,DSTV ni wadhamini wa Simbu.

Serikali imempongeza mwanariadha kimataifa Alphonce Felix Simbu kufuatia ujasiri wake kufuatia ubingwa wa mbio za Marathoni kwa mwaka huu nchini India.

Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nanuye wakata wa hafla maalum iliyoandaliwa na kampuni ya Multi-Choice Tanzania jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na pongezi amemshukuru kwa kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania  katika medani za kimataifa.

Aidha Waziri Nape pia ameipongeza kampuni ya Multichoice Tanzania kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha sekta ya michezo inapiga hatua, huku uongozi wa kampuni hiyo ukiahidi kuendelea kumdhamini mwanariadha huyo katika ushiriki wake kwenye michuano mbalimbali ya kimataifa.

Kwa upande wao, bingwa Alphonce Simbu na Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Wilhelm Gidabuday pamoja na kuishukuru Serikali wamewaomba wadau wa michezo kuwaunga mkono wanariadha wengine jambo litakalosaidia kutengeneza timu bora kwa ajili ya mashindano ya kitaifa na kimataifa.

Thursday, 19 January 2017

MAJALIWA ATATUA MGOGORO WA MPAKA WA KILINDI NA KITETO


Waziri Muu, Kassim Majaliwa  akizugumza na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi   (kushoto)  Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel wakiwa katika kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka  wa wilaya ya Kiteto na Kilindi  Januari 18, 2017.  Mheshimiwa Majaliwa alikwenda Kiteto na Kilindi kutatua mgogoro wa mpaka unaovikabili vijiji vya  Mafisa na Kijungu. Wapili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Muu wa Wilaya ya Tanga mjini , Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Mkuu, Kassim Majaliwa  akielekea kwenye moja ya  jiwe la mpaka wa  wilaya ya Kilindi na Kiteto wakati alipokwenda  kwenye kijiji cha Lembapuli kilichopo kwenye mpaka wa Kiteto na Kilindi kutatua  mgogoro wa mpa Januari 18, 2017. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni  Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akipata maelezo  kutoka kwa watalaam wa upimaji ardhi kuhusu jiwe la alama ya mpaka wa wilaya ya Kilindi na Kiteto katika kijiji cha  mpakani cha Lembapuli  Januari 18, 2017. . Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na kulia kwake ni  Mkuu wa wilaya na Tanga na Kaimu  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akipata  maelezo kuhusu ramani inayoonyesha mpaka  wa wilaya  ya Kilindi na Kiteto katika kijiji cha mpakani cha Lembapuli wakati alipokwenda kutatua mgogoro wa mpaka kati ya wialya hizo Januari 18, 2017.  Mheshimiwa  Majaliwa apia alifuatana na Mawaziri , William Lukuvi wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi na George Simbachawene  wa Ofisi ya Rais- TAMISEMI.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Kiteto na Kilindi  wakati  alipokwenda kwenye kijiji  cha Lembapuli  kilichopo kwenye mpaka wa wilaya hizo  kutatua mgogoro wa mpaka Januari  18, 2017.  Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na wapili kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wa Kiteto na Kilindi  wakati  alipokwenda kwenye kijiji  cha Lembapuli  kilichopo kwenye mpaka wa wilaya hizo  kutatua mgogoro wa mpaka Januari  18, 2017.  Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Manyara, Dkt. Joel Bendera na wapili kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akihutubia  mkutanao wa hadhaa katika kijiji cha  Lembapuli kilichopo mpakani mwa wilaya za Kilindi na Kiteto alikokwenda kutatua mgogoro wa  mpaka  Januari 18, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Baadhi ya wananchi wa  wilaya za Kilindi na Kiteto wakimshangilia  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipohutubia mkutano wa hadhara katika kijiji  cha  Lembapuli kilichopo  mpakani mwa wilaya za Kiteto na Kilindi alikokwenda kutatua mgogoro wa mpaka Januari 18, 2017. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

Wednesday, 18 January 2017

MAJALIWA AFUNGUA DUKA LA DAWA LA MSD KATIKA HOSPITALI YA MPANDA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Rafael Muguga baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda Januari 17, 2017  ambako  alifungua duka la dawa la MSD.  Wpili kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Katavi, Muselem  Said Abdallah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi na watumishi wa Halmashauri na Manispaa ya Mpanda  na wananchi  kwenye Ikulu ndogo ya Mapanda Januari 17, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza na Elizabeth Zephania , mmoja wa wazazi waliojifungua katika hospitali ya Mpanda  wakati alipotembelea wodi ya wazazi ya hospitali hiyo Januari 17, 2017.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa Mpanda kabla ya  kufungua duka la dawa la MSD katika hospitali hiyo Januari 27, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Tuesday, 17 January 2017

*AWASIHI WANASIASA KUJIKITA KATIKA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA *WASITUMIE UONGO NA SHIDA ZA WATU KUSAKA UMAARUFU WA KISIASA





Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimewasihi viongozi wa vyama vya wapinzani kujikita katika siasa safi na uongozi bora, kwa kuachana na matamko ya uongo yanayosababisha taharuki katika nchi na kuchonganisha wananchi na serikali yao, kwa kuwa vitendo hivyo havina manufaa kwa mustakabali wa maendeleo ya taifa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Huphrey Polepole, wakati akizungumza na waandishi wa habari, leo Januari 17, 2017, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, kutoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ya Kichama.

Polepole amsema, wapinzania wamekuwa wakitumia matatizo ya wananchi na kutoa matamko ya uongo ili kutia nchi katika taharuki kwa lengo la kujitafufia umaarufu wa siasa vitendo ambavyo alisema, havisaidii wananchi wala wanasiasa  wa vyama hivyo katika kuleta maendeleo ya nchi.

Alisema, mbali na matamko ya viongozi wa vyama hivyo kutosaidia, katika ujenzi wa maendeleo yamaendeleo ya nchijambo ambalo alisema za kueneza maneno ya yasiyofanyiwa utafiti kwa lengo la kusababisha taharuki kwa wananchi, jambo ambalo alisema, si miongoni mwa siasa safi wala uongozi bora.

Polepole alisema, wapinzani wamekuwa wakifanya siasa za aina hiyo wakiwa wanajua ubaya wake, kwa kuwa wao lengo lao ni kujaribu kuchonganisha wananchi na serikali hata pale ambapo serikali inaonyesha juhudi za dhali za kuijenga Nchi yenye uchumi imara wa viwanda.

"Nawaonba Watanzania tuwapuuze wanasiasa wa vyama hivi,  tuendelee kuiunga mkono serikali, ili itimize mipango na malengo iliyoweka, ikiwemo kuhakikisha Tanzania inakuwa kiuchumi kwa kuwa nchi ya viwanda, hali ambayo itasaidia sana kutukwamua Watanzania kutoka katika umasikini", alisema Polepole.

Polepole alitaja kuwa miongozi mwa mambo ambayo katika kipindi hiki wanayatumia kupotosha ili kujaribu kuletea taharuki wananchi ni pamoja na kueneza propaganda kuwa Tanzania imekumbwa na baa la njaa na pia kutumia matatizo waliyopata wananchi wakati wa janga la tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera kama mtaji wao kisiasa.

"Kwanza mjue, kutungaza taarifa ambazo zitaleta taharuki katika jamii ni kosa la jinai, lakini pia inajulikana na wenyewe wanajua, kwamba Duniani kote zipo taratibu ya utangazaji wa majanga katika nchi yoyote. Baa la njaa ni janga kubwa linapofikia kiwango kibaya, mwenye mamlaka ya kutangaza ni Mkuu wa nchi", alisema Polepole na kuongeza;

Alisema, Tanzania haijawahi kupata  njaa yenye kiwango cha kuitwa baa la njaa, katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, hivyo wanaojaribu kutangaza kuwa Nchi ipo katika baa la njaa ni kushindwa kufanya siasa safi na kukosa uongozi bora kama ilivyo CCM ambayo mambo hayo inayo.

"Ingawa tumekuwa na tatizo la njaa katika sehemu chache za na kuwepo upungufu wa mvua katika maeneo kadhaa ya nchi hali ambayo inaweza kusababisha upungufu wa chakula katika maeneo husika, bado hili siyo baa la njaa. Na kwa kuwa hili serikali inalijua inaendelea kuweka mazingira mazuri ili kuweza kupelekwa vyakula maeneo yote kuondoa uhaba, na kipindi hiki hatujafikia huko", alisema Polepole.

"Baada ya kuona hali ipo hivi nilitarajia viongozi wote bila kujali vyama , tuhimize wananchi kutumia chakula vizuri wasikitumie katika mambo ya anasa au kukiuza hovyo, lakini wao wanakimbilia kutangaza baa la njaa wakati njaa yenyewe haijatokea, hawa watu wa ajabu sana', alisema Polepole.

Alisema, kila kiongozi anayeongozwa na misingi ya uongozi bora na mzalendo kwa nchi yake, analo jukumu la kuwahamasisha wananchi kutunza vyakula walivyonavyo.

Kuhusu tetemeko lilitokea Bukoba  na kusababisha uharibifu na vyumba za watu na miundombinu mbalimbali alisema kama ilivyo ulimwenguni kote, inapotokea mambo haya ya majanga serikali hujenga uwezo wake kwanza ili kusaidia wananchi wake.

"Baada ya tetemeko lile, Serikali ilichofanya ni kujengea uwezo wa wananchi wasiwe mbali na huduma  ndiyo maana ikaimarisha miundombinu ya elimu, afya na barabara, kwa sababu watu waendelee kupata huduma". alimalizia Polepole
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube