BREAKING

Thursday, 15 December 2016

MAJALIWA AWASILI LOLIONDO KUENDELEA NA ZIARA YA MKOA WA ARUSHA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakati alipowasili kwenye  uwanja wa ndege wa Kiltaro katika tararafa ya Loliondo kuendelea na ziara yake

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanawake wa Kimasai wakati alipotembelea Kituo mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni kilichojengwa na UNICEF katika kijiji cha Ololosokwan kilichopo Loliondo wilayani  Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitazama kazi mbalimbali za mikono hasa mapambo yanayotengenezwa na wanawake wa kimasai katika kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro wakati alipotembelea Kituo cha Mafunzo ya kazi za mikono na utamaduni  kijijini  hapo Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwa ndani ya nyumba ya asili ya wamasai maarufu kwa jina la Emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan  kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitoka ndani ya nyumba ya asili ya wamaai maarufu kwa jina la emanyatta katika kijiji cha Ololosokwan kwenye tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Wananchi wa kijiji cha Ololosokwan  kwenye tarafa ya  Loliondo wilayani Ngorongoro  wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipowasalimia akiwa ktika ziara ya wilaya ya Ngorongoro Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanchi wa kijiji cha Ololosokwan katika tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro akiwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 15, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, 13 December 2016

MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUKAMUA MAFUTA YA KULA CHA MERU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akionyeshwa mafuta  ya kula na Mkurugenzi wa Mkuu wa Makampuni ya Meru, Bw. Atul Mittal  (kushoto) wakati alipotembelea kiwanda cha kukamua mafuta cha Meru kilichopo mjini Singida, Desemba 12, 2016.  Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba na watatu kulia na Mbunge wa Viti Maalum na Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Singida, Martha Mlata. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  kiwanda cha kukamua mafuta ya kula cha Meru kilichopo mjini Singida, Desemba 12, 2017. Watatu kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Meru, Bw. Atul Mittal. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Mkurugezi Mkuu wa makampuni ya Meru, Bw. Atul Mittal kuhusu mafuta ya kula yanayozalishwa na kiwanda cha Meru cha Singida mjini  wakati alipotembelea kiwanda hicho Desemba 12, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Sunday, 11 December 2016

JPM AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM LEO

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kilichofanyika leo mjini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, na Kushoto ni Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein.
 Mweyekiti wa CCM, Rais John Magufuli akiwa tayari kuongoza kikao hicho
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk John Magufuli akiwa na baadhi ya viongozi kabla ya kikaokuanza. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Kushoto, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Dk Magufuli kufungua kikao
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Dk Magufuli kufungua kikao
 Mwenyekiti wa CCM, Dk John Magufuli akimsalimia Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dk Shein, alipowasili ukumbini
 Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Vuai Ali Vuai, akimsalimia Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein walipokutana ukumbini kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. 
 Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa akimsalimia Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Jerry Silaa, alipowasili ukumbini kwenye kikao cha kamati kuu ya CCM, kilichofanyika mjini Dar es Salaam, leo.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Dk. Salimu Ahmed Salim alipowasili kwa ajili ya kushiriki kikao cha kamati kuu ya CCM, kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein alipowasili kwenye kikao cha Kamati kuu ya CCM, kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, alipowasili kuendesha Kikao Cha Kamati cha Kamati Kuu ya CCM, leo mjini Dar es Salaam. PICHA: BASHIRI NKOROMO

MAJALWA AWASILI DODOMAMA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Christina Mndeme baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma Desemba 11, 2016 na kesho anatarajiwa kwenda Singida kuwa mgeni rasmi kwenye   sherehe za Maulid. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Thursday, 8 December 2016

BALOZI WA CUBA HAPA NCHINI AMUAGA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA, LEO


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Balozi wa Cuba, Jorge Luis Lopez (kushoto), alipofika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kumuaga kufuatia kumalizika kwa mda wake wa kazi hapa nchini
 Kinana akimkaribsha Lopez kuketi
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Cuba, Jorge Luis Lopez (kushoto), alipofika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kuaga kufuatia kumalizika kwa mda wake wa kazi hapa nchini
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Cuba, Jorge Luis Lopez (kushoto), alipofika leo katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, kuaga kufuatia kumalizika kwa mda wake wa kazi hapa nchini Kulia ni Ofisa wa Makao Makuu ya CCM, kutoka Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Frank Uhahula.
Ofisa wa Makao Makuu ya CCM, kutoka Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Frank Uhahula akimpa mapokezi ya awali, Balozi Lopez, kabla ya Balozi huyo kuonana na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Tuesday, 6 December 2016

MAJALIWA AZINDUA BENKI YA UCHUMI COMMERCIAL KATIKA MJI MDOGO WA KARATU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajumbe wa bodi ya Benki ya Uchumi Commercial, tawi la Karatu kabla ya kufungua benki hiyo Desemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Baadhi ya viongozi na watumishi wa Benki ya Uchumi Commercial tawi la Karatu wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  wakati alipozungumza kabla ya kufungua tawi hilo Desemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa akizungumza kabla ya kufungua Benki ya Uchumi Commercial tawi la Karatu Desemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea Benki ya Uchumi Commercial, tawi la Karatu  baada ya kuifungua Desemba 5, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya Uchumi Commercial  tawi la Karatu baada ya kuifungua Desemba 5, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Thursday, 1 December 2016

UNZI WA KIDATO CHA TATU ANUSURIKA KUFA MARA BAADA YA KUBWAKWA NA KUTELEKEZWA KORONGONI

Image result for KAMANDA WA POLISI
ARUSHA MKUMBO
Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Charles Mkumbo
Na Woinde Shizza,Meru

MWANAFUNZI wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari Kitefu iliyopo
Meru  mkoani Arusha amenusurika kufa mara baada ya kubakwa na kuteketezwa
kwenye  korongo la mchanga na kusababishiwa  maumivu makali
yaliyomsababishia kushindwa kuendelea na masomo yake kwa muda.

Akielezea tukio hilo  mwanafunzi huyo ambae amehifadhiwa jina kwa sababu za
kimaadili alisema kuwa tukio hilo lilitokea novembar 13 majira ya saa 12.30
alipotoka kwa kinyozi.

Alisema kuwa ghafla akiwa anarudi nyumbani alikutana na mtu huyo
aliyemfanyia kitendo hicho na kuanza kumkaba shingoni na kumziba mkono ili
asitoe sauti na ndipo alipomfanyia kitendo hicho cha ukatili ambacho
kimemfanyia ashindwe kuendelea na masomo yake vizuri.

"Nilijitahidi sana kupiga kelele ila kutokana na alivyokuwa amenikaba
shingoni alinifanyia kitendo hiki kikatili ambacho kimejipelekea nishindwe
kuendelea na masomo yangu kwani baada ya vipimo nimeonekana aliniumiza
sehemu nyingi ikiwemo hata kifua changu"alisema mwanafunzi huyo.

Kwa upande wake mama mzazi wa mwanafunzi huyo aliyejitambulisha Rambikiaeli
Akyoo  alisema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili kukithiri kwa mabinti
zao ni vema serikali ikawa inawachukulia hatua mapema wanaohusika kwani
tangu akamatwe mtuhumiw huyo na kupellekwa kituoni bado hajasomewa shtaka
linalomkabili hivyo kufanya wanaohusika na vitendo hivyo kuona wako sawa
kwa vile hakuna hatua kali inayochukuliwa mapema dhidi ya matukio hayo

Nae mkuu wa shule hiyo Nkoe Nicolaus  alisema kuwa tukio hilo limemfanya
mwanafunzi huyo aathirike kisaikolojia kwani tangu afanyiwe ukatili huo
ameshindwa kiendelea na masomo yake vizuri hivyo anawashauri wazazi wa
binti huyo kumuhamisha shule hiyo na kumuhamishia nyingine ili kimbadilisha
mawazo ya kifkra.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha kitefu tanesco Samweli Matayo
alikiri kutokea kwa tukio hilo katika kitongoji chake na kusema kuwa mara
baada ya taarifa walifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa aliyetambulika kwa
jina la Wilson  Elias ambae ndie  aliyehusika na ukatili huo  na kumfikisha
katika kituo kidogo cha polisi usa river ili kukabiliana na shutuma hizo.

Kamanda wa  polisi  Charles Mkumbo amethibitisha kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo ambapo limesema
kuwa mtuhumiwa alikamatwa kwa rb namba RB/R/4250/2016  na atafikishwa
mahamani upelelezi ukikamilika.
 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube